Taarifa ya chama cha wananchi cuf kwa vyombo vya habari kuhusu mgao wa umeme

Mtutuma bila shaka unarusha vijembe kwa wenzako lakini naona kama unajichanganya, kwanza umesema cuf haifanyi maandamano bila specific issue hebu tuambie wana jamvi ni chama kipi kimefanya maandamano bila specific issue? Pili umezungumzia cuf haiko tayari kuindoa serikali iliyoko madarakani kwa maandamano, unaweza kutuhakikishia ni chama gani kinataka kufanya hivyo chini ya serikali ya ccm yenye vyombo vya ulinzi na usalama au na nyie (cuf) mmeingia kwenye siasa za propaganda kama ccm kuzusha uongo ili ku-draw attention ya wananchi? Tatu umesema nyie cuf kwa sasa hamsikiki kwakuwa siasa zimehamia bungeni na kwabahati mbaya unasema kinachoandikwa zaidi ni malumbano ya posho za wabunge! Nafikiri Mtutuma hapo unajichanganya, hoja ya posho ilipoletwa bungeni ililetwa kwaajili ya posho zote na sio za wabunge tu labda wewe mwenzetu ulipitwa na hukujua ilipoanzia, ila kwa mtoa/watoa hoja kuonyesha mfano wa uongozi akaanza kwa kuzikataa posho za ubunge na hapo ndipo vyombo vya habari vilipojikita. Kama ulikuwa makini hata uchambuzi wa bajeti umefanywa kwa kina na kambi rasmi ya upinzani kiasi cha mwananchi wa kawaida kuielewa, ninachotaka kukuhabarisha tu ni kwamba wale wabunge wote ambao ni mwiba kwa serikali na ccm wamekuwa wakisumbuliwa kwenye mijadala bungeni kiasi cha bunge kuonekana ni mahali pa vijembe lakini elewa kwamba wananchi ndio majaji wa mijadala na wamefunguka akili sio wale wa zama zile.
Chadema(magwanda ya mgambo)
 
Hivi ukiachilia mbali kujiuzulu hivi akifa leo umeme ndiyo utapatikana?.............................................CUF ajirini wataalamu waweze kuwashauri mkashaurika.....................................hizi ni pumba bila ya kuwaficha wanandugu zangu....................
Mkuu,
tuwe objective, hili tamko limetulia na lina kila aina ya ukweli. Inatakiwa CUF waunganishe nguvu na Chadema ili waibane hii serikali isio na plan...
 
cuf ni bure kabisa, mbona hatuoni mchango wenu bungeni zaidi ya kusema ndio na kubeza wanamapinduzi wa ukweli.
 
CUF itisheni maadamano Serikali iondoke madarakani imeshindwa na haitaweza kutatua tatizo la Umeme. Fedha zipo tena nyingi mno ltatizo ni serikali ya CCM haina watendaji wenye uwezo kufikiri na kuwa creative "WOTE WALIOKO SERIKALINI NI WAVIVU WA KUFIKIRI"
 
Back
Top Bottom