Taarifa za Ben Saa Nane kuonekana, Jeshi la Polisi lizifanyie kazi Taarifa za Kubenea

Taarifa za Mhe.Kubenea kwamba Ben yupo mtaani anarandaranda na kujificha kwa rafiki zake, ni taarifa zinazopaswa kufanyiwa kazi na Jeshi la Polisi na uongozi wa Chadema. Takribani mwezi mmoja sasa polisi na Uongozi wa Chadema umetoa taarifa rasmi za kumtafuta Ben. Leo Kubenea anasema Ben yupo mtaani, anaonekana kwenye vijiwe vya kahawa.

Ni vizuri Polisi wakamkamata Kubenea aeleze ni mitaa ipi Ben alionekana, na ni vijiwe vipi vya kahawa alivyokutwa. Je alikua na nani? ni siku gani? aliyemuona ni nani? na kwanini alipomuona hakutoa taarifa polisi? Na kwa kuwa Kubenea anajua polisi wanamtafuta kwanini alipojua Ben yupo mtaani hakwenda kuripoti polisi ili awasaidie ktk kufanya uchunguzi? Kwanini Kubenea anawaacha Polisi watumie rasilimali kubwa kumtafuta Ben wakati anajua Ben amejificha ili kujipatia umaarufu wa kisiasa?

Kubenea anasema Ben anatafuta umaarufu, je ni umaarufu gani wa kujipoteza? Ili iweje? Kwa faida ya nani? Kwamba Ben akijipoteza ndo anakua maarufu? Halafu huo umaarufu unamsaidiaje? Kugombea nafasi ya uongozi kwenye chama? Ni nafasi gani ambayo mtu huchaguliwa kwa kujipoteza? Na ni akina nani watakua wajinga wa kumpa mtu kura kwa sababu tu alijipoteza? Hivi kujipoteza kwa Ben kunamuongezea kura au kunampunguzia?

Kama kweli Ben yupo mtaani, je Kubenea haoni kuweka taarifa gazetini ni kumfanya azidi kujificha? Kwanini asingewaarifu polisi kwanza wamkamate then ndo aweke gazetini? Na hao marafiki zake Ben waliomficha huko mtaani ni mahiri wa ujasusi kiasi gani? Je wamewazidi akili polisi, usalama wa taifa na intelijensia ya Chadema? Je Kubenea kuandika habari bila kujibu maswali muhimu (5Ws +H) haoni kunaifanya habari hiyo kukosa uhalali wa kuaminika mbele ya jamii?

Na kwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mhe.Freeman Mbowe alitamka hadharani kuwa kuna uwezekano Ben ametekwa, je Kubenea kusema Ben kajificha haoni anamfanya Mbowe kuonekana ameshiriki kumficha Ben? Kwa kuwa Kubenea ameshindwa kutaja vyanzo vyake vya habari haoni habari hiyo inaweza kuonekana ni ya kutunga maana haina credible source? Je ikija kubainika kuwa Ben ametekwa au amekufa, je Kubenea haoni kwamba atakua amewakosea sana watanzania, kuikosea familia ya Ben, na hata nafsi yake mwenyewe?

Sisemi kuwa Ben hawezi jificha, as a human being anaweza kufanya hivyo na ikibainika kajificha nashauri achukuliwe hatua kali za kisheria. Lakini ukweli ni kuwa habari ya Kubenea imeacha maswali mengi kuliko majibu.

Nahofia Kubenea asije kuwa ameandika habari hiyo kwa chuki binafsi dhidi ya Ben halafu baadae akaja kujuta. Nafahamu ugomvi binafsi kati ya Ben na Kubenea uliosababishwa na tofauti za kisiasa. Kuna mengi yalitokea ambayo siwezi kuyasema yote hapa lakini Ben na Kubenea wamewahi kunyukana kwa nyakati tofauti kwa sababu mbalimbali (ushahidi wa maandishi yao wakinyukana upo).

Sasa isije kuwa Kubenea anaendeleza mnyukano kati yake na Ben akasahau suala la uhai wa mtu ni muhimu kuliko tofauti zao za kisiasa. Ikibainika Ben amejificha Kubenea atakua shujaa kwenye hili, lakini ikija kubainika kuwa Ben amekufa, kuuawa au kutekwa, dhamiri ya Kubenea itamhukumu maisha yake yote. Ni vizuri kuwa na akiba ya maneno.!

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG].!

Malisa GJ
Sasa nyie vichwa maji wa bawacha kwanini msimkamate kubenea na kumpeleka polisi atoe maelezo? kwanini mnalazimisha polisi wamkamate kubenea? Kubenea ni Mbunge wa ubungo kupitia chadema mmeshindwa kumuhoji? leo ndio mnaona umuhimu wa polisi? Nyie si ndio mlisema mna intelijensia hatari ya kubaini hata mawasiliano ya watu? hahahaha acheni Maigizo tunaomba mumulize kwanza Mbowe ni wapi alipo Ben saanane? Kubenea na Mbowe wanajua alipo Ben ndio maana wameanza na gia ya kusema kaonekana......kiki ya kisiasa imeshindika sasa ni lazima watafute njia ya kumrudisha hahahah
 
ACHA WAFU WAZIKANE WENYEWE MKUU
 
Naona harakati za watu kutafuta umaarufu mitandaoni zimepamba moto sasa,anyways ndugu wakigombana.......!
 
Taarifa za Mhe.Kubenea kwamba Ben yupo mtaani anarandaranda na kujificha kwa rafiki zake, ni taarifa zinazopaswa kufanyiwa kazi na Jeshi la Polisi na uongozi wa Chadema. Takribani mwezi mmoja sasa polisi na Uongozi wa Chadema umetoa taarifa rasmi za kumtafuta Ben. Leo Kubenea anasema Ben yupo mtaani, anaonekana kwenye vijiwe vya kahawa.

Ni vizuri Polisi wakamkamata Kubenea aeleze ni mitaa ipi Ben alionekana, na ni vijiwe vipi vya kahawa alivyokutwa. Je alikua na nani? ni siku gani? aliyemuona ni nani? na kwanini alipomuona hakutoa taarifa polisi? Na kwa kuwa Kubenea anajua polisi wanamtafuta kwanini alipojua Ben yupo mtaani hakwenda kuripoti polisi ili awasaidie ktk kufanya uchunguzi? Kwanini Kubenea anawaacha Polisi watumie rasilimali kubwa kumtafuta Ben wakati anajua Ben amejificha ili kujipatia umaarufu wa kisiasa?

Kubenea anasema Ben anatafuta umaarufu, je ni umaarufu gani wa kujipoteza? Ili iweje? Kwa faida ya nani? Kwamba Ben akijipoteza ndo anakua maarufu? Halafu huo umaarufu unamsaidiaje? Kugombea nafasi ya uongozi kwenye chama? Ni nafasi gani ambayo mtu huchaguliwa kwa kujipoteza? Na ni akina nani watakua wajinga wa kumpa mtu kura kwa sababu tu alijipoteza? Hivi kujipoteza kwa Ben kunamuongezea kura au kunampunguzia?

Kama kweli Ben yupo mtaani, je Kubenea haoni kuweka taarifa gazetini ni kumfanya azidi kujificha? Kwanini asingewaarifu polisi kwanza wamkamate then ndo aweke gazetini? Na hao marafiki zake Ben waliomficha huko mtaani ni mahiri wa ujasusi kiasi gani? Je wamewazidi akili polisi, usalama wa taifa na intelijensia ya Chadema? Je Kubenea kuandika habari bila kujibu maswali muhimu (5Ws +H) haoni kunaifanya habari hiyo kukosa uhalali wa kuaminika mbele ya jamii?

Na kwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mhe.Freeman Mbowe alitamka hadharani kuwa kuna uwezekano Ben ametekwa, je Kubenea kusema Ben kajificha haoni anamfanya Mbowe kuonekana ameshiriki kumficha Ben? Kwa kuwa Kubenea ameshindwa kutaja vyanzo vyake vya habari haoni habari hiyo inaweza kuonekana ni ya kutunga maana haina credible source? Je ikija kubainika kuwa Ben ametekwa au amekufa, je Kubenea haoni kwamba atakua amewakosea sana watanzania, kuikosea familia ya Ben, na hata nafsi yake mwenyewe?

Sisemi kuwa Ben hawezi jificha, as a human being anaweza kufanya hivyo na ikibainika kajificha nashauri achukuliwe hatua kali za kisheria. Lakini ukweli ni kuwa habari ya Kubenea imeacha maswali mengi kuliko majibu.

Nahofia Kubenea asije kuwa ameandika habari hiyo kwa chuki binafsi dhidi ya Ben halafu baadae akaja kujuta. Nafahamu ugomvi binafsi kati ya Ben na Kubenea uliosababishwa na tofauti za kisiasa. Kuna mengi yalitokea ambayo siwezi kuyasema yote hapa lakini Ben na Kubenea wamewahi kunyukana kwa nyakati tofauti kwa sababu mbalimbali (ushahidi wa maandishi yao wakinyukana upo).

Sasa isije kuwa Kubenea anaendeleza mnyukano kati yake na Ben akasahau suala la uhai wa mtu ni muhimu kuliko tofauti zao za kisiasa. Ikibainika Ben amejificha Kubenea atakua shujaa kwenye hili, lakini ikija kubainika kuwa Ben amekufa, kuuawa au kutekwa, dhamiri ya Kubenea itamhukumu maisha yake yote. Ni vizuri kuwa na akiba ya maneno.!

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG].!

Malisa GJ
Hizi taarifa alizileta kada wa Chama cha mapinduzi humu! Ukisoma kwa makini ni Kama zimetengenezwa tu hakuna kitu hapo.Mwanahalisi Online ipi mbana taarifa hazionekani? Malissa hebu fatilia kwa umakini ndugu yangu. Tunaumia sana lakini hebu tuwe na u makini Mkubwa juu ya hili.
 
Hiyo ilikuwa fake news kwa tunaojua kuziangalia fake nyuzi watajua tu

Anaonekana na marafiki zake wasio na majina,
Anaonekana sehemu isiyojulikana ni wapi ,Anaonekana muda gani hakuna
Kumbuka hiyo ni investigative news lazima iwe na ushahidi wa hayo niliyataja hapo.
Ujuaji mwingi halafu mweupe kichwani!!

Taarifa iko kwenye mtandao wa mwanahalisi we unabwatuka ni fake! Fake imejiupload huko kwenye site ya mwanahalisi?!
 
Mkuu, ni huyo huyo ambaye aliwahi kuzua kuwa Masheikh wanafanyiwa unyqnyasaji kwa kuingizwa vitu sehemu za haja kubwa. Ni huyo huyo aliyesema kuwa wabunge wanawake wa UKAWA wamevuliwa shanga na chupi

Mkuu Lizaboni.

Umetupia rejea matata sana.

Huu mwendo wanaoenda nao CHADEMA ni mwendo mpya.

Haiyumkini ukatufikisha kwenye rangi, sura na hali halisi ya chama hiki kinachojinasibu kwa Demokrasia na Maendeleo.
 
Hiyo ilikuwa fake news kwa tunaojua kuziangalia fake nyuzi watajua tu

Anaonekana na marafiki zake wasio na majina,
Anaonekana sehemu isiyojulikana ni wapi ,Anaonekana muda gani hakuna
Kumbuka hiyo ni investigative news lazima iwe na ushahidi wa hayo niliyataja hapo.
Kasome mwanahalisi ya J3
 
Ukishapewa lead of direction fanyia kazi if you choose to follow it or ignore kwenye investigation zako sasa ni wewe unaelipwa na serikari. Ebu tuache hizi tabia za kushabikia intimidation kwa waandishi siku zingine watu watakaa kimya tu; polisi wenyewe tayari awana sifa ya urafiki kwenye jamii.
 
Hizi taarifa alizileta kada wa Chama cha mapinduzi humu! Ukisoma kwa makini ni Kama zimetengenezwa tu hakuna kitu hapo.Mwanahalisi Online ipi mbana taarifa hazionekani? Malissa hebu fatilia kwa umakini ndugu yangu. Tunaumia sana lakini hebu tuwe na u makini Mkubwa juu ya hili.

Bofya hii link hapa ni ya mwanahalisionline. Ukaoshe hizo tongotongo zako.
Utata mpya msaidizi wa Mbowe
 
Kubenea bana....Mtoto aliyezoea kuwaibia majirani sasa amenza kuiba ndani kwao.
 
hata Yesu alijipoteza tukaambiwa amekufa baadae alivyojitokeza tukaambiwa amefufuka!!! [HASHTAG]#duniainamambo[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom