Taarifa ya Serikali - Kuzama kwa Meli Zanzibar

Rushwa iliyo kita mizizi itaendelea kutumaliza, MELI HAINA OFISI IDADI KAMILI YA ABIRIA IMEJULIKANAJE,ukija barabarani mabasi yanatoka ubungo mabovu yakiuwa tunaanza kelele.

WATANZANIA MDUDU ANAETUMALIZA NI SERIKALI ILIOKO MADARAKANI KWA KUWA IMEJAA RUSHWA.

Poleni wafiwa na majeruhi mungu awasaidie mpone haraka
 
Jamani Sio sahii kuhusisha maafa yanayotokea na siasa. Hakuna uhusiano kati ya kuzama kwa meli na ccm haya ni maafa tu kama ajali zinazotokea mara kwa mara. Inaonekana huyu jamaa amekariri na ana chuki binafsi na chama hki kwani upepo mkali ndo umesababisha meli izame na si vinginevyo.

unaambiwa meli ilikua mbovu na imewai kuzima katikati ya bahari, ni nani alietoa leseni ya kuendelea kutoa huduma kama sio ccm na serikali yake.!
 
bakhresa ndo anasimamia uendeshaji hizo meli?
watanzania ni watu wa kupenda kutupa lawama kila mara...
badala ya kutatua tatizo kutwa lawama tu...




jee said salim bahresa anazihujumu hizi meli nyingine??? jamani watz tuliangalie kwa undani kabisa haya masuala.
 
Jamani Sio sahii kuhusisha maafa yanayotokea na siasa. Hakuna uhusiano kati ya kuzama kwa meli na ccm haya ni maafa tu kama ajali zinazotokea mara kwa mara. Inaonekana huyu jamaa amekariri na ana chuki binafsi na chama hki kwani upepo mkali ndo umesababisha meli izame na si vinginevyo.

Gudigudi au badibadi whatever your name seal.. Mtu Wa makamo unaweza kweli kushawishika kwamba taatifa hii ni ya Serikali makini??!!

Au ni uhuni tu Wa kupikapika Na kuropoka, hakuna mwenye Kutaka kuhusisha tukio Hili Na siasa but siasa wanaziweka hawa jamaa Kwa kuwadharau wananchi Kwa kiwango hiki.. Taarifa ya serikali lazima iwe Na dondoo zifuatazo..

1. Abiria wangapi walikiwemo ikionyesha listi kamili ya majina, utaifa, Umri Na Jinsia..Na Tiketi registry

2. Mmiliki Wa chombo, sehemu ya ofisi, Na wasifu.

3. Mpaka sasa abiria waliookolewa Kwa mujibu Wa registry, Na ambao wanadhaniwa Bado wemekamatwa Na roho ya Bahari.

4. Idadi ya vyombo vilivyotumwa Kwenye zoezi la uokoaji, Binafsi Na serikali..

5. Usalama Wa chombo (haliyahewa)
-mazingira Chombo kilipokuwa cleared kuondoka Na mamlaka Za hali ya Hewa ilihali wakijua upepo wa mbisho ulikuwa mkali..
-uimara Wa chombo, maintenance schedule
-taarifa ya marine safety & app dept ambao hukagua meli au chombo kabla ya mwendo..
- SUMATRA ----

VYOMBO VINGINE VYA HABARI VYAWEZA KURIPOTI CHOCHOTE BUT SERIKALI LAZIMA IJE NA DETAILS KWA HARAKA KABLA TAARIFA MBAYA HAZIJAENEA..

SI BURE UTASIKIA TUME INAUNDWA NA WATU KADHAA WANAKABIDHIWA MIHELA LUKUKI Kutengeneza movie ya kuuhadaa umma..
 
Poleni ndugu ,watanzania na jamaa wote waliofikwa na msiba Huu.Lakini hii kampumi naomba ichuguzwe isije ikawa inatumia maisha ya abiria kuwa mtaji wake kupitia ajali za meli mbovu wanazozitumia kuendesha biashara ya usafirishaji halafu wanakunja Bima kibindoni.
 
Poleni sana wote waliopatwa na kuhusika na ajali hii mbaya.
Tatizo la hizi boti nikuwa wanunuzi na wasajiri wa meli hawafanyi uchungzi wa kutosha. Meli hii pamoja na nyenzie Kalama zilitengenezwa kwa ajili ya Washington State Ferries na zilikaa muda kabla ya kuanza kazi. Tatizo kubwa lililolalamikiwa wakati zikifanya kazi ni stability wakati wa mawimbi. Moja ya sababu nahisi ni kuongezwa kwa deck moja juu ambayo haikuwamo katika original design!!! Ni tatizo hilo lililoizamisha wakati wa mawimbi makali. Ref The Monohulled Passenger Only Boats Skagit and Kalama.
 
taarifa kama hizi tunazo nyingi sana.tunachohitaji ni kinga na tahadhari dhidi ya maisha ya watu,hivi ni vifo vinavyozuilika.

kuna uzembe mkubwa hapa hasa katika suala la ukaguzi na matengenezo ya mara kwa mara ya vyombo vya usafiri.

juzi hapa watu zaidi ya kumi wamekufa kwa ajali ya gari huko geita.huu ni upuuzi ulipituka mipaka
 
[h=6]EWE MOLA WAPE SUBIRA NA USTAHAMILIVU WALE WOTE WALOPATWA NA MSIBA HUU WA AJALI YA MELI KWANI WOTE SAFARI YETU NI KWAKO. WENZETU WAMETANGULIA SISI HATUJUI NI LINI TUTAFUATIA. WAPONYE WALONUSURIKA WAREJEE KATIKA FAMILIA ZAO. INALILAHI WAINAILAYHI RAJIUN. POLENI WANZANZIBAR POLENI WATANZANIA[/h]
 
Meli nyingine imezama hata kabla mwaka kuisha toka ilipozama ile ya kwenye mkono wa nungwe? This is getting more serious. Bila kuwa na maana ya kumlaumu yeyote yule, iko haja ya watu kuanza kuwajibika. This is too much!
 
Katika hali ya kawaida baada ya matukio mengi ya ajali za majini kuanzia MV Bukoba, Spice Islander serikali kupitia vyombo vyake husika kama SUMATRA wangekuwa wameweka usimamizi na Ukaguzi madhubuti ili kuepusha ajali hizi. Rushwa na ukosefu wa uwajibikaji utaendelea kutuletea ajali hizi kila kukicha. Serikali ni muhimu ifahamu kuwa wakati wa kuongea bila vitendo ulishapita.
 
Back
Top Bottom