Taasisi huru za kiraia kuchagia mabadliko makubwa uchaguzi 2015

Membensamba

Senior Member
Nov 4, 2010
157
10
Hali ilivyo sasa nchini Tz, Inaonekana kwamba adui mkubwa wa mabadiliko tunayoyahitaji ni ujinga wa watz walio wengi. Mfumo wa chama kimoja bado ungalipo vichwani mwa watanzania. Hawajafahamu umuhimu wa siasa katika maisha yao na mustakabali wa taifa lao. Kwa sababu hiyo hata wanaojitokeza kupiga kura ni wachache. Na wanaojitokeza hawapigi kura kwa kuzingatia sera na uwezo wa chama na/au wagombea bali kwa ushabiki tu kama ule wa simba na yanga. Wapo watz leo ambao hata kama ccm ikiwaahidi kuwaongozea umaskini wazi wazi katika ilani yake bado wataichagua. Hii ni kwa sababu ya uhafidhina uliopindukia.

Ipo haja kubwa ya elimu sio tu ya kawaida ya uraia kutolewa bali elimu inayolenga kuleta ukombozi wa kifikra wenye lengo la kuleta mwamko mkubwa wa kisiasa. Watza wengi sio wa kulaumiwa kwa hali waliyo nayo. Ni wa kuhurumiwa, kwa kuwa ni wahanga wa ujinga uliotengenezwa (engineered ignorance) Ikumbukwe kuwa huu ujinga wao ndio mtaji mkuu kabisa wa ccm. Vyama vya upinzani vina kazi kubwa sana ya kuwaelimisha umma juu ya umuhimu wa siasa za mabadiliko. Laikini hata nao wenyewe hawatoshi. Taasisi huru za kiraia zina nafasi ya pekee sana katika hili.

Kwanza ikumbukwe kuwa taasisi huru zina nafasi ya kupokewa na jamii bila kutazamwa kwa macho ya kisiasa (political bias) kuliko vyama vya kisiasa, na hivyo kuweza kusikilizwa hata na wahafidhina waliopindukia. Pili vikwazo wawekewavyo wanasiasa na ccm na serikali yake hawatawekewa kwa kuwa sio washindani wao wa moja kwa moja.

Hivyo umefika wakati sasa taasisi zilizopo za kiraia zi-pull up their socks, ziongeze juhudi na kuwafikia walio vijijini na mijini kutoa elimu, kufanya tafiti, na kuhusu nini kifanyike kuleta mapinduzi haya. Vyama vya ushindani kama wadau wakuu watafaidika sana na kazi yao. Lakini nao pia wana kazi ya ziada ya kuwaendea wananchi na kuwa-sensitize kuhusu umuhimu wa mabadiliko. Vikikaa tu maofisini na kusubiri 2015 ndipo viwaendee wananchi kuwaomba kura mambo yatakuwa yaleyale ya siku zote.
 
Back
Top Bottom