Taarifa ya CCM kukanusha uzushi kuwa Kikwete kakataa kumwachia uenyekiti Magufuli

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinatoa taarifa potofu kuhusu mchakato wa Mwenyekiti wa sasa wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti cha uongozi wa CCM kwa Rais John Pombe Magufuli kama ilivyo mila na desturi ya Chama Cha Mapinduzi.

Yamekuwepo madai eti Mwenyekiti amekataa au anachelewesha kukabidhi kijiti.

Habari hiyo sio kweli kabisa na ni kinyume chake, kwani Dkt. Kikwete amekuwa akisisitiza kukabidhi madaraka mapema iwezekanavyo. Kwa ajili hiyo kwenye kikao cha Mei 3, 2016 alikataa kusiongezwe agenda nyingine ambazo zitalazimisha Mkutano Mkuu Maalum kuchelewa kufanyika kwa sababu ya kukamilisha maandalizi ya agenda hizo. Alisisitiza agenda iwe moja tu.

Dhamira ya kufanyika Mkutano Mkuu maalum mwezi Juni, 2016 iko pale pale. Kilichoelezwa kwenye kikao ni kutaka kukamilisha utaratibu wa kupata fedha za kugharamia mkutano huo. Taratibu zikikamilika tarehe itapangwa. Mipango ya kutafuta pesa inaendelea na ikikamilika tarehe itatangazwa.

Tunawataka wana-CCM wasihamanike wala kubabaishwa na taarifa za upotoshaji zinazofanywa na watu wenye nia mbaya na CCM. Hawa ni wale wale ambao wamekuwa wakiiombea mabaya CCM bila ya mafanikio.

Pia tunapenda kukanusha madai ati kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwatahadharisha Wajumbe wa Kamati Kuu kuhusu ukimya wa Ndugu Edward Lowassa. Hakuna wakati wowote kauli kama hiyo aliitoa. Ni uzushi mtupu. Jina la Ndugu Lowassa halikutajwa kabisa.

Aidha, tunapenda kukanusha madai ya kufanyika mkutano baina ya Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa CCM kuhusu uchaguzi wa Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM. Hapajawahi kufanyika mkutano wa aina hiyo siku yoyote na mahali popote. Hivyo madai ya kuwepo kwa tofauti baina ya Viongozi wakuu kuhusu nani achaguliwe kuwa Katibu wa Wabunge wa CCM hayana msingi wowote.

Kamati Kuu iliteua Wabunge wanne kugombea na kuwaachia Wabunge wa CCM kuamua. Kuhusisha Viongozi na hasa kuzua kuwepo kutokuelewana ni jambo la kusikitisha. Ni taarifa ya uongo yenye nia ovu kwa CCM na Viongozi wake.

Tunapenda kuwatahadharisha waandishi wa habari kuandika habari za ukweli. Waache kuzua mambo yenye kupandikiza chuki na mgawanyiko usiostahili kuwepo ndani ya CCM na kuyaeneza kwa watu. Waheshimu maadili ya kazi zao.

Napenda kuwahakikishia na kusisitiza kuwa hakuna mgogoro wa kukabidhi kijiti cha uenyekiti katika CCM na wala hautakuwepo.

Imetolewa na;

Ndugu Christopher Ole Sendeka

MSEMAJI WA CCM

MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,

05/05/2016
 
haya tuhusu sisi tunajua kuwa mmekorogana basiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

nalala naamka nikijua mmekorogana sitaki mikanusho full stop
 
Mbona umemtaja Lowassa tena, hivi hamuwezi kutoa taarifa zenu bila kumtaja Lowassa, kuna nini mbona mnahangaika sana kukanusha taarifa hii
 
Nimeamini Lowasa alikuwa mizizi hatari ndani ya chama, ni ujasiri tu uliotumika kumkata.

Hatari ni pale atapootesha mizizi hiyo huko aliko, sidhani kama wataweza hata kumhoji.!
 
Mtahangaika sana kukanusha habari ambazo ziko kwenye public media.

Mpeni Magufuli uenyekiti wa chama bana, mbona mnamfanyia figisu ngosha??

Mnaogopa nini??
Mahafidhina na majizi humo kwenye kijani na njano hawataki hilo jambo.Wanauogopa huo moto wa 'Hapa Nazi Tu' hautawaacha salama.
 
Mnatuchanganya, eti sio kweli, mnatufanya sisi wajinga enheee, lengo lenu ni kumpunguza mtukufu raisi speed, tumewashtukia na tunamuombea mungu aendelee kuwatumbua tu. Mkanushe eti habari za uongo ,lakini watu tumeshawasoma.
 
Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinatoa taarifa potofu kuhusu mchakato wa Mwenyekiti wa sasa wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti cha uongozi wa CCM kwa Rais John Pombe Magufuli kama ilivyo mila na desturi ya Chama Cha Mapinduzi.

Yamekuwepo madai eti Mwenyekiti amekataa au anachelewesha kukabidhi kijiti.

Habari hiyo sio kweli kabisa na ni kinyume chake, kwani Dkt. Kikwete amekuwa akisisitiza kukabidhi madaraka mapema iwezekanavyo. Kwa ajili hiyo kwenye kikao cha Mei 3, 2016 alikataa kusiongezwe agenda nyingine ambazo zitalazimisha Mkutano Mkuu Maalum kuchelewa kufanyika kwa sababu ya kukamilisha maandalizi ya agenda hizo. Alisisitiza agenda iwe moja tu.

Dhamira ya kufanyika Mkutano Mkuu maalum mwezi Juni, 2016 iko pale pale. Kilichoelezwa kwenye kikao ni kutaka kukamilisha utaratibu wa kupata fedha za kugharamia mkutano huo. Taratibu zikikamilika tarehe itapangwa. Mipango ya kutafuta pesa inaendelea na ikikamilika tarehe itatangazwa.

Tunawataka wana-CCM wasihamanike wala kubabaishwa na taarifa za upotoshaji zinazofanywa na watu wenye nia mbaya na CCM. Hawa ni wale wale ambao wamekuwa wakiiombea mabaya CCM bila ya mafanikio.

Pia tunapenda kukanusha madai ati kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwatahadharisha Wajumbe wa Kamati Kuu kuhusu ukimya wa Ndugu Edward Lowassa. Hakuna wakati wowote kauli kama hiyo aliitoa. Ni uzushi mtupu. Jina la Ndugu Lowassa halikutajwa kabisa.

Aidha, tunapenda kukanusha madai ya kufanyika mkutano baina ya Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa CCM kuhusu uchaguzi wa Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM. Hapajawahi kufanyika mkutano wa aina hiyo siku yoyote na mahali popote. Hivyo madai ya kuwepo kwa tofauti baina ya Viongozi wakuu kuhusu nani achaguliwe kuwa Katibu wa Wabunge wa CCM hayana msingi wowote.

Kamati Kuu iliteua Wabunge wanne kugombea na kuwaachia Wabunge wa CCM kuamua. Kuhusisha Viongozi na hasa kuzua kuwepo kutokuelewana ni jambo la kusikitisha. Ni taarifa ya uongo yenye nia ovu kwa CCM na Viongozi wake.

Tunapenda kuwatahadharisha waandishi wa habari kuandika habari za ukweli. Waache kuzua mambo yenye kupandikiza chuki na mgawanyiko usiostahili kuwepo ndani ya CCM na kuyaeneza kwa watu. Waheshimu maadili ya kazi zao.

Napenda kuwahakikishia na kusisitiza kuwa hakuna mgogoro wa kukabidhi kijiti cha uenyekiti katika CCM na wala hautakuwepo.

Imetolewa na;

Ndugu Christopher Ole Sendeka

MSEMAJI WA CCM

MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,

05/05/2016
Mzee wa tumbo kubwa nilijua mtakanusha kiini ya habari kwamba mwenyekiti aligoma kujadili tarehe mngetuwekea hiyo tarehe kumbe content ni ile ile tu kama iliyoko mitandaoni?

Mwambie JK akabidhi mamlaka kwa wenyewe... Asisite maana unafiki chuki na wivu ndio malipo yake hayo... Leo asingekuwa wakuishi kwa hofu na mashaka!! Upashukuna na unafiki umemfanya ajikute akikabidhi madaraka kwa asiyemtaka wala kumtarajia!!

Mpeni CCM ngosha aiteketeze vizuri!!!
 
Pia tunapenda kukanusha madai ati kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwatahadharisha Wajumbe wa Kamati Kuu kuhusu ukimya wa Ndugu Edward Lowassa. Hakuna wakati wowote kauli kama hiyo aliitoa. Ni uzushi mtupu. Jina la Ndugu Lowassa halikutajwa kabisa.

LOWASSA BADO ANAWAPA ZA USOEEE TEH TEH
 
Sasa wale wandishi wametoa wapi habar ndefu vile!!!! kumbe tunaofatilia na kusoma magazeti tumelishwa uongo mwingi sana yaan gazeti la mwananchi lilivyo na kurasa nyingi vile unanunua ili usome kumbe yaliyomo ni uongo mtupu!!!!! bora niwe nafatilia taarifa ya habari na hotuba ya live basi haya mengine ni bure.
 
System Theory inatufundisha jambo moja muhimu,ENTROPY...Entropia ni tabia ya kila mfumo kufikia hatua ya kuchoka,kuzeeka na hatimaye kufa...the CCM establishment will eventually run down and die - surely,someday!
 
CC:- TandaleOne.
Hivi taarifa hizi chanzo chake ni wapi isijekuwa walipokutana hao wanne huenda walikuwa zaidi na ndio walioharibu. Na kusema hakuna kitu kama hicho ni kuzidi kupotosha na kutuchanganya wadau. Kupishana kwenye kukubaliana kupo as long as bado upo hai na hiyo ni afya ya akili.
Huenda mwenyekiti kaguswa na bei ya sukari kupaa mara tatu zaidi kwa miezi saba tu. Je kwa miaka 5 bei itakuwa sawa na mfuko wa sementi? Kama hajakomaa kuwa mwenyekiti msimharakishe badala yake mpeni semina elekezi. Au uoga umefika hadi huko ccm? Rudisheni maeneo ya wazi na mali mlizojimilikisha tangu 1992 serikalini.
 
Propaganda zetu tumezibaini kutaka kuonesha Ngosha ni mwenye heri huko chamani..Mnaitengeneza wenyewe kisha mnakanusha..
 
Back
Top Bottom