Wadau
Kuna taarifa zipo kwamba IPTL wamezima mitambo yao ya kuzalisha umeme na kusababisha umeme kutokuwepo katika mikoa mbalimbali Tanzania.
Hii inatokana na mwekezaji huyo kufanya maamuzi ya kuondoa mitambo yake na kuipeleka Burundi
IPTL wanatoa 75% ya umeme wa Dar es Salaam
Kama ni hivyo basi hili ni chezo tunachezewa ili tuone umuhimu wa iptl na kukubali yaishe.
Haya haya yalifanywa wakati wa Richmond.
Hapa hakuna cha Burundi,huo mtambo ni wa watz wa hapa hapa huyo kalasinga ni knock tu na hiyo iptl ni front company na wenyewe ni vigogo ndani ya serikali hii ya awamu ya nne.
Kuna kundi la watu ndani ya ccm linapaswa kumulikwa na kushughulikiwa,otherwise haka kanchi kataomba po kwa matatizo yanayosababishwa na hicho kikundi kibaya.
CCM inapaswa kuokolewa toka mikono ya mashetani.Inatumika vibaya na inaangamiza nchi huku wasamaria wema ndani na nje ya ccm mkikaa kimya.
Tatizo tunaiona ccm kama taasisi binafsi ya watu fulani wakati hiki ni chama cha watz wote,kinawajibika kwetu na tunao uwezo wa kukihoji na kukiwajibisha.
Kabla hatujafikiria chadema,cuf etc,tujiulize ni akina nani wameiharibu ccm,ni wakenya?ni nani wamo ndani ya chadema,cuf,ni wajerumani?
Ndio maana nasema tatizo hapa si ccm,chadema,cuf,iptl,tanesco,etc,tatizo ni "watanzania".
Msinishangae kuingiza siasa kwenye uzi huu,i know some individuals ndani ya serikali na ccm wako behind this iptl thing.
Tukumbuke ule usemi,kwamba uovu hutamalaki pale watu wema wanapochagua kukaa kimya.
Watanzania tumechagua uovu,ndio maana tupo kimya,hatuchukui hatua ngumu zaidi ya kuwajibisha vidagaa tu akina Muongo,kalasinga huku "wenyewe" wanaoharibu nchi hii tukiwaacha,na hata hao akina muongo wakilialia sana tutawaonea huruma na kuwaacha kama akina chenge,ndio maana nasema tatizo ni "utanzania".