Taasisi ya kidini yatetea wahalifu wa escrow

Taasisi ya kidini yatetea wahalifu wa escrow

Sheikh Godigodi umekula kiasi gani kumzidi Kilaini?... Jina la Waislam usilitumie kwenye maoni Binafsi ... Pleaseeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Sisi katika dini yetu uwezi kukuta kiongozi wa dini asiye na elimu,lazima kwanza uende elimu dunia ya kutosha ndio uwe kiongozi wa dini,nadhani tofauti iko hapo.

Ni kwa sababu dini yenyewe imebuniwa na WATU wenye elimu ya dunia tu.
 
Tunaposema elimu dunia ni muhimu kwa viongozi wetu wa dini, ni katika mazingira kama haya.[/QUOyE]


Tatizo lenu ni pale mtu anapotofautiana nanyi kumwona kama mwenda wazimu.WATU WENGI NA HUSUSANI WENYE AKILI WANALIONA KUWA SWALA LA ESCROW SIO TU LA KISIASA ZAIDI BALI VISA NA CHUKI.HAYO YA SHEHE NI NYONGEZA NA WENGI TULIO MAKINI TUNAAMINI HVYO(NA HATUUNGI MKONO C C M).

Ukitaka kujua akili ya huyo Shekh,mkumbushe kuhusu MOU;atakurupuka na kutoa matamko ya ajabu.Kwa ufupi ni wepesi sana kutumika hawa jamaa.
 
Mmoja wapo wewe unyenufaika na pesa za Mengi kuendeleza kuchafua watu kwa ishu ya escrow kutwa kucha.

Hahahahaha nyani haoni ku...nd..ule. may be upo sahihi ila niwe mkweli kwamba si shikamani na upande wowote ..mi nasimama kwenye ukweli.Duh mkuu hii ya leo kali
 
ESCROW YAIBUA MAPYA

TAASISI ya Tanzania Islamic Peace Foundation (TIPF), imesema sakata la kashfa ya uchotwaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, limegeuzwa kuwa mtaji wa kisiasa zaidi.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Shekhe Sadiki Godigodi, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa, baadhi ya wagombea urais katika Mchaguzi Mkuu mwaka huu, wamejipanga kuwachafua wanasiasa wenzao kupitia sakata hilo.

Shekhe Godigodi alisema Rais Jakaya Kikwete tayari ameanza kuchukua hatua kwa watu waliotajwa kuhusika na sakata hilo na kulitolea ufafanuzi Desemba 22,2014 alipohutubia Taifa kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.

“Kama Rais Kikwete tayari amechukua hatua na kulitolea ufafanuzi, iweje leo kila kukicha watu waendelee kuchafuliwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,” alihoji.

“Taasisi yetu imefanya uchunguzi wa kina na kulifuatilia kwa karibu suala la Escrow na kubaini suala hili lipo kisiasa zaidi kuliko uhalisia wenyewe.

“Utafiti wetu umeanzia katika ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambayo imeeleza wazi kuwa kampuni ya VIP iliuza hisa zake asilimia 30 kwa halali, kulipa kodi na haimchagulii Bw. James Rugemalira marafiki wala kumpangia utaratibu wa kuzitumia fedha zake,” alisema.

Aliongeza kuwa, kutokana na maelezo ya PAC ni wazi kuwa hakuna kosa lolote la viongozi wa dini, wanasiasa na watu wengine waliopewa fedha na Bw. Regemalira kwa makubaliano wanayoyajua wenyewe.

Alisema kitendo cha viongozi na wanasiasa kuomba misaada kutoka kwa watu, kampuni na taasisi mbalimbali ili kutatua kero za wapigakura ni jambo la kawaida kwani mara nyingi wamekuwa wakipewa misaada ya fedha, bati, nondo, saruji, vifaa vya michezo.

“Kama ukweli ndio huo, iweje leo wanasiasa na viongozi waliopewa fedha na Bw. Rugemalira wasakamwe...tulichokiona, hapa ajenda kuwa na mambo ya kisiasa, tunampongeza Rais Kikwete kwa umakini wake wa kutekeleza maazimio ya Bunge.

“Rais Kikwete ametumia vizuri madaraka yake kwa kuheshimu misingi ya utawala bora ikiwa ni pamoja na kutomhukumu mtu bila kumpa nafasi ya kujitetea ndio maana akaagiza uchunguzi ufanyike ili aweze kujiridhisha kama wana makosa au ni uzishi,” alisema Shekhe Godigodi.

Aliishauri mihimili mingine Bunge na Mahakama, iige busara na hekima za Rais Kikwete kwa kufanya uchunguzi wa kina, kuwahoji watuhumiwa na aliyewapa fedha kabla ya kuwahukumu badala ya kukurupuka kuwaadhibu.

Shekhe Godigodi alitoa wito kwa Watanzania kuwa makini kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu kwani mengi yatasikika yakiwa na lengo la kuwachafua baadhi ya watu wanaoonekana kuwa na mvuto katika jamii kwa uzalendo na uadilifu wao.



Chanzo: Gazeti majira


Kwani BAKWATA si chama cha kisiasa,inamaana mlikuwa hamjui hilo?na ujue hawa jamaa wanamatatizo,ngoja CCM impitishe mkristo kugombea urais ndo utaamini ninachokisema hapa,let us wait and see
 
Back
Top Bottom