Taarifa: Uhakiki wa vyeti vya kidato cha 4&6 kwa Walimu na Watumishi wa Umma

Napendekeza iundwe wizara maalum ya uhakiki wa vyeti vya Elimu na Watumishi hewa maana naona mama Kairuk anabeba majukumu mazito sana kiasi kwamba ana concentrate kutangaza uhakiki kila siku kuliko kushughulikia matatizo mengine ya watumishi
 
Ushauri zoezi lijumuishe wote wanaotoa vyeti ili lifanyike mara moja na kuisha. iundwe timu ikiwa na watu wa TCU, NECTA, NACTE na wengine ili lifanyike kwa pamoja.
 
Hawa nao hawajielewi,mfano cheti changu kimetolewa na udsm,hao tcu wanawezaje kudhibitisha uhalali wa cheti changu pasipo udsm wenyewe?
 
Hawa nao hawajielewi,mfano cheti changu kimetolewa na udsm,hao tcu wanawezaje kudhibitisha uhalali wa cheti changu pasipo udsm wenyewe?
Mkuu hilo swali mimi nimejiuliza, TCU au NACTE, wataweza vipi kuhakiki cheti cha UDSM, UDOM, DIT, IFM et al, wakati wao hawatoi vyeti? Kwa upande wa NECTA ni sawa, lakini siyo TCU au NACTE.
 
Wafanya kazi laki tano wa umma toka may kweli zoezi hili limeshindwa kutekelezeka kwa wakati?kweli hawa mawaziri husika wamekosa utashi wa kutatua tatizo hili au ni siasa uchwara tu
 
Ukiwa na vyeti halali ulivovilowekea miguu kwenye beseni huna tatizo waje mchana au usiku alfajiri au jioni alasiri au adhuhuri,nyumbani au ugenini kanisani au msikitini mjini au kijijini. Njooni fasta
Haujui tu usumbufu wake, unakuta upo likizo inabidi kukatisha,vurugu kwa sababu hawana utaratibu mzuri, huduma kutotolewa kwa usahihi hasa mahospitali kila mtu anataka akahakiki kwanza, watumishi walioko vyuoni ndo shida wikii hii watu warirudi kwa ajiri ya form zilizotolewa tar 3 wamejaza wamerud mavyuoni.Hii tena kwa miezi 6 sijui wanarudi mara ngapi hapo pigia mtu anaetoka Mwanza mbeya.

Sent from mTalk
 
Mimi kuna kitu sielewi,hivi vyeti na utendaji kazi wa mtu vina uhusiano gani...badala ya kukagua wafanyakazi wanaofanya kazi chini ya kiwango kwasababu ya kukosa umahiri badala yake wanakagua hayo makaratasi,hawana hekima.
 
Back
Top Bottom