Taarifa Kwa Vyombo vya Habari Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by abdulahsaf, Aug 9, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Waziri Wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbaruok

  [h=3][/h]

  SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
  WIZARA YA HABARI UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Idara ya Habari(MAELEZO) tunawakumbusha tena waandishi wa habari juu ya ulazima wa kuwa na kitambulisho cha kufanyia kazi ya uandishi wa habari Zanzibar kilichotolewa na Idara ya Habari Maelezo(Press Card) kwa mujibu wa sheria Zanzibar.

  Aidha, waandishi wa habari kutoka nje ya Zanzibar hawataruhusiwa kufanyakazi ya uandishi wa habari mpaka pale amepata ruhusa ya Idara ya Habari Maelezo kwa mujibu wa sheria ya usajili magazeti N0 5 ya mwaka 1988 ya Zanzibar.

  Kutokana na hali ilivyojitokeza hivi sasa duniani, tunashauri vyanzo vya habari ikiwemo viongozi wa Serikali wakiwemo Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Waziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na wasemaji katika Taasisi mbalimbali kutotoa taarifa zozote kwa vyombo vya habari kwa mwandishi ambaye hana Press Card iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

  Hivyo, kuanzia tarehe 1/09/2012 waandishi wa habari wote wakiwa kazini ni muhimu kuonyesha kitambulisho kilichotolewa na Idara ya Habari Maelezo.

  Aidha,, tunasisitiza kwamba kwa mujibu wa sheria ya usajili wa magazeti sheria N0 5 ya mwaka 1988,kifungu cha 13 kinasisitiza kwamba mtu yeyote atakayechapisha Kitabu, Magazeti, Vipeperushi, Vijarida,Ramani na Chati lazima awasilishe nakala tatu si zaidi ya siku 14 baada ya kuchapishwa kwa Mrajis Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

  Kutofanya hivyo ni kwenda kinyume cha sheria ya Usajili Magazeti na Vitabu N0 5 ya mwaka 1988 hatua za kisheria zitachukuwa kwa atakayekiuka.

  IMETOLEWA NA:
  IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR
  09/08/2012
   
 2. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kumekucha Zanzibar.
   
 3. d

  danizzo JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dola ya ludi yakhe!?
   
 4. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,097
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hahahaha! Wazanzibari bana! Haya na watekeleze vizuri. Si muda mrefu watasema huruhusiwi kupata mafuta petrol station hadi uwe na ID ya Uzanzibari. All the best.
   
 5. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,823
  Likes Received: 2,587
  Trophy Points: 280
  Work permit requiment ipo njiani!
   
 6. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Hafidh Ali upooo!
   
Loading...