Taasisi ya kidini yatetea wahalifu wa escrow

Taasisi ya kidini yatetea wahalifu wa escrow

issenye

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
3,795
Reaction score
5,255
ESCROW YAIBUA MAPYA

TAASISI ya Tanzania Islamic Peace Foundation (TIPF), imesema sakata la kashfa ya uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, limegeuzwa kuwa mtaji wa kisiasa zaidi.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Shekhe Sadiki Godigodi, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, baadhi ya wagombea urais katika Mchaguzi Mkuu mwaka huu, wamejipanga kuwachafua wanasiasa wenzao kupitia sakata hilo.

Shekhe Godigodi alisema Rais Jakaya Kikwete tayari ameanza kuchukua hatua kwa watu waliotajwa kuhusika na sakata hilo na kulitolea ufafanuzi Desemba 22,2014 alipohutubia Taifa kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.

"Kama Rais Kikwete tayari amechukua hatua na kulitolea ufafanuzi, iweje leo kila kukicha watu waendelee kuchafuliwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii," alihoji.

"Taasisi yetu imefanya uchunguzi wa kina na kulifuatilia kwa karibu suala la Escrow na kubaini suala hili lipo kisiasa zaidi kuliko uhalisia wenyewe.

"Utafiti wetu umeanzia katika ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambayo imeeleza wazi kuwa kampuni ya VIP iliuza hisa zake asilimia 30 kwa halali, kulipa kodi na haimchagulii Bw. James Rugemalira marafiki wala kumpangia utaratibu wa kuzitumia fedha zake," alisema.

Aliongeza kuwa, kutokana na maelezo ya PAC ni wazi kuwa hakuna kosa lolote la viongozi wa dini, wanasiasa na watu wengine waliopewa fedha na Bw. Regemalira kwa makubaliano wanayoyajua wenyewe.

Alisema kitendo cha viongozi na wanasiasa kuomba misaada kutoka kwa watu, kampuni na taasisi mbalimbali ili kutatua kero za wapigakura ni jambo la kawaida kwani mara nyingi wamekuwa wakipewa misaada ya fedha, bati, nondo, saruji, vifaa vya michezo.

"Kama ukweli ndio huo, iweje leo wanasiasa na viongozi waliopewa fedha na Bw. Rugemalira wasakamwe...tulichokiona, hapa ajenda kuwa na mambo ya kisiasa, tunampongeza Rais Kikwete kwa umakini wake wa kutekeleza maazimio ya Bunge.

"Rais Kikwete ametumia vizuri madaraka yake kwa kuheshimu misingi ya utawala bora ikiwa ni pamoja na kutomhukumu mtu bila kumpa nafasi ya kujitetea ndio maana akaagiza uchunguzi ufanyike ili aweze kujiridhisha kama wana makosa au ni uzishi," alisema Shekhe Godigodi.

Aliishauri mihimili mingine Bunge na Mahakama, iige busara na hekima za Rais Kikwete kwa kufanya uchunguzi wa kina, kuwahoji watuhumiwa na aliyewapa fedha kabla ya kuwahukumu badala ya kukurupuka kuwaadhibu.

Shekhe Godigodi alitoa wito kwa Watanzania kuwa makini kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu kwani mengi yatasikika yakiwa na lengo la kuwachafua baadhi ya watu wanaoonekana kuwa na mvuto katika jamii kwa uzalendo na uadilifu wao.



Chanzo: Gazeti majira
 
Pole sana Shekhe, uenda ujui kinachoendelea. Endelea kuwatetea CCM
 
Tehe tehe tehe, sheikh amenikumbusha mbali sana enzi zile za sheikh mtopea na imamu wake mh. Lyatonga sasa huyu sijui imamu wake ni nani lakini tutamjua tu tusubiri
 
Hili soo la eskoroo linachanganya sana(and this confusion was made intentionally and planned)Mkuu wa nchi alikiri linachanganya na haya matamko yanazidi kuchanganya tu. Na kwa mchanganyiko huu wenye haki watapoteza haki zao.
 
Tunaposema elimu dunia ni muhimu kwa viongozi wetu wa dini, ni katika mazingira kama haya.
 
Tatizo lenu ni pale mtu anapotofautiana nanyi kumwona kama mwenda wazimu.WATU WENGI NA HUSUSANI WENYE AKILI WANALIONA KUWA SWALA LA ESCROW SIO TU LA KISIASA ZAIDI BALI VISA NA CHUKI.HAYO YA SHEHE NI NYONGEZA NA WENGI TULIO MAKINI TUNAAMINI HVYO(NA HATUUNGI MKONO C C M).
 
Hujakosea kaka maana umeonyesha udhaifu wa dini yenu maana wahusika wote ni wa dini yenu pamoja viongozi wenu,je hiyo ndio elimu waliofunzwa huko. Point zingine ni sawa na toilet paper kwani una lazima ya kucomment?
Sisi katika dini yetu uwezi kukuta kiongozi wa dini asiye na elimu,lazima kwanza uende elimu dunia ya kutosha ndio uwe kiongozi wa dini,nadhani tofauti iko hapo.
 
Hujakosea kaka maana umeonyesha udhaifu wa dini yenu maana wahusika wote ni wa dini yenu pamoja viongozi wenu,je hiyo ndio elimu waliofunzwa huko?. Point zingine ni sawa na toilet paper kwani una lazima ya kucomment?
Sisi katika dini yetu uwezi kukuta kiongozi wa dini asiye na elimu,lazima kwanza uende elimu dunia ya kutosha ndio uwe kiongozi wa dini,nadhani tofauti iko hapo.
 
Tunaposema elimu dunia ni muhimu kwa viongozi wetu wa dini, ni katika mazingira kama haya.[/QUOyE]


Tatizo lenu ni pale mtu anapotofautiana nanyi kumwona kama mwenda wazimu.WATU WENGI NA HUSUSANI WENYE AKILI WANALIONA KUWA SWALA LA ESCROW SIO TU LA KISIASA ZAIDI BALI VISA NA CHUKI.HAYO YA SHEHE NI NYONGEZA NA WENGI TULIO MAKINI TUNAAMINI HVYO(NA HATUUNGI MKONO C C M).

Mkuu na wewe upo MAKINI? Hebu niambie nini sio siasa katika maisha ya mwanadamu. Watu waliomakini hawawezi kudanganyika na propaganda za kudai kuna mambo ya siasa na mambo yasiyo ya siasa. kula, kunywa kulala, kuvaa, kutembea, kuzaana, mahusiano, kuabudu nk nk nk (taja na mengine mengi), halafu wewe unayedhani upo makini uniambie nini hapo hakiathiriwi na siasa.
CHUKI Binafsi zipi kwenye ESCROW? Rais ana chuki na Tibaijuka au?
 
hapa inakuwa dini shamba, yaani dini inakuwa chanzo cha mapato kama yale ya kilimo
 
Baadhi yao ni kitu rahisi sana baada ya kukaribishwa ubwabwa na kushikishwa mgao mnene. Wengi wanaojiita "viongozi wa kidini" hawana sifa hata moja ya kuwaongoza waumini wa dini yoyote ile.

Kutetea wezi wa escrow kunahitaji moyo wa kiwendawazimu hasa ukiwa kiongozi wa dini
 
Baadhi yao ni kitu rahisi sana baada ya kukaribishwa ubwabwa na kushikishwa mgao mnene. Wengi wanaojiita "viongozi wa kidini" hawana sifa hata moja ya kuwaongoza waumini wa dini yoyote ile.
BAK acha waumini hata kuongoza kundi la panyaroad ni shida
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Pamoja nan nja yake kubwa zaidi ni Elimu ndogo sana
 
Back
Top Bottom