Taasisi za Tanzania ambazo zijiandae kufa Raila akiwa Rais wa Kenya

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Zifuatazo kwa uchache ni taasisi ambazo zijiandae kuzorota (siyo kufa asilani) kwa ushindani mkali ambao haujawahi kutokea EAC na Afrika kwa ujumla.

TPA
Tayari kwa ushirika na serikali ya Uhuru, Kisumu Port imejengwa Ultra-modern kuliko Musoma, Mwanza, Kemondo Bay, Bkb na Port bell, akiingia Ikulu nguvu inahamia Mombasa ambayo ni EAC gateway.

SGR
Kuna mikakati mikali ya ushindani ambayo imepangwa kuendeleza SGR toka Nairobi kwenda Kisumu hadi Busia, Uganda itaunga toka Busia hadi Kampala. Rwanda itashawishiwa hata kwa kuahidiwa investment incentives iunge SGR toka Kampala hadi Kigali.

ATCL
Tayari KQ imechukuwa kwa mkataba SAA na sasa hivi ndege zote za KQ na hizo za SAA ukipanda kuingia EAC lzm lzm kwanza utue JKIA. Naona dalili za KQ kuichukuwa pia ATCL na sasa KQ itakuwa na SAA na ATCL na kuipa ushindani Ethiopian Airways. ATC iliwahi kuchukuliwa na SAA.

TANESCO
Kenya ni potential customer wa umeme EAC, km JNHEP ikiendelea at a snail's pace, ili kuharakisha uchumi wa Kenya, Raila ataelekea Uganda kununua umeme. Uganda inaongoza kwa idadi kubwa ya miradi EAC: Muzizi Hydro Power Sttn 44.7MW, Isimba Hydro Power Sttn 183MW, Karuma Hydro Power Sttn 600MW, Nalubaale Power Sttn (zamani Owen Falls Dam. Nalubaale ni istilahi ya Luganda inayomaanisha ziwa Victoria) inachangia kwy gridi ya taifa 180MW, Kiira Power Sttn 200MW. Bujagali Falls Hydropower Dam Jinja 250MW. Wakati JNHEP inapigwa vita na wanamazingira wa ndani na nje ya JMT, mto Nile una miradi 25 mingi ikiwa Uganda. Tz gesi inasuasua, Kinyerezi idadi ya phases zake zilizokusudiwa zimekwama kukamilika.

Mhe. Raila anasema anataka kuibadili Kenya ndani ya awamu moja ya uongozi wake km walivyofanya Joseph Stalin, Abeid Karume, Nelson Mandela, William Tubman, John Magufuli, Hussein Mwinyi.

Mhe. Raila anasema anataka kupunguza utegemezi kwa wafadhili wa nje, kwamba anaziona ela ziko ndani ya Kenya na anajuwa zilipo na namna atavyozipata ili zijenge Kenya.

Moja ya mbinu za msingi za kuipaisha Kenya ni ku-redress graft na ukoo wa Jaramogi Oginga ni wazuri kwy vita hiyo kwa sbb pia ni wasafi. Kibaki alipogundua ugumu wa vita ya ufisadi alikubali ushirika na Jemedari wa vita Raila (ODM na PNU) Kibaki akapata ushindi ktk medani ya ufisadi.

Mhe. Raila aliokoa fedha na ardhi za thamani kubwa.

Mhe. Raila ameahidi kutoa elimu bure kuanzia ya msingi hadi chuo kikuu kwamba Kenya ina uwezo huo.
 
Nakukumbusha tu, hayo yotee yamesemwa na wanasiasa..

Hao watu sio wa kuwaamini.
You sound a bit positive but August 9th in on the threshold, lets wait and prove beyond doubt.

Raila, UN Special Envoy (two times) and AU's High Representative for Infrastructure Development in Africa is determined to set precedence long awaited for.
 
Kwahiyo hizi taasisi zinategemea Kenya ili ziendelee na zilianzishwa kwa ajili ya Kenya na sio Tanzania
TPA inabd iingize pesa kwa jirani zetu kupitisha mizigo hapa. Sasa kama wakitupiga bao wakahamia Kenya inakula kwetu
 
Kwahiyo hizi taasisi zinategemea Kenya ili ziendelee na zilianzishwa kwa ajili ya Kenya na sio Tanzania
That is being academic.

Kwy diplomasia ya uchumi lzm ufanye ujasusi (intelligence) kujuwa mwenzio anakuathiri vipi.

Chai ya Tz inasuasua, chai ya Kericho Kenya na Mulanje Hills Malawi zinaendelea kuishi.

Kahawa za Tz zimeporomoka wkt Rwanda inaongoza Afrika kuuza Kahawa nje.

Viwanda vya minofu ya Sangara vya Tz vinasuasua wkt vya Kenya vinaendelea kufanya vzr sokoni Ulaya. Tz inamiliki 51% ya ziwa Victoria, Kenya 6% na Uganda 43%.

Vitunguuswaumu vinavyolimwa Manyara vinasindikwa Kenya kwa nembo ya Kenya.

Sekta ya nyama Tz ilikuwa haina kiwanda ila Kenya ilikuwa na viwanda vya nyama vilivyotegemea rasilimali ya ng'ombe toka Tz ambayo ni ya 2 Afrika kwa idadi ya mifugo.

Kiwanda kilichojengwa Kibaha kimekwama kuchinja ng'ombe kwa kuwa hakuna wa kukitumia. Kiwanda cha Vingunguti ni aibu tupu.

Matufaa (aples) za Njombe (the world sweetest) zinasindikwa Kenya kwa nembo ya Kenya.

Tanzanite hapo awali ilienda Ulaya kwa nembo ya Kenya na India.

Kiwanda cha karatasi Mgololo kimekufa na shamba la miti la Sao Hills kuchukuliwa na muwekezaji toka Kenya ambapo kiwanda chao cha karatasi cha Webuye Paper Mills kimenawiri kwa miti ya Sao Hills (kinaendeleza uzalishaji).

Sharubati (juice) zinazonywewa Tz ni imported lkn malighafi za majimaji ya matunda hayo zinatoka Tz.
 
Kisumu mji wangu pendwa nje ya Dar es salaam na Ikizu, Mungu ampambanie Raila Odinga awe Rais. Kwa ufupi ndiye Raisi wa kenya ni muda wa kuwekeza kisumu sasa
Mhe. Raila kupitia Governor wa Kisumu Prof. Anyang' Nyong'o (Mwandishi wa kitabu cha "Daggers in the heart of Africa") amejenga Kisumu Airport iliyokuwa mere Regional Airport kuwa International Airport lkn kuna Sangara tu pale Kisumu.

Chato Regional Airport imepigwa dongo wkt kule kuna migodi, mazao, hifadhi 6, samaki, mifugo nk. Wanasema Mchungaji mwenye maono yake akiondoka kbl ya kuyatimiza Mchungaji mgeni hawezi kuyatimiza kwa viwango vilivyokusudiwa na mbeba maono.
 
Umekosea ungepost hii huko kwenu maana sisi hatupigi kura.
Watz tunasifika nje ya mipaka yetu kwa kuwa na mawazo ya wastani kwenye mambo yanayohitaji serious actions, ndiyo maana tunapigwa kwy mikataba.

Tulipompeleka Prof. Kabudi Mambo ya Nje, wazungu hawakuamini ni Mtz kwa kuwa hawakuzoea ladha mpya ya Kabudi. Wazungu walilalamika kwamba kwy mikutano Kabudi anawapa mateso ya kubeba dictionaries 3 ili waweze kumuelewa.
 
Back
Top Bottom