Taarifa za Ben Saa Nane kuonekana, Jeshi la Polisi lizifanyie kazi Taarifa za Kubenea

Hakuna haja ya kulihusisha jeshi la polisi na upuuzi huo. Halafu pia Ben hawezi kukutwa na hatia kwa kujificha kwake; ila wale walitumia mapumziko ya Ben kuleta taharuki kwa watu na kuichafua serikali.
Ina maana ni kweli yupo mitaani anaonekana?
 
Owkay, nimeliona mkuu! Mwanzo sikuelewa bizuri. Mimi nafikiri kwa hili naungana na Malissa kua Kubenea akamatwe ohojiwe aeleze anamuona wapi Beni?
Kumbuka kubenea ni mmiliki na ni mhariri mkuu wa hilo gazeti kama sijakosea na PIA NI MKURUGENZI WA FEDHA ndani ya CHADEMA hivyo Mbowe na watu wake wanapaswa kutake initiatives mapema
Na wala sio gazeti la chadema....
ila ni gazeti la Mkurugenzi wa Fedha wa CHADEMA
 
mie sijaiangalia hii topic yote ila,

from the first post,mtoa mada mbona hujatoa source ya habari yako,unamtuhumu Kubenea ambayo ni sawa,ila ingependeza kama ungeonyesha sehemu aliyoandika au kama ungeweza ungeweka link,ya aliyoyaandika.Thanks.

BEN-SAANANE-620x308.jpg

Bernard Saanane, Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema
Utata mpya msaidizi wa Mbowe
 
Taarifa za Mhe.Kubenea kwamba Ben yupo mtaani anarandaranda na kujificha kwa rafiki zake, ni taarifa zinazopaswa kufanyiwa kazi na Jeshi la Polisi na uongozi wa Chadema. Takribani mwezi mmoja sasa polisi na Uongozi wa Chadema umetoa taarifa rasmi za kumtafuta Ben. Leo Kubenea anasema Ben yupo mtaani, anaonekana kwenye vijiwe vya kahawa.

Ni vizuri Polisi wakamkamata Kubenea aeleze ni mitaa ipi Ben alionekana, na ni vijiwe vipi vya kahawa alivyokutwa. Je alikua na nani? ni siku gani? aliyemuona ni nani? na kwanini alipomuona hakutoa taarifa polisi? Na kwa kuwa Kubenea anajua polisi wanamtafuta kwanini alipojua Ben yupo mtaani hakwenda kuripoti polisi ili awasaidie ktk kufanya uchunguzi? Kwanini Kubenea anawaacha Polisi watumie rasilimali kubwa kumtafuta Ben wakati anajua Ben amejificha ili kujipatia umaarufu wa kisiasa?

Kubenea anasema Ben anatafuta umaarufu, je ni umaarufu gani wa kujipoteza? Ili iweje? Kwa faida ya nani? Kwamba Ben akijipoteza ndo anakua maarufu? Halafu huo umaarufu unamsaidiaje? Kugombea nafasi ya uongozi kwenye chama? Ni nafasi gani ambayo mtu huchaguliwa kwa kujipoteza? Na ni akina nani watakua wajinga wa kumpa mtu kura kwa sababu tu alijipoteza? Hivi kujipoteza kwa Ben kunamuongezea kura au kunampunguzia?

Kama kweli Ben yupo mtaani, je Kubenea haoni kuweka taarifa gazetini ni kumfanya azidi kujificha? Kwanini asingewaarifu polisi kwanza wamkamate then ndo aweke gazetini? Na hao marafiki zake Ben waliomficha huko mtaani ni mahiri wa ujasusi kiasi gani? Je wamewazidi akili polisi, usalama wa taifa na intelijensia ya Chadema? Je Kubenea kuandika habari bila kujibu maswali muhimu (5Ws +H) haoni kunaifanya habari hiyo kukosa uhalali wa kuaminika mbele ya jamii?

Na kwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mhe.Freeman Mbowe alitamka hadharani kuwa kuna uwezekano Ben ametekwa, je Kubenea kusema Ben kajificha haoni anamfanya Mbowe kuonekana ameshiriki kumficha Ben? Kwa kuwa Kubenea ameshindwa kutaja vyanzo vyake vya habari haoni habari hiyo inaweza kuonekana ni ya kutunga maana haina credible source? Je ikija kubainika kuwa Ben ametekwa au amekufa, je Kubenea haoni kwamba atakua amewakosea sana watanzania, kuikosea familia ya Ben, na hata nafsi yake mwenyewe?

Sisemi kuwa Ben hawezi jificha, as a human being anaweza kufanya hivyo na ikibainika kajificha nashauri achukuliwe hatua kali za kisheria. Lakini ukweli ni kuwa habari ya Kubenea imeacha maswali mengi kuliko majibu.

Nahofia Kubenea asije kuwa ameandika habari hiyo kwa chuki binafsi dhidi ya Ben halafu baadae akaja kujuta. Nafahamu ugomvi binafsi kati ya Ben na Kubenea uliosababishwa na tofauti za kisiasa. Kuna mengi yalitokea ambayo siwezi kuyasema yote hapa lakini Ben na Kubenea wamewahi kunyukana kwa nyakati tofauti kwa sababu mbalimbali (ushahidi wa maandishi yao wakinyukana upo).

Sasa isije kuwa Kubenea anaendeleza mnyukano kati yake na Ben akasahau suala la uhai wa mtu ni muhimu kuliko tofauti zao za kisiasa. Ikibainika Ben amejificha Kubenea atakua shujaa kwenye hili, lakini ikija kubainika kuwa Ben amekufa, kuuawa au kutekwa, dhamiri ya Kubenea itamhukumu maisha yake yote. Ni vizuri kuwa na akiba ya maneno.!

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG].!

Malisa GJ
Unazungumzia Kubenea wa Mwanahalisi yupii kamanda ? Yule aliyetuaminisha kupitia magazeti yake kwa zaid ya miaka nane kuwa Lowasa ni fisadi papa.
 
Mwishowe mtatuambia na Kubenea ni mtu wa 'Kitengo' .... kama mlivyoanza kutuaminisha kwa Zitto na wengineo

Hii vita ya mabwana, watwana kaeni mbali
 
Hivi hata km kubenea kasema uongo mnataka akamatwe kwa kosa gani!!? Issue ya saa nane inakuzwa na bavicha tu,lkn siyo issue yenye uzito huo unaoelezwa. Ben ni mtu mzima,hawezi kupotea na hata police hawana wajibu wa kumtafuta.

Hata kwa akili ya kawaida tu,police watamtafutia wapi mtu mzma ambae anaweza kwenda popote bila kuulizwa wala kuaga!!? Km angekuwa ni mtoto hapo sawa.

Hata ben mwenyewe hana kosa la kuhojiwa wala kushitakiwa kwa kupotea kwake..hata akijitokeza mwaka 2018,bado anao uhuru wa kufanya hivyo bila kuingiliwa wala kuhojiwa...! Tuacheni porojo,binafsi bila kujali habari za mwanahalisi,naamini ben yupo na atakuja kujitokeza akichoka kujificha..!!
 
UTATA kuhusu kutoonekana kwa Bernard Saanane, msaidizi wa masuala ya siasa wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe sasa unazidi kuongezeka. Wanaandika Waandishi Wetu …. (endelea).

Taarifa zinasema Saanane ambaye haonekani nyumbani wala kazini, anaonekana kwa marafiki zake mitaani.

Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya Chadema amesema, “Nina wasiwasi kama siyo mkakati binafsi wa kisiasa. Kijana Saanane amekuwa akionesha kutaka kukwea madarakani haraka hata nje ya taratibu. Tafuteni tu mtaona.”

Taarifa kamili juu ya Bernard Saanane, soma gazeti la MwanaHALISI, Jumatatu wiki ijayo.
 
Back
Top Bottom