Tabasamu la JK na utingo aliyeachwa na dereva

Tabasamu la JK na utingo aliyeachwa na dereva

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,881
Reaction score
861,449
Unapoiona semi inayoyoma barabarani, sifa sio kwa dereva pekee.

Unapoona gari la abiria limefika salama safari yake sifa na shukrani sio kwa dereva pekee.

Unapoona hesabu ya tajiri imetimia tambua nyuma ya dereva kuna msaidizi muhimu almaarufu kama konda ama kwa Kiswahel sanifu, utingo.

Makonda (sio mabarcity) ni watu muhimu sana kwenye tasnia nzima ya usafiri. Kwenye magari ya mizigo ndio wasimamizi wa kupakia na kuhakikisha mzigo umefungwa vema.

Ndio wanaosimamia service ya gari, ndio wanaojua shida zote za gari hata inapopata pancha n.k n.k, na hata dereva anapochoka ama kwenda kuosha rungu kwa mpango wa kando utingo ndio hubaki na gari.

Mabus ya mikoani tunajua dhima kubwa ya makonda kuanzia kupakia abiria mpaka ku-overtake barabarani na matangazo yote safarini na dharura.

Kwenye daladala zetu ndio unaweza kuona nguvu halisi ya makonda. Yeye ndio wa kuamrisha gari isimame ama itembee ni mshika pesa ni mpanga matumizi nk nk.

Chini ya makonda ndio kuna wasaidizi wengine wote inapotokea kutoelewana kati ya konda na dereva mambo huenda kombo. Ni wakati wa uchaguzi, kila chama kimeshapata dereva wake, na kila dereva atakuwa na utingo wake na kila utingo atakuwa na wasaidizi wake.

Wakati vyama vingine vikionekana kujipanga vema kitimu na kuwa wamoja, chama tawala kina makunyanzi mengi. Makonda na wasaidizi muhinu wanaonesha wazi hawana furaha ama hawako pamoja na dereva wa jahazi, makada wote muhimu wako kimya kabisa!

Ninini kitatokea? CCM watachezeshwa segere mwanzo mwisho, watakuwa kama YANGA na SIMBA ama SAULI na NEW FORCE
Viwanjani ni SIMBA, SIMBA, SIMBAA.

Barabarani ni SAULI, SAULI, SAULI.

Nyuma ya tabasabu la JK kuna BM anacheka!

hqdefault-1.jpg
 
Mkuu Mshana Jr kuna ukweli kiasi fulani katika uchambuzi wako. Ni kweli kuna kundi ndani ya chama Tawala haliridhiki na mambo yanavyokwenda. Na katika kura za maoni limeibuka kundi jingine la wasioridhika namna mchakato wa kuchaguana ulivyokua. Angalau hawa wa pili bado wanamatumaini pengine vikao vya juu vinaweza kurekebisha hali.

Lakini hapo ndio inapoonekana nguvu ya CCM. Wakati wa changamoto kama hizi zinazopelekea wanachama wake kutoridhika wengi wanadhani sasa CCM ama inasambaratika au inaangushwa lakini matokeo yake siku zote yanakua kinyume na matarajio hayo.

Hii inatokana na oganaizesheni yao. Nidhamu ndani ya CCM ni ya hali ya juu sana. Hata kama una manung'uniko genuine kabisa uwezekano wa kukihujumu Chama ni mdogo kwasababu ya nidhamu hiyo. Wasioridhika wamewekea utaratibu maalum wa kufuata japo una urasimu kiasi. Watanuna sawa ila inapofika kwenye kutafuta ushindi wa Chama wote wanafanya kazi kwa maslahi mapana ya Chama chao

Hii ni tofauti na vyama vingine. Inapotokea storm/dhoruba yoyote iwe ni mapungufu ya viongozi ndani ya Vyama vyao au factors za nje ya Vyama basi wanaacha kuheshimiana, wanatukanana, wanaparurana na hatimaye wanasambaratika huku wakiwa wameacha vyama/chama kikiwa kimejeruhiwa vibaya sana na mifano waweza kuipata hapo CUF tu.
 
Pia kumbuka kuna wale watakaopigwa panga na kamati kuu Kwa kile alichoita polepole "waliopitishwa na wajumbe Kwa njia ya rushwa"

Mara nyingi watu hawa wakishakatwa huwa wanarudi upande wa pili na wapambe wao yaani Kwa kifupi tutegemee mvurugano zaidi.
 
Kuosha rungu, nakerekaga asubuhi unapokutana na soksi ya baba (au unyevu unaonata nata) kwenye siti ya nyuma kabsaaaa, jioni hawa dada/mama lishe wanatoa huduma ya ziada kwa hawa makonda/dereva kimasihara sanaaaa...na wanasahau kwenda piga kura [emoji1787] [emoji1787]
Mchana daladala usiku gest[emoji1787][emoji1787][emoji1787]serving multipurpose.
 
Mchana daladala usiku gest[emoji1787][emoji1787][emoji1787]serving multipurpose

Apo unamuuliza kura yako utampa nanii anasema kwa utulivu kabsaaa SIMBA Kumbe anamwaza SAULI, asubuhi anakwambia siendi piga kuwa kwa sababu sijajiandikishaaa.

Nimeona wengi hawajajiandikisha kwa kuwa waliona kilichotokea uchaguzi wa serikali za mitaaaa. Juzi nakutana na wadau ukiongelea ka wamejiandikisha wanajikunyata ka mmbwa koko alokunjia mkia kalioni 🤣 🤣 kwa hali hiyo ya kutojiandikisha tasogea kweli.
 
Thanks kwa uchambuzi uliojaa weledi lakini kumbuka anusurikaye janga maranyingi mwishowe humtokea

Rejea hotuba ya JK pale kijijini Lupaso kwenye msiba wa Mkapa...ukipata muda sikiliza tena kwa makini kisha tafakari kile alichoongea
Kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi shamrashamra zingekuwa nyingi CCM zikiongozwa na wale vijana mahiri huku wakipewa backup na wazee leo hii si hao vijana wala wazee wao wote wako kifungoni...kifungo cha kifikra...hawana uhuru wa kufanya jambo mpaka wapate ruksa toka juu.

Bashiru huwezi kamwe kumlinganisha na Kinana...lakini Kinana wa kumsaidia Bashiru yuko wapi?

Mkapa hayupo ..je ninani atakuwa konda kwa mgombea urais wa ccm? Kikwete? Sidhani....
 
Apo unamuuliza kura yako utampa nanii anasema kwa utulivu kabsaaa SIMBAa....kumbe anamwaza SAULI, asubuhi anakwambia siendi piga kuwa kwa sababu sijajiandikishaaa

Nimeona wengi hawajajiandikisha kwa kuwa waliona kilichotokea uchaguzi wa serikali za mitaaaa.... Juzi nakutana na wadau ukiongelea ka wamejiandikisha wanajikunyata ka mmbwa koko alokunjia mkia kalioni [emoji1787] [emoji1787]...kwa hali hiyo ya kutojiandikisha tasogea kweliii
Ila kuna hardcore mmoja kaja atabadili upepo wote toka upepo mwanana mpaka ule wa kisulisuli
 
.... kuosha rungu ...... nakerekaga asubuhi unapokutana na soksi ya baba (au unyevu unaonata nata) kwenye siti ya nyuma kabsaaaa, jioni hawa dada/mama lishe wanatoa huduma ya ziada kwa hawa makonda/dereva kimasihara sanaaaa...na wanasahau kwenda piga kura [emoji1787] [emoji1787]
Na huku kadi wanayo?
 
Thanks kwa uchambuzi uliojaa weledi lakini kumbuka anusurikaye janga maranyingi mwishowe humtokea
Rejea hotuba ya JK pale kijijini Lupaso kwenye msiba wa Mkapa...ukipata muda sikiliza tena kwa makini kisha tafakari kile alichoongea
Kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi shamrashamra zingekuwa nyingi ccm zikiongozwa na wale vijana mahiri huku wakipewa backup na wazee ..leo hii si hao vijana wala wazee wao wote wako kifungoni...kifungo cha kifikra...hawana uhuru wa kufanya jambo mpaka wapate ruksa toka juu..
Bashiru huwezi kamwe kumlinganisha na Kinana...lakini Kinana wa kumsaidia Bashiru yuko wapi?

Mkapa hayupo ..je ninani atakuwa konda kwa mgombea urais wa ccm? Kikwete? Sidhani.....
Legendari Mshana, naheshimu maoni yako. Pia ngoja niitafute hiyo hotuba ya Kikwete ya Lupaso maana sikupata fursa ya kuisikia. Nisikilize mistari yake na hata kati ya mistari
 
CCM hua wanaparuana ila ukifika muda wa kupambania kombe utadhani siyo wale waliokua wanaparuana.

Kama kuna chama kupita kwake wanatarajia ugomvi wa CCM uwaboost wanakosea sana.
Not this time...hakuna kuparurana bali kuna kujitenga na kujiweka pembeni pakubwa.....wale makonda waliotukanwa na Musiba kisha akaachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote leo wataweza kweli kusimama jukwaani na kusema sisi ni wamoja?
 
Thanks kwa uchambuzi uliojaa weledi lakini kumbuka anusurikaye janga maranyingi mwishowe humtokea
Rejea hotuba ya JK pale kijijini Lupaso kwenye msiba wa Mkapa...ukipata muda sikiliza tena kwa makini kisha tafakari kile alichoongea
Kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi shamrashamra zingekuwa nyingi ccm zikiongozwa na wale vijana mahiri huku wakipewa backup na wazee ..leo hii si hao vijana wala wazee wao wote wako kifungoni...kifungo cha kifikra...hawana uhuru wa kufanya jambo mpaka wapate ruksa toka juu..
Bashiru huwezi kamwe kumlinganisha na Kinana...lakini Kinana wa kumsaidia Bashiru yuko wapi?

Mkapa hayupo ..je ninani atakuwa konda kwa mgombea urais wa ccm? Kikwete? Sidhani.....
Mkuu hao ni ma ccm kindaki ndaki usiwawekee maneno mdomoni.

Hao watu hata kama roho zao hazipendi ama hazimpendi aliyepo kwenye kiti, ni lazima wajitokeze tu kutetea hata kwa huba la kinafiki!

Maisha yao yote; furaha yao, umaarufu wao, utajiri wao ni sisiemu, hawana ubavu huo wa kukihujumu ama kumhujumu mwenyekiti kwa vyovyote vile!

Mtu hawezi kukata tawi la mti alilolikalia hata akiwa mwendawazimu hafanyagi hivyo.

Kura zinavyotosha kwa aliyeko madarakani, ndiyo mafanikio yao binafsi pia.

Sisiem ikienda horijojo ama kuangukia pua na maisha yao yatakuwa yameanguka kwa kushindo hicho hicho na yameisha.

Hao wazee wewe kumbe haujawafahamu!
 
Not this time...hakuna kuparurana bali kuna kujitenga na kujiweka pembeni pakubwa.....wale makonda waliotukanwa na Musiba kisha akaachwa bila kuchukuliwa hatua yoyote leo wataweza kweli kusimama jukwaani na kusema sisi ni wamoja?
Kuna wale wengine wanapiga jaramba nje ya uwanja, wanasema wao ni jeshi la akiba wakitakiwa kuingia uwanjani wapo tayari hata saa tisa za usiku, unawaonaje hawa hawana impact? Na sio timu ndogo kama unavyodhani. Ni wale wanaosema msipotupa tunachukua wenyewe
 
Kuna wale wengine wanapiga jaramba nje ya uwanja, wanasema wao ni jeshi la akiba wakitakiwa kuingia uwanjani wapo tayari hata saa tisa za usiku, unawaonaje hawa hawana impact?
Hebu hili tulipe muda...muda utasema na yatokanayo yatajitokeza wazi upenuni penye mwanga mkali
 
Back
Top Bottom