TAARIFA rasmi kutoka CHADEMA

TAARIFA rasmi kutoka CHADEMA

​viongozi wa ukawa msiwe na shaka sisi malofa huwa hatubadiliki tukisha amuwa ! Kura zetu zote ni kwa ukawa!
 
Niwatake wana ukawa tu kuwa, lolote lijalo mbele yetu.. Tulione kama upepo.. Upitao.. Huo ni msala upikwao na JM na sio upitao.. Ingawa hata ungekuwa ni msala upitao bado tusingea anguka.. Kama wanatengeneza hii ya m4c means wamekosa sera badala yake wanaamua kutumia sera na nembo za ukawa kuwachanganya watanzania wasio na uelewa juu ya m4c ukawa na m4c ccm.
 
Hata hii ni ya uzushi siyoo???
Imenifikia

Mwambieni Magufuli Duniani kote
Ni kujidanganya mweyewe kuwa

utaingia Ikulu kwa Jina lako mwenyewe bila taasisi iliyokutuma !!!!
 

Attachments

  • 1442661392248.jpg
    1442661392248.jpg
    52.2 KB · Views: 241
sikuna sheria ya makosa ya mtandao? Kwanini chama kisiwasilishe tuhuma hizi ili wahusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua stahiki?

Ili kukomesha hili genge la watu kuleta taharifa za kupika kwenye mitandao?
Anayeilipa mishahara tume ya mawasiliano ndio huyo huyo anaye fadhili genge hilo hilo la kueneza uongo. Hivyo hao ni mapacha au ndugu
 
Kama hii taarifa ni ya kweli bado nina mswali kwa Makene..
- Kwanini uongozi umechelewa sana kukanusha huu uvumi?

- Mbona Makene hujatumia account yako ya Jf ili kuuaminisha umma wa humu kwamba taarifa imetoka kwako?

Kuna tatizo ndani ya ukawa ambalo haliwekwi wazi.

Makene alishahama UKAWA, anasubiri tu kukabidhi gwanda, yupo tu huko kimwili
 
mimi sioni alichoandika huyu zaidi ya Pumba tupu sasa kwani uongo Mbowe hawked a Marekani?
 
Hizo ni mbinu za JM.. htuwezi kutikisika.. Ukawa ni wa1 ccm wataisoma number.. Ukawa tumejipanga kuondoa kunguni pale magogoni.. View attachment 288581[/QUOT]


kikao cha SG - Secretary General Kinana, Lubuva na Lukuvi....!!! 😨😨😨😨

Eti...? Kumbe hawa na Lubuva wanafanya yao..?

Lubuva, plz, na washafanya KIKAO...!!

Hii kitu hatari sana, UKAWA walipeleke kwa VIONGOZI HARAKA sana hili...!!
 
Salaam

Kuna taarifa ya kutunga inasambazwa kwa njia za mawasiliano ya mitandao ya kijamii hususan Facebook na WhatsApp ikieneza habari za uongo kuhusu Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe na Mgombea Urais wa CHADEMA anayeungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA, Edward Lowassa.

1. Chama hakijatoa taarifa yoyote kuhusu kuwepo kwa safari ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe. Hatujatoa taarifa hiyo kwa sababu hakuna habari ya Mwenyekiti Mbowe kusafiri.

Mwenyekiti Mbowe amekuwa kwenye campaign trail (field) ya Mgombea Urais katika maeneo kadhaa kabla ya kuendelea na shughuli zingine za campaign trail nje ya field, ofisini kwake jijini Dar es Salaam ambazo anaendelea nazo hadi sasa na leo Jumamosi, Septemba 19, atakuwa na mkutano na waandishi wa habari.

Ukiangalia kwa makini pia, taarifa hiyo ambayo imeitwa ni Barua ya Wazi kwa Vyombo vya Habari, haiko katika mwonekano wa taarifa sahihi na rasmi za chama ambazo huwa zinatolewa na/kwa uratibu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chama.

2. Mgombea Urais wa CHADEMA anayewakilisha pia vyama washirika wenza vinavyounda UKAWA (CUF, NCCR-Mageuzi na NLD) anaendelea na ziara za kampeni mikoani akiwafikia wananchi wa vijijini na mijini. Habari zingine tofauti na hizo ni mwendelezo wa wapinzani wetu yaani CCM kutaka kuhamisha mjadala wa uchaguzi wa MABADILIKO ili wapiga kura wajadili vitu vingine visivyokuwa muhimu kwenye wakati ambapo Watanzania wanajiandaa kuandika historia mpya katika nchi yao.

Kubadili mjadala ndiyo mbinu ambayo CCM wameamua kuitumia ili eti kuwachanganya wapiga kura ambao wamejikita kutaka kusikia UCHAGUZI wa MABADILIKO. Si mabadiliko ya sura ndani ya CCM ile ile, bali mabadiliko ya kiutawala na kimfumo, kwa kuiondoa CCM madarakani na kukabidhi dhamana ya uongozi wa serikali na nchi kwa vyama vinavyounda UKAWA.

Kujikita kujadili porojo na uzushi kwa sasa badala ya agenda za uchaguzi huu unaolenga Mabadiliko, ni kuisaidia CCM inayopoteza uhalali wa kisiasa kadri uchaguzi unavyokaribia ili hata uhalali wa kisheria ilionao sasa, ukahitimishwe hapo Oktoba 25, mwaka huu.
Hatutawaachia wapumue kwa sisi kuanza kujadili uongo wanaozusha. Wananchi wana matumaini makubwa na UKAWA. Wanaimba mabadiliko na Lowassa, Lowassa na Mabadiliko. Wanasubiri mabadiliko kutoka kwa CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.

Tunasimamia hapo kusonga mbele.

Makene
Safi saaaaaaaana
 
Back
Top Bottom