Taarifa ya Serikali - Kuzama kwa Meli Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya Serikali - Kuzama kwa Meli Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jul 18, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  MAAFA YA KUZAMA KWA MELI ZANZIBAR


  Meli ya Mv. Star Gate imezama karibu na Kisiwa cha Chumbe ambapo watu 12 wamefariki hadi muda huu na wengine kadhaa wamejeruhiwa.


  Akitoa taarifa fupi kwa waandishi wa habari,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini alisema taarifa za kuzama kwa meli hiyo ilitolewa na Boti iendayo kasi ya Kilimanjaro III iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar ndipo ilipoiona meli hiyo ikizama.


  “Tulipata taarifa kutoka Boti ya abiria ya Kilimanjaro III saa 7:50 mchana waliporipoti kuona meli ikizama karibu na Kisiwa cha Chumbe” Alisema Waziri Mwinyihaji.


  Waziri huyo alisema Meli hiyo imezama maili sita kuelekea Kisiwa cha Yasin Kusini mwa Kisiwa cha Chumbe kilichopo Unguja maili kadhaa kutoka Bandari ya Malindi.  Waziri Mwinyihaji alisema idadi ya abiria walikuwa 250 ambao ni watu wazima, watoto 31 na mabaharia 6. “Tumepeleka waokoaji, kuna boti tano zipo eneo la tukio kushirikiana na waokoaji wengine” Alisema Waziri Mwinyihaji.


  Alisema maiti zote zitapelekwa viwanja vya Maisara Zanzibar kwa ajili ya ndugu na jamaa kuzitambua maiti za ndugu zao ambapo majeruhiwa wote watatibiwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.


  Katika Bandari ya Malindi mwandishi wetu ameshuhudia maiti kadhaa zikiwemo za watoto zikishushwa, Miongoni mwa abiria waliookolewa ni raia 13 wa Mataifa mbalimbali ya nje huku raia mmoja ambaye hakuweza kutambuliwa utaifa wake amepoteza maisha.


  Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd alifika eneo la Bandari ya Malindi Zanzibar pamoja viongozi wengine akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, Mawaziri na baadhi ya Wajumbe a Baraza la Wawakilishi walikuwepo kutoa msaada unaohitajika.


  Katika eneo la pembezoni mwa bandari ya Malindi, makundi ya wananchi yalikuwa yamekusanyika wakisubiri taarifa za tukio hilo tangu saa 8:30 mchana.


  Vikosi vya ulinzi na usalama, msalaba mwekundu na watoaji wengine wa misaada ya dharura walifika kwa haraka eneo la tukio.


  Hadi sasa kazi ya uokoaji inaendelea karibu na Kisiwa cha Yasin ilikozama meli hiyo.


  Meli ya Mv. Star Gate inamilikiwa na kampuni ya kizalendo ya Sea Gull Sea Transport Ltd ambayo mwaka 2009 Meli yake nyengine ya Mv. Fatih ilipinduka na kuzama katika Bandari ya Malindi Zanzibar na kua watu sita.


  Mwaka jana Zanzibar ilikumbwa na maafa baada ya Meli ya Mv. Spice Islanders kuzama katika bahari ya Hindi eneo la Nungwi katika Kisiwa cha Unguja ikielekea Kisiwani Pemba ambapo taarifa rasmi ya Serikali ilisema watu 197 walipoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.


  Taarifa zaidi zitatolewa hapo baadea.


  Imetolewa na:
  Idara ya Habari(MAELEZO) Zanzíbar
  Julia 18,2012

  Picha ziadi maafa ya meli  [​IMG]
  Watalii na raia wa kigeni pia walikuwemo katika meli iliyozama hawa ni baadhi ya waliosalimika

  [​IMG]

  Abiria waliookolewa kutoka katika meli iliozama ya Star Gate katika bahari ya Chumbe Zanzibar
  [​IMG]
  Abiria aliyeokoka kutoka katika meli iliyozama
  [​IMG]
  Abiria aliyookoka katika Meli iliozama ya Star Gate akifarijiwa na Jamaa zake Baada ya kuteremka katika Meli iliowaokoa hapo Bandarini


  [​IMG]


  Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamad Masoud Hamad akiwa katika hali ya huzuni Baada ya kushiriki katika uokoaji na kuwaona Majeruhiwaliookolewa katika Meli iliozama ya Star Gate wakiteremka hapo Bandarini Zanzibar.
  [​IMG]
  Askari wa Vikosi mbalimbali wakiwa katika kazi ya Uokozi kwa Abiria waliokuwa katika Meli ya Star Gate ambayo iliozama katika ikiwa imebeba abiria 250 huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar


  Picha zoe na Yussuf Simai Maelezo​
   
 2. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni majonzi makubwa
   
 3. S

  Same ORG JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jee said salim bahresa anazihujumu hizi meli nyingine??? jamani watz tuliangalie kwa undani kabisa haya masuala.
   
 4. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  hakuna hujuma yoyote bali ni uzembe wa utendaji!iweje boti hii chakavu iendelee kutoa huduma wakati marekani waliiona ni chuma chakavu?
   
 5. mcubic

  mcubic JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 10,165
  Likes Received: 4,195
  Trophy Points: 280
  Huyu Nchimbi taarifa za watu saba tu waliofariki kaitoa wapi?? maana kwenye TBC1 amehojiwa amesema ni saba tu..wakati wenyewe wanasema 12..which is which?
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  HAKUNA ATAKAYEWAJIBIKA KWA VIFO VYA WATANZANIA WENZETU, SHAME ON YOU ccm
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  waziri amesahau kusema SERIKALI IMEJIPANGA AJALI KAMA HII ISITOKEE TENA!maana ndio msemo wao siku hizi.Innalillah
   
 8. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Inasemekana zaidi ya watu mia mbili wamefariki. INAALILAHI WAINA ILAIHI RAJIUUN.
   
 9. G

  GUDIGUDI Member

  #9
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani Sio sahii kuhusisha maafa yanayotokea na siasa. Hakuna uhusiano kati ya kuzama kwa meli na ccm haya ni maafa tu kama ajali zinazotokea mara kwa mara. Inaonekana huyu jamaa amekariri na ana chuki binafsi na chama hki kwani upepo mkali ndo umesababisha meli izame na si vinginevyo.
   
 10. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  mkuu menginitis, ile sheria ya manunuzi ya vitu chakavu iliyopitishwa kwa mbwembwe inaapply hadi ng"ambo ya chumbe au mwisho wakke bara tu. maana wenzetu vyombo chakavu wameanzanavyo looong time. nimeshashauri kwenye uzi mwingine kuwa vyombo vyote vya udhibiti viwe chini ya jamhuri ya muungano.
   
 11. m

  mkataba Senior Member

  #11
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh. Hamad Masoud usihuzunike hio ndio kalamu ya Allah, haiepukiki. Ni muhimu kuwaombea dua waliotangulia inshaaallah.

  Innalillahi wainnailayhi rajjighuuuun.

  "Hakika sisi ni wa Alla na kwake yeye ndio tutarejea"
   
 12. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  Duuu maskini wa Mungu R.I.P marehemu wote
   
 13. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,418
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Kuna ndugu zetu wengi sana wamezama na wanaendelea kufa ila sijaona tv hata moja inayo toa up dates, nimejiuliza kama bunge limeweza kuahiriswa inakuweje hamna habari mpya yeyote inayoendelea kutolewa?
   
 14. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,600
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  Naona jmaa wanhistoria ya kuua!
   
 15. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kero za muungano zinaongezeka!
   
 16. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  lazima kuna mkono wa kigogo kwenye hii kampuni
   
 17. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Inasemekana zaidi ya watu mia mbili wamefariki.
   
 18. T

  Twigwe Member

  #18
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bomu zote.zinacopy tu kwa tv zingine
   
 19. BABU CHONDO

  BABU CHONDO JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Iliyozama ni meli au ni boti?

  Sent from my Nokia 3310 using JamiiForums
   
 20. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  ivi inawezekana kuhujumu meli ambayo haina hata OFISI? hii inachangiwa na UDHAIFU wa serikali ya CCM na CUF rushwa inalitafuna Taifa letu.
   
Loading...