Madenge Origino
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 1,847
- 1,096
Hii ni taarifa ya habari ya asubuhi kutoka televisheni yako ya Mabadiliko ya jijini Dar es salaam, Tanzania, msomaji ni mimi mwanamabadiliko! Habari za Kitaifa!
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) imemtangaza rasmi mgombea wa kiti Urais wa Chadema, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowasa kuwa ni mshindi wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015.
Rais mteule Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowasa anatarajiwa kuiongoza Tanzania mpya kwa muhula wa miaka mitano ya 2015-2020! Lowasa amechaguliwa kwa idadi ya kura nyingi tu na kumwacha kwa mbali kabisa mpinzani wake aliemfuatia Ndugu John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi , CCM, aliepata kura chache sana.
Mheshimiwa Lowasa ataapishwa rasmi kuwa ni Rais wa Tanzania hapo tarehe 01/11/2015 katika sherehe zitakazofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Ikumbukwe tu ya kwamba Lowasa na chama chake cha chadema walikataliwa na serikali iliopo madarakani kufungulia mikutano yake ya kampeni za kugombea Urais katika uwanja huo wa Taifa!
Hii hapa ni sauti ya Rais mteule Mheshimiwa Lowasa akielezea shukrani zake kwa watanzania mara tu baada ya kutangazwa mshindi!
"...napenda niwashukuru Watanzania kwa kunipa ridhaa mimi na Chama Changu cha Chadema ya kuiongoza nchi yetu ya Tanzania kuelekea kwenye Mabadiliko. Watanzania wameamua wanataka Mabadiliko na napenda niseme ya kwamba safari yetu ya mabadiliko ndio imeanza sasa. Mimi nitakuwa ni Rais wa watanzania wote. Nitakuwa ni Rais wa wenye kupenda mabadiliko na hata wale wasiopenda mabadiliko..."
Hata hivyo wanahabari wetu wa Televisheni yako ya mabadiliko walijaribu bila ya mafanikio yoyote kuzungumza na mpinzani wake wa karibu wa uchaguzi huo, Ndugu Magufuli, bila ya mafanikio yoyote. Taarifa zisizo rasmi zimetuarifu ya kwamba Ndugu Magufuli amejifungia ndani ya ikulu ya Rais ya Magogoni akilia pamoja na Rais wa Tanzania anaemaliza muda wake Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.
Taarifa zilizotufikia hivi punde tu kutoka kwa wanahabari wetu ni kwamba ndugu Magufuli na timu yake ya kampeni ya chama cha mapinduzi wamejiandaa kukata rufaa mahakama kuu ya Tanzania kupinga ushindi wa mheshimiwa Lowasa. Hata hivyo Televisheni yako ya mabadiliko haiamini ya kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu kupinga Ushindi wa mabadiliko mahakamani!
Ahsanteni
Wimbo wa Taifa...