TAARIFA: Maandalizi ya Heshima za mwisho na Mazishi ya Mh Bob N. Makani

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
By CHADEMA

TAARIFA: Heshima ya mwisho kwa mpendwa wetu Bob N. Makani zitatolewa kesho; Juni 11, 2012 kuanzia saa 6 mchana, Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam

UDATES:

Kwa mjibu wa vyanzo vikuu vya habari vya CHADEMA,

Taarifa rasmi ya ratiba kamili ya msiba huu mkubwa wa mwasisi wa Chama cha Ukombozi mpya wa Tanzania (CHADEMA) itatolewa wakati wowote kuanzia sasa!

Taifa liungane katika msiba huu!
 
May his soul rest in peace. Chama ulichokiasisi kimewafungua watanzania wengi macho.
 
Mi nashauri wahusika waweke ratiba kamili hii tuliosikia kwenye vyombo vya habari Marehemu Bob Makani ni public Figure
 
By CHADEMA

TAARIFA: Heshima ya mwisho kwa mpendwa wetu Bob N. Makani zitatolewa kesho; Juni 11, 2012 kuanzia saa 6 mchana, Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam
Duh itabidi nihudhurie manake hapo Karimjee pananikumbusha mwaka 1993 tulipoandamana kwenda Bungeni kufikisha kilio cha wapinzani kunyanyaswa. Tulitoka Viwanja vya mnazi mmoja tukapita makao makuu ya CHADEMA pale kisutu tukaelekea Karimjee. Lakini tulipofika tu hapo lilipo jengo la PPF tower tulikumbana na mkono wa sheria. Tukapigwa mabomu na kutawanywa lakini kila mtu kwa njia yake tulifika viwanja vya Karimjee. Pamoja na wapiganaji wengine tulikuwa na Marando, Bob, Ngwilulupi, Lamwai na wengine wengi naona naanza kuwasahau. Bob alikuwa msitati wa mbele na nakumbuka kabla hatujatawanywa aliwaamutu viongozi waliokuwa mbele washikane mikono na kusonga mbele
 
Mkuu Kimbunga kumbe umeanza harakati za siasa siku nyingi, huyu Mzee Makani nilikuwa namkubali sana nakumbuka wakati anagombea ubunge pale Shinyanga Mjini nilifika pale kwenye mikutano yake uwanja Kambarange na Ngokoro.
 
Last edited by a moderator:
UDATES:

Kwa mjibu wa vyanzo vikuu vya habari vya CHADEMA,

Taarifa rasmi ya ratiba kamili ya msiba huu mkubwa wa mwasisi wa Chama cha Ukombozi mpya wa Tanzania (CHADEMA) itatolewa wakati wowote kuanzia sasa!

Taifa liungane katika msiba huu!
 
Mkuu Kimbunga kumbe umeanza harakati za siasa siku nyingi, huyu Mzee Makani nilikuwa namkubali sana nakumbuka wakati anagombea ubunge pale Shinyanga Mjini nilifika pale kwenye mikutano yake uwanja Kambarange na Ngokoro.

Aisee,kumbe ritz ulikuwepo na ulishuhudia jinsi Mzee Bob Makani alivyomchachafya 'Ng'wana Derefa'?na uliona jinsi CCM ilivyoanza kuchakakachua kura siku nyingi?..eeh pale ni NGOKOLO-sio Ngokoro (Wasukuma hawana 'R'). Unakumbuka pia picha yake (bango) la Bob lilivyokuwa limesheheni CV nzito (ingawa lilikuwa black and white)?Unakumbuka alivyokuwa akivuta umati wa watu na msisimko katika mikutano yake? Hiyo ilikuwa miaka ya tisini(Then watu wanasema mageuzi Shinyanga yameanza juzi!!).
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kimbunga kumbe umeanza harakati za siasa siku nyingi, huyu Mzee Makani nilikuwa namkubali sana nakumbuka wakati anagombea ubunge pale Shinyanga Mjini nilifika pale kwenye mikutano yake uwanja Kambarange na Ngokoro.

ritz nimeshihudia mageuzi ya nchi hii yanavyoanza. Nimeshuhudia vyama vya upinzani vinavyoanza. Kuna watu humu hawajui kama CDM ilikuwa na makao makuu pale kisutu na kama NCCR ilikuwa na makao makuu pale Aggrey.

Mkuu nilishiriki katika kampeni kule Shinyanga tukiwa upande wa Bob tukipambana na Ng'wana Derefa. Mzee Makani alikuwa tishio na sauti yake iliyokuwa ikiunguruma. Tumeanza mbali tumewaachia vijana wale matunda japokuwa nasikia wanalalamika kiwa matunda hakuna kwa kuwa kuna kikindi kidogo cha watu ndio kimejimilikisha matunda hayo.
 
Last edited by a moderator:
pamoja mkuu,mimi nafahamu ila nilikuwa namjibu yule aliyesema kuwa ataenda kuzikwa kaskazini,ndo nikamuuliza kwanini akazikwe kaskazini wakati kwao shinyanga?huyu mzee namfahamu sana,hadi watoto wake nawafahamu
Watasafiri jumanne kwa ajili ya mazishi nyumbani shinyanga mkuu!
 
Back
Top Bottom