Taarifa ya chama cha wananchi cuf kwa vyombo vya habari kuhusu mgao wa umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya chama cha wananchi cuf kwa vyombo vya habari kuhusu mgao wa umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtutuma, Jul 3, 2011.

 1. m

  mtutuma Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imetolewa na;Julius Mtatiro,
  Naibu Katibu Mkuu CUF – Tz Bara,
  Jumapili, 03 Julai 2011 saa 5.00 Asubuhi – Dar es salaam.

  UTANGULIZINdugu waandishi wa habari,Nchi yetu hivi sasa inakabiliwa na mgao wa umeme ambao ni mkali kuliko
  ule 2006. Umeme unaofuliwa haukidhi mahitaji. Tunaambiwa maji katika mabwawa yanayofua umeme yamepungua sana.
  Tatizo hili ni la muda mrefu. Watanzania wana kila sababu ya kukasirishwa sana na mgao huu wa umeme miaka 5 baada ya mgao wa 2006 na kuahidiwa na serikali ya CCM kuwa mgao wa umeme utakuwa ni historia. ATHARI ZA MGAO WA UMEME.Ndugu waandishi wa habari, 1. Athari za mgao wa umeme ni kubwa sana. Wananchi wanasumbuka, vyombo vya umeme majumbani, maofisini na viwandani vinaharibika kwa sababu ya ukataji wa umeme wa mara kwa mara . 2. Shughuli za uzalishaji bidhaa na utoaji huduma umeathirika na ajira kupungua. Wawekezaji wa ndani na wa nje wanasita kuwekeza vitega uchumi na hivyo kuongeza ajira kwa sababu ya kutokuwa na umeme wa uhakika.
  1. Mgao wa umeme unasababisha katizo la ajira nyingi sana. Hivi sasa vijana wengi wanaotegemea ajira katika viwanda vodogovidogo vya useremala, kusindika matunda n.k. Vijana hawa wanajikuta hawana pa kukimbilia kwa sababu ya ukosefu wa umeme.
  2. Hivi sasa viwanda vingi vidogo na vikubwa vinafungwa au inabidi vizalishe bidhaa kwa gharama kubwa ambapo mwananchi wa kawaida ambaye ni mlaji ndiye anayebebeshwa mzigo wote.
  3. Kwa kifupi mgao wa umeme usiokwisha ni sawasawa na SHETANI LITIALO Umasikini kwa jamii ya watu ambao tayari ni masikini. Na kwa hakika, Serikali ya Tanzania imebadilisha umeme kutoka kuwa tatizo linalotatuliwa hadi kuwa JANGA LA KITAIFA.
  UDANGANYIFU WA SERIKALI YA CCMNdugu waandishi wa habari,Sababu zimekuwa zilezile za uongo wa kila namna Mabwawa hayajajaa,mitambo imeharibika, mafuta yamekwisha n.k. Hizi ni sababu za kijinga sana kwa nchi mabayo imepata uhuru kwa miaka 50 yenye viongozi waliosoma kila aina ya elimu huku nchi ikiwa na rasilimali za kutosha. Pamoja na hali hii ngumu ya upatikanaji wa umeme RAIS Kikwete katika hotuba yake ya kufunga mwaka 2010 aliwajulisha watanzania kuwa katika kipindi cha miaka mitano 2005-2010 “TANESCO kwa msaada wa Serikali, imeongeza uwezo wa kuzalisha umeme kwa MW 145 (MW 100 Ubungo na MW 45 Tegeta) kwa kutumia gesi asilia.” Katika hali halisi rais ameendelea tu kuahidi utekelezaji wa miradi mingine kadhaa itakayotoa takribani megawati 1130 katika kipindi cha 2011-2013 jambo ambalo litakuwa maajabu ya dunia, yaani serikali iliyoweza kuongeza uzalishaji wa megawati 145 tu katika kipindi cha miaka mitano 2005-2010 itaweza vipi kuzalisha megawati 1130 katika kipindi cha miaka mitatu? Watanzania wanadanganywa mchana kweupe tena bila chembe ya aibu. Ndugu waandishi wa habari,MTIZAMO WA CUF.
  1. CCM, SERIKALI yake, WIZARA ya nishati na madini na TANESCO wanaendelea kuua uchumi wa Tanzania kwa uzembe, wameshindwa kutafuta suluhisho la matatizo makubwa ya watanzania ambayo ndiyo msingi wa ahueni ya kiuchumi mahali popote.
  2. Serikali ya CCM ni dhaifu, haina mbinu za kukabiliana na mitihani hii migumu, Serikali ya CCM imechoka na hata kila mtu mwenye ubongo mzuri anapojaribu kuwasaidia watanzania kupitia CCM anafeli kabla hajaanza.
  TATIZO LIKO WAPI.Ndugu waandishi wa habari, Tatizo la kwanza ambalo chama cha wanachi CUF kimelifanyia utafiti wa kina na ambalo serikali ya CCM wamekuwa wakilificha na ambalo ndilo chanzo cha mgao wa sasa, jana, leo na kesho ni upungufu wa umeme.Tumegundua kuwa umeme unaozalishwa hivi sasa ni mdogo mno kulingana na mahitaji. Hata kama mabwawa yote yakijaa maji na mitambo ikawa na mafuta ya ya kutosha tatizo la umeme litakuwa palepale kwa asilimia 100.Hadi sasa hitaji la matumizi ya umeme ni megawati takribani 3000 nchi nzima lakini umeme unaopatikana ni megawati takribani 800 tu,hali hii inatishia ustawi wa taifa letu kiuchumi,kiviwanda,kiajira na ki-vipato na hali hii inayoendelea inaonesha katika miaka miaka mitano ijayo ya Rais Kikwete na CCM hali itakuwa mbaya sana na kama watanzania wanahitaji mabadiliko ya kweli kiuchumi na kuongeza vipato vya watanzania suluhisho ni wao wenyewe kupitia masanduku ya kura mwaka 2015. Tumegundua kuwa tatizo la umeme haliwezi kupunguzwa wala kuisha kwa sababu watumiaji wa umeme wameongezeka mno, viwanda vidogovidogo vimeongezeka kwa wastani na viwanda vikubwa vingi vimekuwa vikipanuliwa ili kuendana na teknolojia na mabadiliko ya mahitaji ya masoko ya bidhaa na hivyo kila eneo likijikuta linahitaji umeme mwingi mno ambao serikali haiwezi kutoa.Wakati haya yakiendelea vyanzo vya umeme vinabakia kuwa vilevile na hasa tangu serikali ya awmu ya kwanza ilipomaliza muda wake hakuwahi kutokea rais au serikali yoyote ambayo iliwekeza nguvu kubwa katika umeme na hasa kutafuta vyanzo mbadala tofauti na kutegemea maji. Hapa tuna maana kuwa waziri wa nishati na madini na TANESCO wamewadanganya watanzania, tatizo la kukosa umeme wa uhakika siyo mabwawa kuokosa maji wala mitambo kukosa mafuta. Tatizo ni kuwa hivi sasa TANESCO wamezidiwa na umeme unaohitajika kwa hiyo serikali, waziri na TANESO wameona njia pekee ya kukimbia “bomu” hili lililojificha ni kutangaza mgao mkali wa umeme hadi mwakani huku wakiamini watanzania wataziamini sababau zao za uongo.Kwa maana nyingine hata Rais anapotafuna fedha za umma kwa safari za nje za kila kukicha kiguu na njia kuonana na wawekezaji na kuwashawishi waje kuwekeza Tanzania –“anawahadaa” na “kuwadanganya” kwani hadi sasa wawekezaji waliopo tu ukiongeza na chini ya 10% ya nyumba ambazo zimeunganishiwa umeme, wako katika mgao mkubwa ambao utaendelea bila kikomo.CUF – Chama cha wananchi tunamshauri rais Kikwete asipoteze muda wake kwenda nje kusaka wawekezaji kwani walioko ndani ya nchi tu serikali yake imeshindwa kuwapatia umeme wa uhakika. Gharama anazotumia kwenda kutafuta wawekezaji ni kiini macho tu kwa sababu duniani haijawahi kutokea wawekezaji wenye mitaji yao ya uhakika kuja kuwekeza GIZANI.Ndugu waandishi wa habari, Tatizo la pili ni kuwa watendaji walioko ndani ya serikali ya CCM wanaogopa sana kuanzisha vyanzo vipya vya umeme asili kutokana na kukosa miradi ya kukatiwa 10%.CCM wanaamini kuwa usipokuwa na vyanzo vingi vya asili vya umeme inasaidia kuleta dharura za ukosekanaji wa umeme mara kwa mara na hivyo hii ina –“encourage” inavutia maamuzi ya haraka ya kuleta mitambo ya mafuta n.k ambapo ni rahisi kupata 10% za wakubwa. Huu ni ugonjwa wa hatari ambao pia unalifikisha taifa hapa lilipo. Ndugu waandishi wa habari, NINI KIFANYIKE KWA SASA.
  1. CUF - Chama cha wanachi tumekuwa tukimtaka waziri wa nishati na madini Wiliam Ngeleja ajiuzulu kwani ameshindwa kusimamia TANESCO walau katika mfumo huohuo mbovu wa serikali ya CCM apewe mtu mwingine ambaye anaweza kujaribu kuiondoa Tanzania kwenye tatizo la mgao wa umeme usiokwisha. Kitendo cha waziri kung’ang’ania kuongoza wizara ilihali imemshinda ni ishara ya wazi kwamba anamaslahi na Tanesco na hawafikirii watanzania.
  2. Nchi yetu imejaliwa vianzio vingi vya nishati ya umeme iwapo tungepata serikali shupavu na makini inayoweza kuongozwa na chama chenye visheni,maadili na viongozi imara kama CUF tungeweza kutatua tatizo la umeme kwa zaidi ya 80% kwani kuna kila namna ya vyanzo ndani ya nchi yetu ambavyo CCM hawana muda wa kufikiria kuvitumia kwa uhakika na nia thabiti bila kuweka maslahi binafsi.
  i. Maeneo ya maporomoko ya maji yakitumiwa yote yanaweza kufua umeme wa MW 5000 ukilinganisha na uwezo wa sasa wa umeme wa MW 562 na umeme wote wa gridi ya taifa ya MW 791. ii. Makaa ya mawe ambayo yameshagunduliwa yanaweza kufua umeme wa MW 1000 kwa zaidi ya miaka 50 ijayo. iii. Vile vile gesi iliyonguduliwa Mnazi Bay, Mtwara,Mkuranga na Songo songo, Kilwa inaweza kufua umeme wa zaidi ya MW 1000 kwa zaidi ya miaka 50 ijayo. iv. Madini ya urani (uranium)yaliyogunduliwa Namtumbo na Manyoni nayo yana uwezo wa kufua umeme malaki ya MW kwa muda mrefu. v. Gharama za kufua umeme wa jua na upepo zimepungua na zinaendelea kupungua. Tanzania ina maeneo mengi ya kuweza kufua umeme wa solar na kwa kutumia upepo. Miaka hamsini baada ya kupata uhuru, hatuna sababu ya kutokuwa na umeme wa uhakika isipokuwa ombwe la uongozi na ufisadi ndani ya CCM na serikali zake.
  1. CUF – Chama cha wananchi tunawaomba watanzania watambue kwamba sababu ya umasikini wao, maradhi yao, uchumi uliodumaa na kila aina ya matatizo yanayowakabili ni mazao ya kuikumbatia CCM. Watanzania wasitafute mchawi wa mgawo wa umeme, mchawi wanamjua vizuri sana – Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Serikali ya CCM na Waziri wa nishati na madini(wa milele) Bwana Ngeleja.
  2. Wakati watanzania wakishughulikiwa na makali haya ya magao wa umeme yanayozidi kuwapa maumivu makali ya uchumi na vipato. Watumie muda mfupi na kujipanga KUIONDOA CCM madarakani mwaka 2015. Tunaamini wakati huo tukakuwa na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, ni wakati muafaka wa kuweka mbali ushabiki wa Kapelo na Khanga vinavyogawiwa na CCM, ni wakati wa kuwashughulikia kupitia masanduku ya kupigia kura ili tupate serikali adilifu itakayomtumikia mtanzania. CCM na Serikali yake ndio chanzo cha umasikini na matatizo ya Mtanzania.
  “HAKI SAWA KWA WOTE”
  Posted by Mohammed Mtutuma,
  Msaidizi Maalum wa NAIBU KATIBU MKUU – CUF,
  Tanzania Bara.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Asante kwa tamko,naimani yalitoka na yanatoka na yatatoka meeeeng,lakin hayataleta UMEME.....
  SOLIDARITY FOREVER
   
 3. i

  in and out Member

  #3
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tumewasikiaaaa!!! mbona mnakuwa kimya sana?
   
 4. Yousuph .M.

  Yousuph .M. Senior Member

  #4
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mtutuma,
  Ahsante sana kwa bandiko la tamko la CUF hapa jamvini, je mnamikakati gani thabiti ya kuwaeleza wananchi wasio na uwezo wa kuperuzi mtandaoni juu ya tamko lenu ama kutakuwa na maandamano ya kuamsha ari ili wapiga kura huko uswahilini wajumuike katika kupaza sauti za tatizo la umeme?
  Kwa wananchi kusubiri mpaka 2015 kuiondoa madarakani CCM ndipo utatuzi wa ufumbuzi wa tatizo la umeme...hapo ni mbaali sana kwani hali ya maisha itakuwa tafrani kubwa hususan wajasiriamali uswahilini wasioweza hata kumudu kununua generator, maana wengu sana uswahilini tunategemea maisha ya kuuza barafu, juice, mtindi, maji ya vipaketi (yalee uswahilini huuzwa sh.50/ mpaka 100/=.
  Kwani haiwezekani ninyi kama chama walau mngeweza hata kuchukua kijiji kimoja tu na mkafanya uzalishaji wa umeme kwa MW hizo chache ili kuangalia tatizo linaweza kuwa KUBWA kiasi gani au ni DOGO kiasi gani, mkianza kwa mfano itawawia rahisi sana kupaza sauti zenu na kusikika iwapo mtaanza kwa mfano. Mkijaaliwa kupunguza matumizi yenu kwa mwezi halafu mkafanya experiment ya kijiji kimoja kuzalisha umeme hata wa upepo (kwa hizo fedha kidogo mlizonazo) nadhani mtatoa taswira nzuri na yenye mwanga wa uchungu wa matatizo ya kitaifa, kisha ushauri ufuatie.

  Ni maono yangu tu kwa CUF, sina chuki wala uhasama wa kisiasa.
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  safi sana CUF .
  sasa ngeleja asipoondoka tufanye nini? tangazeni maandamano tuingie mtaani.
   
 6. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Tulianzishe mbele kwa mbele Waziri ajiuzullu
   
 7. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  He,,,,,,,,,Jamani Cuffffffffffffffffffffffffffffff mpo bado mna exist eti?
   
 8. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Watanzania wasitafute mchawi wa mgawo wa umeme, mchawi wanamjua vizuri sana – Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Serikali ya CCM na Waziri wa nishati na madini(wa milele) Bwana Ngeleja.
  Hii nimeipenda!

  Sasa daini talaka mtangaze maandamano ya kung'oa Kikwete na Ngeleja watu tuindie kataa
  A friend of my enemy is my enemy too!
   
 9. OPTIMISTIC

  OPTIMISTIC Senior Member

  #9
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ahsante CUF kwa kuonyesha mwelekeo, kwa bahati mbaya wananchi watanzania tunafikiria mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa ni matokeo ya jitihada za vyama vya upinzani vya siasa ambayo ni asilimia ndogo sana,
  Ushauri wangu kwa viongozi wa vyama tuwaeleze wananchi na vyama hivi viungane vinapotetea mambo ya msingi ya kitaifa taifa liache kuburuzwa. Kuna umuhimu wa kuwa na sauti moja ya kitaifa ili kushinikiza CCM watambue kwamba nguvu ya mabadiliko na uamuzi juu ya maendeleo ya taifa sio RAISI bali ngazi ya juu kabisa ni sauti ya WANACHI WATANZANIA.

  GOD BLESS TANZANIA
   
 10. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mmh! kumbe Mzee yusuph makamba nawe humo humu jamvini? Najua utakataa kata kata, lakini theway ulivyotoa comment yako....haina ubishi wewe ni mzee makamba wa ccm. Hata hivyo napingana na wewe kwa kuwaeleza CUF eti wakachukue kijiji kimoja na wazalishe umeme kama majaribio, kwani hao Cuf ndio wanaingoza serikali? nyinyi mmekaa madarakani miaka 50 na ushee lakini hadi leo umeme hakuna kwanini usiseme acha nimshauri kikwete na ccm yenu kuwa mtoke madarakani na muaachie CUF kwa majaribio?

  Ni maoni yangu tu kwako,sina chuki wala uhasama na wewe mzee makamba
   
 11. m

  mtutuma Member

  #11
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuongoza wananchi na kuwapatia maendeleo ya uhakika hakuna uhusiano na maandamano, hata wanaondamana huku na kule sijajua huwa tumefanya tathmini kujua mafanikio ya maandamano hayo, unahitaji maandamano ya bila kikomo nchi nzima kuiondooa serikali madarakani lakini CUF tuna mtizamo tofauti juu ya hili. Tunaamini kuingia madarakani kwa ridhaa ya wananchi na kwa kupitia masanduku ya kura tu. Ikitokea leo uongozi unaondolewa kwa kutumia maandamano na nguvu ya wananchi sisi hatutoshiriki katika serikali hiyo. Na ndiyo maana hata Zanzibar tumeingia serikalini baada ya wananchi kuamua kwa kupiga kura kuwa chama kitakachopata asilia 5 ya kura kitaingia serikalini.

  Hizi tactics za kuondoa serikali kwa nguvu hazina tija kwetu kwani tunaamini utawala unaoingia kwa mabavu lazima utaondoka kwa mabavu na hatukuunda chama ili tuingie madarakani mara moja na kuondoka forever, tutakuwa hatujawasaidia watanzania.

  Tunachopaswa kufanya kama chama ni kuendelea kushinikiza kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi na katiba mpya yenye misingi ya demokrasia na utawala bora ili baada ya hapo kuwe na free and fair elections ambayo italutea viongozi watanzania wawatakao. Lakini kwa sasa kama chama hatuthubutu kuwashawishi wananchi waing'oe serikali na hata tunapokuwa na maandamano yanakuwa na specific issue na tunayafanya mara moja tukimaliza tunaendelea kuibana serikali kwa namna za kawaida kama cha siasa cha upinzani.

  Suala la CUF kuanzisha chanzo cha umeme katika kijiji cha majaribio hilo hatuwezi kufanya unless otherwise tupewe access ya kukusanya kodi na mapato ili ku_generate mtaji kwa ajili ya chanzo hicho , huwezi kukitaka chama ambacho hakiongozi nchi kianze kuleta maendeleo, labda chama chenyewe kiwe cha matajiri wawe wanachanga.
   
 12. m

  mtutuma Member

  #12
  Jul 3, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wala hatuko kimya hata kidogo, hivi sasa siasa zimehamia bungeni na ndiyo kawaida ya siasa katika nchi yoyote. Bungeni wabunge wetu wanasema mambo muhimu mara nyingi mno lakini kwa bahati mbaya bunge na vyombo vya habari kila kukicha kipaumbele ni posho za wabunge. Vyama vinavosigana kuhusu podho za wabunge vitaandikwa sana wakati huu lakini bunge la bajeti litakapoisha watanzania hawatajua chochote kuhusu bajeti zaidi ya kukaririshwa kuwa tatizo ni posho. Sie mtizamo wetu ni review ya posho zote na kuzipunguza katika kila sekta ndani ya nchi. Kuna watu wanalipana posho nyingi sana kila kukicha, katika vyuo vikuu vyetu hivi posho ya kikao kimoja cha COUNCIL ni 450,000/-, kila sekta imeoza na ndiyo maana Mnyaa alilisitiza hili lakini kwa bahati mbaya nchi hii mjadala wa bajeti ni posho za wabunge na ikiwa hauongelei posho za wabunge wewe hautaandikwa. But the truth is tunajitahidi sana lakini huwezi kutusoma mahali. Wakubwa watalifanyia kazi hili.
   
 13. m

  marmoboy Member

  #13
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu mtutuma,
  Nimeipenda sana hiyo statement, kamkwere kamelal zake ikuluuuuuuuuuuuuuuuu, na nimepta logic kuwa hii kampeni ya CCM ya kuleta wawekezaji wanakuja kuwekeza kwa kutumia nishati ipi? Au ndo kuja kuwekeza kwa mitishamba na tunguli za ababu loliondo?
  Mwambie comrade mtatiro akaze buti.
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wale mnaoshangaa kuwa CUF ,eti mnashuka na suali ,ipo wapi,wengine eti kumbe CUF mpo ? Na wengine wale wa mwendo mdundo nao hawaeleweki,kwani mabomu yao yanaonekana kudumaa !!

  Kwa ufupi wandugu wapenzi CUF ipo na itaendelea kuwepo kama uwepo wa jua na mwezi ,mnassahau tu kuwa baadhi ya wakati mwezi hupotea na hata jua hukamatwa au hupatwa , So far so good CUF ipo nabado inatisha tena kwa siku zijazo mtaona ni akina nani wataingia mitini na wengine kukimbia nchi ,kwani wanangangari wapo na wanajipanga kishujaa ,siku ikitangazwa na kupigwa tarumbeta basi msikae nyuma ,mambo ni mbele kwa mbele.Kutawaliwa na CCM hakutakiwi tena Tanzania ,kama viongozi waliokaa kwa madarakani kwa miaka mingi wanaondolewa madarakani .basi hata Chama kinachokaa madarakani kwa muda mlefu nacho hakina budi kuondoka kama hakiondoki ni lazima kiondolewe kwa nguvu,nguvu ya umma.Huu ujanja ujanja wa kupokezana vijiti wakati waliopita wanakaa pembeni na kupokea mamilioni ya hela ,hawa hawana tofauti na wale wanaokaa madarakani milele wakisubiri nguvu ya umma izuke,safari hii nguvu ya umma itakishukia Chama kizima cha CCM,kwani viongozi wote wa serikalini wameshakaa madarakani zaidi ya miaka 30 ni wao kwa wao wakirithishana.
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280
  Hivi ukiachilia mbali kujiuzulu hivi akifa leo umeme ndiyo utapatikana?.............................................CUF ajirini wataalamu waweze kuwashauri mkashaurika.....................................hizi ni pumba bila ya kuwaficha wanandugu zangu....................
   
 16. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mtutuma bila shaka unarusha vijembe kwa wenzako lakini naona kama unajichanganya, kwanza umesema cuf haifanyi maandamano bila specific issue hebu tuambie wana jamvi ni chama kipi kimefanya maandamano bila specific issue? Pili umezungumzia cuf haiko tayari kuindoa serikali iliyoko madarakani kwa maandamano, unaweza kutuhakikishia ni chama gani kinataka kufanya hivyo chini ya serikali ya ccm yenye vyombo vya ulinzi na usalama au na nyie (cuf) mmeingia kwenye siasa za propaganda kama ccm kuzusha uongo ili ku-draw attention ya wananchi? Tatu umesema nyie cuf kwa sasa hamsikiki kwakuwa siasa zimehamia bungeni na kwabahati mbaya unasema kinachoandikwa zaidi ni malumbano ya posho za wabunge! Nafikiri Mtutuma hapo unajichanganya, hoja ya posho ilipoletwa bungeni ililetwa kwaajili ya posho zote na sio za wabunge tu labda wewe mwenzetu ulipitwa na hukujua ilipoanzia, ila kwa mtoa/watoa hoja kuonyesha mfano wa uongozi akaanza kwa kuzikataa posho za ubunge na hapo ndipo vyombo vya habari vilipojikita. Kama ulikuwa makini hata uchambuzi wa bajeti umefanywa kwa kina na kambi rasmi ya upinzani kiasi cha mwananchi wa kawaida kuielewa, ninachotaka kukuhabarisha tu ni kwamba wale wabunge wote ambao ni mwiba kwa serikali na ccm wamekuwa wakisumbuliwa kwenye mijadala bungeni kiasi cha bunge kuonekana ni mahali pa vijembe lakini elewa kwamba wananchi ndio majaji wa mijadala na wamefunguka akili sio wale wa zama zile.
   
 17. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kumbe CUF bado wapo? Duh!
  Walikuwa wamesahau kabisa kuwa Nchi hii ikiwa na Matatizo tunaumia wote, na hivyo tunao wajibu wa msingi wa kuiepusha Nchi yetu na Viongozi wasiowajibika!
   
 18. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kauli nzuri inayohitaji uungaji mkono. Ila mmefail short kwa kutoitisha maandamno kwani ndio kitu inayomkosesha Jeykey usingizi. Well done Mtatiro, 2015 jivue gamba uingie CDM kwa wajasiri wenzio kwani wala tende na halua kukusariti ni dakika yoyote.
   
 19. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kudos CUF sasa itisheni maandamano maana tunataniana na washawishini Chadema. Hapo nilipoweka wino mwekundu ndio tatizo hasa la umeme kwamba hawataki CCM upatikane umeme wa uhakika kwani utaharibu dili za wakubwa na vigogo pale Tanesco.
   
 20. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,591
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  CUF mna mpango gani wa kuitisha maandamano kuhusu mgawo huu mkali wa mume?, so far kauli na tamko ni zuri, lakini wananchi tunitaji kutoa push kidogo kwa kutumia maandamano, je hili mmelifikiria?
   
Loading...