Taarifa ya tathmini ya mgogoro wa madaktari toka tarehe 03.03.2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya tathmini ya mgogoro wa madaktari toka tarehe 03.03.2012

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mayoscissors, Mar 9, 2012.

 1. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Uongozi unapenda kutoa taarifa kwa madaktari wote nchi nzima kuwa hali ya ushirikiano na umoja miongoni mwetu imeendelea kuimarika sana, hospitali mbalimbali zimeendelea kushiriki katika kushinikiza madai yetu kutekelezwa ili madaktari waweze kutoa huduma za afya.

  Ni muhimu ikafahamika kuwa mpaka sasa Serikali haijatoa jibu la msingi juu ya utekelezaji wa hatua muhimu ya kuendelea na mazungumzo, na hilo ni juu ya Kuwajibika kwa Waziri na Naibu Wazari wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa lengo la kupisha meza ya mazungumzo.

  Pia tumepata taarifa kupitia vyanzo visivyo rasmi juu ya Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukutana na kuzungumza na Wazee wa Dar es Salaam, hivyo basi tuna imani Mhe, Rais atatumia hekima na busara katika kumaliza mgogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu sasa.

  Mwisho, tunapenda kutoa rai kwa madaktari wote kuendelea kusimamia maamuzi tuliyokubaliana tarehe tatu, kwa mabadiliko yoyote tutafanya sote kwenye kikao itakapobidi.

  Imetolewa uongozi.
  08.03.2012
   
 2. K

  KINYAPENYAPE Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kesho ndo mwisho wa uhuni katika afya,hao ni wahuni ,ngoja kesho jk hitimisho kwa hawa wahuni na magaidi wanaotumia uhai wa watanzania kama ngao ya kupitisha hoja zao.baada ya kesho najua baadhi ya magaidi ndio utakuwa mwisho wa wao kupractice
   
 3. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Hamna suluhisho lolote kwa tatizo hili kwa JK kuongea na press. Matarajio yangu nikuwa atafanya yale Pinda aliyofanya na kujaribu kuwatisha madaktari kwa sababu tatizo haliko kwa wazee. JK anatafuta sympathy kwa kundila watu wa yes sir! Mtaniambia hapa kutakuwa na udaku tu na kurushiana vijembe kwenye kikao hicho. JK si decision maker hata siku moja, believe me. He is such a coward!
   
 4. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unajua maana ya ugaidi au unashobokashoboka tu hovyo. Usiuze utu wako kwa bei rahisi kiasi hicho. Please back up!!!
   
 5. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,021
  Trophy Points: 280
  Post ya pili tu unaibuka na upup.u! Tumia ID yako ya zamani basi maana sioni kamba yako mguuni kwa uandishi wa post hii.
  Join Date : 9th February 2012
  Posts : 2
  Rep Power : 0
   
 6. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Kugoma wagome maDaktari hitimisho aktolee kwa wazee wa Dar es salaam....what about wazee wa Mwanza, Mbeya, Dodoma...kwani hao hawaathiriki na kukosekana kwa huduma za afya?

  JK ni rais wa nchi hii...anaogopa nini kukutana na maDaktari ambao ni kiasi kidogo tu cha wananchi wake akotoa hilo hitimisho on their face? is he coward kwenda kukusanya wazee wa CCM akatoe hitimisho huko?!

  Kuna forums nyingi tu za wanataaluma mbali mbali, JK ameshindwa kutumia mojawapo ya forums hizo kutoa hilo hitimisho lake? Au anaogopa challenge ya maswali ambayo hana majibu yake...so anakimbilia kwa wazee wa CCM Dar kwani wao wajua kushangilia bila kuchallenge kwa maswali!?

  NB: Kama kweli unadhani na unaamini JK atatoa hitimisho la mgomo kwa maDaktari kwenye mkutano wake na wazee, basi ni simply unatuambia hapa kuwa 'amiri jeshi mkuu' ni coward na hawezi kukaa kwenye jumuiya ya wanataaluma akatoa uamuzi wake kwa kuogopa kuwa challenged!
   
 7. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu mtu kwanini aongee na wazee wa Dar es Salaam, ambao mda mwingi wanasubiri aweke pozi kidogo wampigie makofi????? mimi nilitegemea suala nyeti kama hili angekaa labda na wasomi wa vyuo vikuu au madaktari wenyewe!!!!!
   
 8. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Subiri mipasho yake, huwa siku zote nahisi Watanzania kuna kitu tumemkosea Mungu mpaka akafanya huyu mtu atuongoze, jamani tumuombe Mungu atuondolee huu mzigo.
   
Loading...