Taasisi ya China-Afrika kufungua vituo vitano Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Gianna Amani
Taasisi ya China-Africa (CAI) ambayo inajihusisha zaidi na utafiti wa masuala yanayohusu uhusiano kati ya China na Afrika imesema inatarajia kufungua vituo vitano barani Afrika ili kusogeza huduma karibu kwa Waafrika.

Akizungumza na waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika waliotembelea makao makuu ya taasisi hiyo mjini Beijing, Mkuu Mtendaji wa CAI Li Xinfeng amewaeleza kuwa kila ukanda (Mashariki, Kusini, Magharibi, Kaskazini na Kati) kutakuwa na kituo kimoja hivyo.

“Kuna nchi tano zitachaguliwa kuwekwa vituo hivyo ili kusogeza huduma lakini si hivyo tu, tutaendelea kuboresha uhusiano wetu na wanazuoni kutoka nchi zote za Afrika ili kuboresha tafiti zetu kwa maslahi ya watu,” alisema Xinfeng.

Alisema CAI itaendelea kuboresha na kuongeza mchango wake wa kitaaluma katika kutafuta suluhu ya masuala mbalimbali yanayohusu China na Afrika. “Kazi yetu kubwa ni kufanya utafiti na kupitia utafiti huo tunatoa ushauri kwa Serikali za nchi za Afrika na China kuhusu masuala mbalimbali”.

Itakumbukwa kuwa uhusiano wa China na Afrika ulianza miaka ya 1960, baada ya takribani nchi 10 za Kiafrika kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Jamhuri ya watu wa China na nyingi zilikuwa ni zile zilizofuata siasa za mrengo wa kushoto, zikiwemo Algeria, Misri na Guinea.

Tangu wakati huo hadi sasa uhusiano kati ya China na Afrika katika nyanja tofauti hususani za kiuchumi na kidiplomasia umekuwa ukiimarika zaidi na CAI imekuwa ikitoa mchango mkubwa kwa pande zote mbili kwa zaidi ya miongo saba iliyopita kupitia tafiti zake.

图像_2022-11-03_095639367.png
 
View attachment 2405462
Asante sana
 
karibuni china ila uwepo wenu kwetu uwe na masilahi sio munufaike nyie tu
 
Back
Top Bottom