Tabasam la Sitta kwa wananchi au wabunge wake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabasam la Sitta kwa wananchi au wabunge wake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngekewa, Jun 18, 2010.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu hebu ioneni hii na baadae mhipatie jibu!

  Sitta amlaumu Mkulo kuchelewesha fedha Send to a friend Friday, 18 June 2010 09:31 0diggsdigg

  Salim Said

  SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta alielezea kukerwa na tabia ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo ya kucheleweshwa kwa fedha za mfuko maalum wa chombo hicho, akisema kuwa haipendezi.

  Spika Sitta alimpa Waziri Mkulo ujumbe huo jana asubuhi jana wakati wa kipindi cha maswali wakati waziri huyo wa fedha akitaka kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

  “Waziri unaondoka nilikuwa na ujumbe kidogo,” alisema Spika Sitta na kumfanya Waziri Mkulo kurejea kwenye kiti chake.

  “Mambo ya kucheleweshwa kwa fedha za mfuko maalum wa Bunge hayapendezi hata kidogo,” alisema Spika Sitta huku Mkulo akisikiliza kwa makini.

  “Hata kama unaondoka lakini lijue hilo: We nenda lakini lifanyie kazi hili ili mchana tuone watu wanatabasamu,” alisisitiza Sitta.

  Kauli hiyo ya spika ilionyesha kuwa wabunge hawakuwa wamepata posho zao. Baada ya kusema hayo Waziri Mkulo alitoka ndani ya ukumbi huo. Ulipomalizika muda wa maswali na majibu Spika Sitta alisoma orodha ndefu ya matangazo ya wageni na kazi mbalimbali za wabunge na kabla ya kumaliza, alisoma ujumbe kutoka kwa Waziri Mkulo.

  “Waheshimiwa wabunge nimepata ujumbe kutoka kwa Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapha Mkulo kwamba mambo yamekamilishwa,” alisema Spika Sitta na kuongeza: “Yale mambo... yale nadhani mnayajua, yamekamilika leo (jana) na kesho (leo) watu watafurahi.
  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
  [​IMG] [​IMG] [​IMG]
   
 2. K

  Kagasheki Member

  #2
  Jun 21, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Spika nae amekuwa mtu wa maslahi zaidi pamoja na kuhubiri kasi na viwango ambavyo vimemshinda kutekeleza ndani ya chombi hicho.Sasa tunapokaribia uchaguzi na wanajua hawawezi kushinda bila kutumia hela ndipo inapowalazimu kumshurutisha Mkulo kuwapatia fedha hizo hivi sasa ili waweze kuandaa mazingira mazuri ya kuhonga wapiga kura mapema kabla ya kampeni kuanza.Kimsingi Siasa imekuwa ni ajira nzuri na bora sana kwa watafuta mafanikio na utajiri wa muda mfupi maana unawekeza kiasi cha wastani lakini mwishoni unaambulia manono yasiyofikirika.Nafikiri mwaka huu hali itakuwa mbaya zaidi kwa wagombea wapya kwenye majimbo
   
Loading...