Taarifa ya kongamano kwa wazanzibar wote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya kongamano kwa wazanzibar wote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Oct 4, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kamati ya Maridhiano Zanzibar (Kamati ya Mzee Moyo) imeandaa Kongamano kubwa la Kitaifa kuzungumzia Nafasi ya Zanzibar katika Mjadala wa Katiba Mpya.

  Kongamano hilo litafanyika siku ya Jumamosi, tarehe 06 Oktoba, 2012 saa 3:00 asubuhi katika Ukumbi wa SALAMA, Hoteli ya Bwawani. Mwenyekiti wa Mjadala atakuwa Prof. Abdul Sheriff.

  Wazungumzaji ni pamoja na Mzee Hassan Nassor Moyo, Sheikh Salim Said Rashid (Katibu Mkuu wa mwanzo wa Baraza la Mapinduzi), Mwanasheria Mkuu Mhe. Othman Masoud Othman, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Mhe. Ibrahim Mzee, Amiri Mkuu wa JUMIKI Sheikh Msellem Ali Msellem, Waziri asiye na Wizara Maalum na Mwakilishi wa Kiembe Samaki Mhe. Mansoor Yussuf Himid, Mwenyekiti wa ZAHILFE Ndugu Kassim Hamad Nassor, Mwenyekiti wa Vijana wa Umoja wa Kitaifa Ndugu Khaleed Gwiji, Rais wa Zanzibar Law Society (ZLS) Ndugu Salim Toufiq, Mwakilishi wa WAHAMAZA Ndugu Salma Said, Mwakilishi wa UKUWEM Dk. Mohamed Hafidh na wengine wengi.

  Tunaomba kila mmoja amuarifu mwenziwe. BWAWANI KUFURIKE!
   
Loading...