Taarifa za mgomo wa Wafanyabiashara nchi nzima

MZEE MSASAMBEGU

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,780
Reaction score
2,556
Wakuu nipo hapa Mbalizi Mbeya,naskia gari ya matangazo inapita kuwahamasisha wafanyabiashara leo kurudi tena na kufungua maeneo yao ya biashara.

Je, mwenyekiti wao aliyekuwa anashikiliwa na polisi kashaachiwa?

Je, mgomo umeisha?

mwanza.png
Taswira jiji la Mwanza leo
 
Wakuu nipo hapa mbalizi mbeya,naskia gari ya matangazo inapita kuwahamasisha wafanyabiashara leo kurudi tena na kufungua maeneo yao ya biashara.je mwenyekiti wao aliyekuwa anashikiliwa na polisi kashaachiwa na je mgomo umeisha?
 
Kufuatia mgomo unaoendelea, wafanyabiashara wamegoma kufungua maduka Yao baada ya kuambiwa wafungue maduka baada ya kikao kilichofanyika Jana na waziri mkuu.

Watu ni wakali wanataka minja atoke, wanasema hawataki majibu mepesi yaliyotolewa na waziri Mkuu kwamba Kodi kupanda 100% atalibeba yeye na suala la mwenyekiti atalishughulikia.

Mungu atusaidie tupate suluhu haraka ili tusiingie matatizoni.
 
Wakuu nipo hapa mbalizi mbeya,naskia gari ya matangazo inapita kuwahamasisha wafanyabiashara leo kurudi tena na kufungua maeneo yao ya biashara.je mwenyekiti wao aliyekuwa anashikiliwa na polisi kashaachiwa na je mgomo umeisha?
Mkuu nipo kariakoo leo ndio wamegoma zaidi inaonekana maazimio ya Jana na Pinda hayakufikiwa mwafaka.

Minja bado yupo ndani.
 
huku songea baada ya maduka kufungwa juzi na jana leo mapema wamefungua,,tunaendelea kupata huduma.
 
We unaejiita UAMINIFUKAZI hujui unachokiongea , na ninawasiwasi na uwezo wako wa kielimu huyu mfanyabiashara ndiye anayeuza kila kitu sasa cjui tafsiri yako ikoje? Na km wewe ni mtumishi cjui mahitaji yako utayapataje na hata Mshahara wako utajitengenezaje. Au ndo wale wale Baba mwalimu na watoto ni walimu au Baba ni askari na watoto wote ni recruit. Think wisely my friend dont allow people laughing at u
 
Agizo kutoka kwa viongozi wa wafanyabiashara nchini ni kwamba wenye maduka kufungua biashara zao lkn wafanyabiashara wamekataa hilo agizo la viongozi wao wakishinikiza mpaka wamwone Mwenyekiti wao ndio wafungue biashara,
Na kauli mbiu yao siku zote ni "MWENYEKITI KWANZA BIASHARA BAADAE".
 
I like this👇

NCHI YANGU TANZANIA;

One of the cardinal principles of Economics is Opportunity Cost. Do the fast thing first, and those which can wait let them wait.....

Hebu tujaribu kufanya hesabu ndogo za kugawanya na kuzidisha za darasa la tano. Ni hivi, wabunge wawili walioteuliwa watalipwa mishahara ya miezi mitano bure maana hatutegemei jipya watakalolifanya huko bungeni. Mshahara kwa mbunge mmoja ni Mil.11 mara miezi mitano watakayofanya kazi ni jumla ya Sh.Mil 55 kwa kila mmoja. Kwa wote wawili ni Mil.110.

Wabunge hawa walioteuliwa leo watalipwa kiinua mgongo kwa viwango vya wabunge wa kawaida Sh.Mil.90 kila mmoja ifikapo tar.31 mwezi July mwaka huu. Kwa wote wawili ni Mil.180.

Taarifa ya Ikulu inasema uteuzi wao unaanza tarehe 20, hivyo basi kuanzia tar.21 wataanza kulipwa posho za vikao vya bunge kwa siku 10 zilizobakia kwenye bunge hili linaloendelea. Posho ya siku moja ni Sh.330,000/= kwa siku kumi ni Mil.3 na laki 3.

Kwenye bunge la bajeti Watalipwa posho ya 330,000/= kwa siku. Bunge hilo litatumia jumla ya siku 60. Hivyo mbunge mmoja atalipwa Mil.19 na laki 8, kwa muda wote wa bunge la bajeti. Kwa wote wawili watalipwa mil.39 na laki 6.

Wabunge hawa "watakopeshwa" magari ya kifahari ya kutembelea. Yani kama walikua wakitumia usafiri wa umma, kuanzia tar.20 March wameambiwa stop. Watapanda Mashangingi yanayokadiriwa kugharimu Mil.120 kwa moja, kwa wote wawili ni Mil.240.

Kwa ujumla makadirio ya gharama zote za wabunge hawa wawili kwa miezi mitano tu watakayofanya kazi watatumia jumla ya Shilingi Milioni 573 na laki 2.

Pesa hizi zinatosha kulipia mikopo ya elimu ya juu kwa semester moja kwa wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza Chuo kikuu cha St.Augustine, au Chuo Kikuu Dodoma kwa wanafunzi wanaosoma Social Science.

Pia pesa hizi zingeweza kujenga maabara za kisasa katika shule 12 Tanzania. Zingeweza kulipa mishahara ya waalimu (daraja la pili) 1,432 wa shule mbalimbali za sekondari nchini. Pia fedha hizi zingeweza kutolewa kama mkopo kwa vijana wanaohitimu vyuo vya Elimu ya juu nchini na kukosa ajira. Jumla ya vijana 573 wangenufaika kwa mkopo wa Mil.1 kila mmoja.

Lakini cha ajabu pesa zote hizi zitatumiwa na wabunge wawili tu tena kwa kipindi cha miezi mitano tu, with no expectation of return. Hatutegemei wabunge hawa watafanya lolote jipya huko bungeni litakalogharimu hizo Mil.573 watakazotumia.

Kwa lugha rahisi ni kuwa hatutegemei output ya wabunge hawa izidi input. Hakuna mbunge yeyote atakayeweza kutoa hoja zitakazo-value hizo Mil.573 watakazotumia, hata wakisaidiwa na huyo aliyewateua.

Sasa nimejiuliza, hivi katika mazingira haya ambayo hatuna rasilimali za kutosha kulinganisha na mahitaji tuliyonayo, je kulikua na ulazima wowote wa kuteua wabunge hao?

Tunahitaji pesa za kujenga maabara, kujenga shule, kulipia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mikopo, kulipa mishahara, kununua madawa etc. Lakini tumeacha vyote hivyo tumetoa kipaumbele kwa wabunge tena wa kuteuliwa.

Tafakari chukua hatua.
 
Inafika wakati nahisi hasira ata sijui sababu, jamani haya mambo nchi hii mpaka lini tunaacha mambo ya msingi tunawekeza katika mambo yasiyokuwa ya msingi. Kwa kwl ifike wakati watanzania tuseme basi
 
Hili bunge la.Ndiooooo ndio chanzo cha matatizo yote Tanzania

Wakuu nawaomba mturekebishie aina ya wabunge hasa hao wanaovaa nguo za kijani
Wahoji kwanza mambo kwa kina ndio wapitishe mengine yanaleta madhara na usumbufu kwa viongozi wakuu wa kitaifa yanapoleta shida kwa jamii
 
Mwitikio wa Mgomo wa Wafanyabiashara umekuwa mkubwa hapa Manispaa ya Mbeya. Shughuli zote za kibiashara zimesimama. Milango ya Maduka na Fremu za kawaida imebandikwa matangazo ya kuunga mkono mgomo huo. Tangazo hilo linasema "hawatafungua maduka na biashara zingine mpaka pale kiongozi wa wafanyabiashara aliyeko mahabusu atakapoachiwa".

Hali ikiendelea hivi wananchi wanaotoka sehemu za mbali vijijini wataathirika sana. Maana ni siku ya pili leo hawajapata huduma walizofuata hapa mjini.
 
Huko mikoani napo mambulula watupu huku Dar kma kawaida tunapiga miluzi tu kariakoo fungeni huku mitaani mauzo kama kawaida
 
waendelee kugoma hesabu ya kodi ya mapato inaendelea kuhesabu na riba za bank ipo palepale
 
Hali hii mbaya sana Leo Wanajeshi baada ya kufanya usafi wamebeba meza na vibanda vya wafanyabiashara wadogo sido mbeya. Inatia huruma sna
 
Back
Top Bottom