Taarifa ya Shellukindo dhidi ya Makamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya Shellukindo dhidi ya Makamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TIQO, Mar 21, 2012.

 1. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  TAARIFA YA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA FAMILIA YA WILLIAM SHELUKINDO KUHUSU UBUNGE JIMBO LA BUMBULI MKOANI TANGA

  Kumezuka taarifa za uhakika kwamba tangu Mhe. Januari Makamba ashinde Ubonge katika Jimbo la Bumbuli hajawahi kukutana hata siku mmoja na mbunge wa zamani wa jimbo hilo Mzee William Shelukindo.

  Katika hutuba yake alioitoa mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kura za maoni katika Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Januari Makamba ailisema ataendelea kumuheshimu kama Mzee Shelukindo kama kiongozi wa muda mrefu kwenye Serikali.

  Mheshimiwa Makamba aliendelea kusema Mzee Shelukindo ni hazina kubwa na uzoefu na busara zake bado zinahitajika katika jimbo la Bumbuli na kuahidi kuomba ushauri wake pindi atakapohitaji kufanya hivyo, wakati akiwatumikia wananchi wa Bumbuli kama mbunge wao.

  Lakini kutokutana kwa viongozi hawa kutokutana tangu mheshimiwa Makamba achukue kumesababisha minong'ono na kuleta wasi wasi mkubwa kwa baadhi ya wanasiasa na wananchi wa Bumbuli.

  Kumekuwa na upotoshwaji wa habari kwamba Mzee Shelukindo anawatayarisha watoto wake ili waweze kushindana na Mhe. Makamba katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

  Sisi kama watoto Mzee Shelukindo na tunawashutumu vikali baadhi ya wanasiasa wa Bumbuli ambao wamekuwa wakichochea maneno ili kuleta ugomvi na malumbano yasiokuwa ya msingi kati ya familia hizo mbili za Shelukindo na Makamba.

  Watoto wa Mzee William Shelukindo, Bw. Samuel Shelukindo na Baraka Shelukindo wanawaasa wanasiasa wa Bumbuli kuacha uchochezi na kutotoa taarifa potufu na badala yake kumsaidia Mhe.Makamba ili kushughulikia changamoto zinazolikabili jimbo la Bumbuli.

  Tunasema bado tuna mahusiano mazuri sana na Mhe. Makamba na tunamheshimu kama Mbunge wetu na hawatakubali kuona uhusiano huo unavurugwa na watu wachache wenye maslahi yao binafsi.

  Sisi kama familia ya Shelukindo tunasema kwamba hakuna ndugu wala mtoto yoyote kutoka kwenye familia yetu mwenye nia ya kuingia kwenye siasa ili kupambana na Mhe. Makamba mwaka 2015.

  Kama familia tupo kwenye mikakati ya kuwakutanisha Mhe. Makamba na Mzee Shelukindo ili kufuta fitna zilienezwa na kumuezesha Mhe. Makamba kuendelea kufanya kazi yake ya ubunge bila wasi wasi wowote kwa manufaa ya watu wote wa Bumbuli.

  Asanteni
  Bw. Samuel Shelukindo na Bw. Baraka Shelukindo
  Cont:0784888765- Baraka Shelukindo
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Najaribu kuconnect dots hapa nipate taarifa kamili
   
 3. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  This must be a hoax!

  It is too simple a statement.

  There are so many shellukindos......

  But let me call these numbers
   
 4. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuna tetesi kuwa Makamba hatagombea tena ubunge baada ya kuona majukumu ni mengi na kuwa busy kupindukia. Sina uhakika, inawezekana watoto hao wanajua fika kuwa January atawaachia ili mmoja wao agombee na kuchukua jimbo hivyo saizi wanajikomba.
   
 5. CULCULUS

  CULCULUS Senior Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyie Watoto wa Shullukindo ifike hatua muwe wakweli maana kwa jinsi Mtoto wa Makamba (Januari Makamba) alivyomshusha kwenye kiti cha Ubunge Baba yenu wakati alikuwa bado anataka haikuwa fair kabisa. Kati ya vitu ambavyo Mzee William Shullukindo anakinyongo, kinamuuma na kumsononesha ni hiki kitendo ambacho kwa namna nyingine tunaweza kusema ni Upinduaji wa familia moja dhidi ya nyingine katika ufalme.

  Mi nawashauri Samweli na Baraka Shullukindo mjipange vizuri 2015 kurejesha heshima ya Baba na familia yenu.
   
 6. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Ubunge mtamu thubutu Makamba aliachie jimbo wkt anajitengenezea CV za uwaziri wa nishati na madini na shemeji ake wa mgodini kisha ombwa tafu tayari asaidie $
   
 7. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,833
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Ivi inakuaje eti ubunge kiwe ni kitu cha kuwachiana katika familia? Hii dhana inatoka wapi, wengine wamediriki kusema na sioi nae apewe ubunge eti kama kifuta machozi cha babayake, na makongolo nyerere tungempa urais kama kifuta machozi cha babake. Nyie akina sherukindo ubunge siyo wa familia .
   
 8. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Hivi kulikuwa na mgombea wa chadema huko?
   
 9. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Huo u busy na majukumu si kwa ajili ya Ubunge?
  Au ana kazi zake binafsi?
   
 10. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hawa sio mamluki kweli?
  Hizo simu walizotoa hazipatikani....
   
 11. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Tafuteni kanga za kuandikia iyo mipasho yenu,hiyo mirathi ya ubunge ina umuhimu gani kwa Taifa,nyie kama vipi fungueni shauri la kuteua msimamizi ya mirathi ya ubunge wa wazee wenu wakati mkisubiri hasira za walima miraba,wavuvi na wajasiriamali wanaodhulumiwa kila kukicha,kama ugomvi wenu ungekuwa chanzo ni ukosefu wa huduma za kijamii ningewaunga mkono lakini kumbe mnataka suluhu ili muendelee ku enjoy vile vitenda vya wizarani!!!
   
 12. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  News makers and PR painters at work...
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Mimi nashangaaa hiyo suluhu yenu ina maslahi gani kwa wana bumbuli walio maskini na wenye huduma mbovu. Au ni njia moja ya kuendekeza ulaji wenu na kuendeleza ubunge wa kurithishana
  Fanyeni kazi muwaletee maedeleo wana Bumbuli na si hizi bla bla zenu hapa
   
 14. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,949
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  hii ni mitego ya kupata namba zetu za simu. Stup*id
   
 15. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  ccm kiboko!ubunge mmefanya ni wa ukoo au familia!eti sioi apewe ubunge kufuta majonzi ya kufiwa na babake!damn shit
   
 16. N

  Newvision JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  This does not hold water!
   
 17. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  If you can't beat the Makamba's join them you LOSERS Shelukindo...

  Bumbuli yote ni koo hizi mbili tu zinaweza kuongoza wasambaa wengine hawawezi??
   
 18. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  eti sisi kama watoto tupo kwenye harakati za kuwakutanisha mzee wetu na makamba ili kufuta fitina,ngonjera imetungwa na kumalizia vibaya kwa kuonesha huo mgogoro...pia sioni sababu ya hawa watoto kujishuku eti makamba hawana tatizo naye,watoto acheni kujikomba!
   
 19. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Changa la macho.....! Hii ni janja ya January Marope. Dogo noma kwa majungu, tangu foreign hadi Ikulu mambo yake ni haya haya kuharibia wengine...Nimetoka kuongea na Baraka, hawajui chochote kuhusiana na hii.

  Anajiweka victim ili haurumiwe? Amefanya kosa kuileta hapa. angeipeleka kwa PR wake U-turn Blog
  Nyambaf
   
 20. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hakuna wagombea wengine bumbuli zaidi ya hizi koo mbili
   
Loading...