TAARIFA: Maendeleo ya Afya ya Kibanda

TAARIFA: Maendeleo ya Afya ya Kibanda

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,461
Taarifa ya maendeleo ya afya ya Kibanda jioni hii....


Habari za jioni wakuu,

Muda umekwenda lakini nimeona ni vyema tukashirikishana taarifa fupi tulizopata kutoka Afrika Kusini anakotibiwa Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda kama nilivyoahidi.

1. Tangu walipowasili jana katika hosipitali ya Milpark, Kibanda amekuwa akiendelea na matibabu kwa maana ya kufanyiwa vipimo mbalimbali vikiwamo CT Scan na X Ray hasa kichwani na sehemu nyingine za mwili ambazo zilipata majeraha.

2. Baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo, jopo la madaktari wenye ujuzi wa aina tofauti, walikuwa akitarajiwa kukutana ili kusoma taarifa ya matokeo ya uchunguzi huo, ili kutafsiri maana ya matokeo hayo kisha kutoa mwelekeo wa nini kinafuata au aina ya tiba anayopaswa kupata Kibanda.

3. Taarifa nyingine ni kwamba, imebainika kwamba mfupa laini (fizi) uliopo kati ya pua na mdomo ni kama umekatika. Hii natokana na nguvu na nyenzo walizotumia watesaji kumg'oa meno. Kutokana na hali hiyo ana maumivu makali sana kwenye kinywa chake.

4. Pia imebainika kwamba meno kama sita hivi katika kinywa cha Kibanda yamelegea. Haya ni tofauti na yale mawili yaliyong'olewa katika tukio la awali.

5. Kesho Ijumaa Jukwaa la Wahariri litakutana katika mkutano wa wahariri wote ili kujadili hatua zaidi za kuchukua kwa maana mbili; kwanza ni kuhusu matibabu na afya ya Kibanda na pili usalama wa waandishi wa habari kikazi.

6. Uongozi wa Taasisi iitwayo Southern African Investigative Journalism Forum umemtembelea Kibanda katika hosipitali ya Milpark na kueleza masikitiko yake kuhusu yaliyomkuta. Wameahidi kushirikiana na taasisi za kihabari za Tanzania, kuchunguza tukio hilo kwa lengo la kupata majawabu ya nini kilichojiri na sababu za unyama huo.

Tutaendelea kuwaarifu hatua kwa hatua jinsi tutakavyokuwa tukipata taarifa kutoka Afrika Kusini.


--

Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556
 
Mungu ampe nafuu,, nanyi waandishi sasa ni wakati wa kuwa wamoja isije kuwa kama wakati wa Mwangosi mnatoa tamko la kuacha kuripoti taarifa za Polisi (Iringa) then tunashuhudia kwenye vyombo vingine wanafanya hivyo alhali mwenzenu alifanyiwa kiu mbaya sana.

Neville, I have trust in you kwamba wewe ni jasiri, waongoze wenzio katika kipindi hiki kigumu...vyeo vya U-kuu wa Wilaya wanavyowafutia machozi (wanavyopewa hasa wale wanaojipendekeza kwa wakubwa aka the Salva and Muhingos) ni dhihaka kwa taaluma yenu.

My take:
Pole Kibanda, Inshallah Mungu atakuponya haraka ujumuike na familia yako mapema ukiwa buheri.
 
Asante sana Mkuu kwa kutimiza ahadi yako, sisi wengine tunaendelea kupiga magoti kumwombea mwenzetu na tunaamini Mungu atamponya na waliofanya vitendo hivi vya kinyama watabainika maana Mungu ni mwenye haki!
 
Ahsante mkuu ila ina huzunisha kwa yalio mfika
 
inauma sana,wanamtoa meno bila ganzi,i can imagine maumivu aliyopata.
 
Shukran kwa updates tuzidi kumwombea apone haraka
 
Susieni tena habari za polisi coz ati wanadai tukio hilo sio la kihalifu..there'z something behind.MEENA tunataraji tamko zito
 
...Mungu aendelee kumjalia afya iimarike.
Tanzania nahisi hatuelewi tunakoelekea.
 
Taarifa ya maendeleo ya afya ya Kibanda jioni hii....


Huo ndo utawala na sura halisi ya nchi yetu ambayo ETI tunaamini kuwa tuna amani. Ni sura halisi ya UTAWALA lulokuwa nao katka nchi yetu na ambao sasa umeanza kushamiri na hata tunataka kuaminishwa kuwa ni matukio ya kawaida tu.

Haihitaji kupata Shahada mbili kutambua UNAA unaofanywa na serikali kwa kutumia jeshi la Polisi na kujifanya wakitengeneza sinema mbalimbali bila kuzifikisha mwisho wake. WANACHUMA LAANA ITAKAYOWAWAKIA MIKONONI MWAO SIKU ZA USONI......

SINAO UHAKIKA KAMA TUTAFIKA SALAMA< NA HATA TUKIFIKA SALAMA NANI ATAWANUSURU WATAKAOUMIA NA LAANA YA WALAANIWA?
 
So sad..serikali inaepuka lawama ?? kama c kushiriki basi kuzembea usalama wa raia wake. Ni muda muafaka tena wamechelewa kwa waandshi wa habari kuungana na kusimama kidete hali inazdi kuwa mbaya na 2endako ndo kubaya mana uchaguz,katba siasa za ushndani...swal je,? Mkuu wa nchi anahusika ? Kama hahusiki mbona kimya?? Je,kinachotendeka ni chema machoni pake na n stahili kwa binadamu/raia?
 
Watanzania sote kwa ujumla tu wavumilivu hata litokee tukio lip!

Mi nazani huu si ubumilivu bali ni ujinga. Sijui kwanini tuna vichwa vya kuku kusahau kila saa. Wakati wa Mwamgosi na ulimboka yalibebwa mabango wee kila koba baada wati wakasizi. Mungu ampunguzie maumivu
 
Mungu amjalie kupona haraka. Na zaidi naomba awafichue wahalifu waliohusika na kitendo hiki cha kinyama kisichomithilika.
 
Mungu awe nae...ipo cku yatawekwa wazi...hakuna maref yasiyokua na ncha
 
Du aki kuna binadamu wabaya,waliotenda walaaniwe mpa kwenye unyayo wa miguu,yaani hawa wamezaliwa na wanawake kweli?ole wa mama aliyezaa watu wa namna hyo,kha kha kweli Mungu ingilia kati
 
Watanzania sote kwa ujumla tu wavumilivu hata litokee tukio lip!

Mkuu tofautisha uvumilivu na kutojitambua; Amini usiamini matukio ya kutekwa na kuteswa kwa waandishi wa habari na serikali ikiendeleza utamaduni wake wa kutoa majibu ya kukera, hayawezi tokea nchi yoyote ile isipokuwa Tanzania.
 
Hebu pata picha kama uliwahi ng'oa jino ganzi ikiisha maumivu unayoyapata. Sasa mateso haya jamani duh hata kama ni kwaresma basi mwenzetu ameshiriki kikamilifu. Inauma sana
 
tumuombee kwa Mungu amponye ndugu yetu Absalom Kibanda.
kwa Mungu hakuna linaloshindikana.
 
Back
Top Bottom