Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka CCM kuhusu matukio ya Tanga

kamati ya ufundi january anachekesha kweli. tulitazamia angelaani kwa nguvu zote kitendo cha vijana aliowakodisha wakavuruge mkutano wa ukawa kule bumbuli lakini leo anakuja na urongo usio na mashiko kutaka kutuaminisha ati wafuasi wa ukawa walitupa mawe ofisi za ccm. kwa taarifa ya january na ma-ccm wengine ni kuwa sisi tulipokuwa tunatoka mkutanoni kwa makundi tukirejea majumbani polisi walitupiga mabomu na kila mtu akakimbia kivyake. labda january kabla hajasema urongo huu atutupie clip moja inayoonyesha wafuasi wa ukawa wakirusha chupa za mikojo. sisi ni wastaarabu sana japo kina january wanadhani kuwa wanayo hatimiliki ya tanzania yetu.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama cha Mapinduzi kinasikitishwa na kitendo cha wafuasi wa vyama vinavyounda UKAWA kupiga mawe na kutupa chupa, baadhi zikiwa na mikojo, kwenye Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga jana, tarehe 28 Septemba 2015, kabla na baada ya mkutano wao wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tangamano, Tanga Mjini.

Kama ilivyo kawaida yetu miaka yote, CCM iliazimia kufanya kampeni za amani, zinazoheshimu sheria za nchi na utu wa wapinzani wetu. Hadi sasa, tumeweza kuwadhibiti wapenzi, washabiki na wanachama wa CCM wasifanye vitendo vya ufunjifu wa amani.

Tukio la Tanga sio la kwanza. Tarehe 27 Septemba 2015 viongozi wa UKAWA waliwapanga vijana, katika eneo la stendi ya Uyole, mkoani Mbeya ili wasimamishe msafara wa Mgombea wa Urais wa CCM na kumfanyia vurugu na kumpigia kelele ili wananchi wasimsikie vizuri. Ingawa Mgombea wetu alifanikiwa kukabiliana na hali hiyo, tunaamini kwamba huu sio ustaarabu. Washabiki wa CCM pia wana uwezo wa kupanga na kufanya mambo haya, tena kwa ufanisi mkubwa zaidi. Lakini viongozi wa CCM wa ngazi zote wamekuwa wanawahimiza wasifanye mambo haya kwasababu CCM hatuamini kwamba hiyo ni njia sahihi ya kuomba ridhaa ya Watanzania kuliongoza taifa letu na pia, kwa kuwa sisi ndio tuliokabidhiwa na Watanzania nchi hii kuiongoza, tunafahamu dhamana yetu kubwa ya uongozi wa taifa na ulinzi wa amani ya taifa letu.

Tunawasihi wenzetu wa UKAWA kwamba, katika kipindi hiki cha kampeni kilichobaki, tufanye kampeni kwa amani ili tumalize uchaguzi kwa amani na taifa liendelee kuwa na amani baada ya uchaguzi. Wenzetu wa UKAWA wasitufikishe mahala ambapo washabiki wa CCM watashindwa kuvumilia kuona Chama chao na viongozi wao wanadhalilishwa.

Tukio la Tanga la Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga kupigwa mawe limewaudhi na kuwakera wana-CCM na wapenda amani wote wa Tanga. Hata hivyo, tumewasihi wana-CCM wasilipize kisasi. Chama chetu kina dhamana ya uongozi wa nchi na ulinzi wa amani ya nchi yetu. Wenzetu dhamana hiyo hawana. Chama chetu kina uhakika wa kushinda na kushika dola, wenzetu wana uhakika wa kushindwa na wamekwishakata tamaa.

Tunawapongeza wana-CCM kote nchini kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha kampeni. Tunawashukuru kwa kubaini na kutoyumbishwa na propaganda za wenzetu ikiwemo ya Tanga, kwamba mkutano wa Tanga uliahirishwa kwasababu watu walikuwa wengi. Itakuwa ni mara ya kwanza katika historia kwamba mkutano wa kampeni unaahirishwa kwasababu ya wingi wa watu. Katika mikutano ya kampeni, ikiwemo ya CCM, na hata katika sherehe za kitaifa, baadhi ya watu huzidiwa nguvu na huhudumiwa na wahudumu wa huduma ya kwanza huku mikutano ikiendelea.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa wenzetu kutafuta kisingizio cha kutofanya mikutano ya kampeni. Mkutano wa kampeni ya UKAWA wa Geita pia waliuahirisha kwa kisingizio tofauti, kwamba jukwaa na vipaza sauti havikuandaliwa ingawa aliyetangaza kuahirisha alisimama jukwaani na akasikika na watu wote. Mabadiliko wanayoyahubiri wenzetu yanaanza na kusema ukweli. Imefika mahali sasa wenzetu wa UKAWA wawaeleze ukweli Watanzania kuhusu mgombea wao kushindwa kuhutubia baadhi ya mikutano au kuhutubia kwa dakika 3 kuliko kuwahadaa kwa kutengeneza matukio na vioja ili kuficha mapungufu ya mgombea wao.

Tunarudia kuwataka viongozi wa UKAWA kuacha kupanga vurugu, kuharibu mali za CCM, na kutukana wana-CCM. Tunarudia kuwataka waache kauli zao za kuibiwa kura. Kauli hizo ni za kukata tamaa na kuwandaa watu kufanya fujo. Tunadi sera zetu na wagombea wetu kwa amani ili tuwape Watanzania fursa ya kuchagua kwa amani ili taifa liendelee kuwa la amani, umoja, utulivu na mshikamano mara baada ya uchaguzi.

Imetolewa na:

January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
29.09.2015
 
Kuna wanaotukana kama viongozi wa CCM?

Zile fujo zilizoanzishwa Tarime na moja wa kada wa Chadema kuuwawa zilianzishwa na chama gani?... Acheni siasa uchwara

Naona Makamba anatafuta nafasi ya uwaziri Mkuu kwa nguvu zote... Unatoa tamko kama nani?. Nape yuko wapi, Kinana yuko wapi, Mangula yuko wapi?... Wewe ni msemaji wa CCM?
Agcr1cDsxIv-PdQ62lzxEoxHqKO9jgF1rSnSLNM9ZAUp.jpg
 
Hawa watu narudia wameachwa sana, kiroba chako usumbue wengine nimuda Wa kuliangalia hili
 
Yaani kuwa mjumbe ndio unakuwa msemaji mkuu? Hiyo halmashauri na hiyo kamati hazina viongozi? maana sasa Makamba ndiye msemaji...anyway, hayo tuwaachie wenyewe..Ila tu akumbushwe kuwa yeye hapo anapiga propaganda wala hasemi wala kusimamia kweli. Sihitaji kufafanua.
 
January Makamba ni mjinga! Chama kilichoasisi siasa za kijinga kwenye huu uchaguzi ni CCM! Sasa ni jino kwa jino!

January Makamba ni mjinga!
 
Nadhani lengo kuu ni kupunguza maumivu waliyopata fisiem huko Tanga, sijaona mahali UKAWA wanalia lia kama JM, pamoja na kutukanwa matusi ya aina zote
 
Huyu jamaa aliyeiba mtihani wa form four Galanos na kufutiwa matokeo, akiwa waziri mkuu itabidi wengine tuhamie Kenya. Uzuri ni kwamba mwenyezi Mungu ana mawazo mengine na ametuletea Edward Lowassa kuwa rais wa tano wa JMT. Hao akina Makamba waendelee kujikomba wataishia kunawa. Watoto wa mjini wanasema hata aoge au avae nguo mpya, MJINI haendi. UKAWA ndio habari ya mjini
 
Sera gani mnazinadi zaidi ya matusi mliyobarikiwa kuyamwaga kwa jamii,nakuonyesha ndiyo Sera zenu za ccm
 
January kemea na yale matusi na udhalilishaji aliofanya Nape jana mjini Iringa,anawezaje kumuita mtu mwenye umri sawa na baba yake kuwa ni maiti?ndivyo mlivyofundishwa nyie kaka zetu mlioko ccm?kisa ni ugali tu?mbona sie wengine tunakula pasipo kutukana wazee wetu mbele ya kadamnasi ya watu?katika maisha lazima uishi kwa nidhamu tena ya hali ya juu.
Pili ulitaka mkutano uendelee ili yatokee maafa makubwa ya watu kukanyagana?mwisho wa siku tungelaumiana kwa mambo ambayo yangeweza kurekebishwa yasitokee?busara huwa inatuongoza kufanya nini?
Niwaulize?what are you smoking over there?
Ai_3ZdbIfrINYt3sCxAZeWOZ6MyOzorJxemvsMW4c9ao.jpg
 
Mwigulu jana hapa Karatu alivyotutukana wambulu kwa matusi yote akamalizia kuwaita wapinzani nyumbu nalo unasemaje.....
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama cha Mapinduzi kinasikitishwa na kitendo cha wafuasi wa vyama vinavyounda UKAWA kupiga mawe na kutupa chupa, baadhi zikiwa na mikojo, kwenye Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga jana, tarehe 28 Septemba 2015, kabla na baada ya mkutano wao wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tangamano, Tanga Mjini.

Kama ilivyo kawaida yetu miaka yote, CCM iliazimia kufanya kampeni za amani, zinazoheshimu sheria za nchi na utu wa wapinzani wetu. Hadi sasa, tumeweza kuwadhibiti wapenzi, washabiki na wanachama wa CCM wasifanye vitendo vya ufunjifu wa amani.

Tukio la Tanga sio la kwanza. Tarehe 27 Septemba 2015 viongozi wa UKAWA waliwapanga vijana, katika eneo la stendi ya Uyole, mkoani Mbeya ili wasimamishe msafara wa Mgombea wa Urais wa CCM na kumfanyia vurugu na kumpigia kelele ili wananchi wasimsikie vizuri. Ingawa Mgombea wetu alifanikiwa kukabiliana na hali hiyo, tunaamini kwamba huu sio ustaarabu. Washabiki wa CCM pia wana uwezo wa kupanga na kufanya mambo haya, tena kwa ufanisi mkubwa zaidi. Lakini viongozi wa CCM wa ngazi zote wamekuwa wanawahimiza wasifanye mambo haya kwasababu CCM hatuamini kwamba hiyo ni njia sahihi ya kuomba ridhaa ya Watanzania kuliongoza taifa letu na pia, kwa kuwa sisi ndio tuliokabidhiwa na Watanzania nchi hii kuiongoza, tunafahamu dhamana yetu kubwa ya uongozi wa taifa na ulinzi wa amani ya taifa letu.

Tunawasihi wenzetu wa UKAWA kwamba, katika kipindi hiki cha kampeni kilichobaki, tufanye kampeni kwa amani ili tumalize uchaguzi kwa amani na taifa liendelee kuwa na amani baada ya uchaguzi. Wenzetu wa UKAWA wasitufikishe mahala ambapo washabiki wa CCM watashindwa kuvumilia kuona Chama chao na viongozi wao wanadhalilishwa.

Tukio la Tanga la Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga kupigwa mawe limewaudhi na kuwakera wana-CCM na wapenda amani wote wa Tanga. Hata hivyo, tumewasihi wana-CCM wasilipize kisasi. Chama chetu kina dhamana ya uongozi wa nchi na ulinzi wa amani ya nchi yetu. Wenzetu dhamana hiyo hawana. Chama chetu kina uhakika wa kushinda na kushika dola, wenzetu wana uhakika wa kushindwa na wamekwishakata tamaa.

Tunawapongeza wana-CCM kote nchini kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha kampeni. Tunawashukuru kwa kubaini na kutoyumbishwa na propaganda za wenzetu ikiwemo ya Tanga, kwamba mkutano wa Tanga uliahirishwa kwasababu watu walikuwa wengi. Itakuwa ni mara ya kwanza katika historia kwamba mkutano wa kampeni unaahirishwa kwasababu ya wingi wa watu. Katika mikutano ya kampeni, ikiwemo ya CCM, na hata katika sherehe za kitaifa, baadhi ya watu huzidiwa nguvu na huhudumiwa na wahudumu wa huduma ya kwanza huku mikutano ikiendelea.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa wenzetu kutafuta kisingizio cha kutofanya mikutano ya kampeni. Mkutano wa kampeni ya UKAWA wa Geita pia waliuahirisha kwa kisingizio tofauti, kwamba jukwaa na vipaza sauti havikuandaliwa ingawa aliyetangaza kuahirisha alisimama jukwaani na akasikika na watu wote. Mabadiliko wanayoyahubiri wenzetu yanaanza na kusema ukweli. Imefika mahali sasa wenzetu wa UKAWA wawaeleze ukweli Watanzania kuhusu mgombea wao kushindwa kuhutubia baadhi ya mikutano au kuhutubia kwa dakika 3 kuliko kuwahadaa kwa kutengeneza matukio na vioja ili kuficha mapungufu ya mgombea wao.

Tunarudia kuwataka viongozi wa UKAWA kuacha kupanga vurugu, kuharibu mali za CCM, na kutukana wana-CCM. Tunarudia kuwataka waache kauli zao za kuibiwa kura. Kauli hizo ni za kukata tamaa na kuwandaa watu kufanya fujo. Tunadi sera zetu na wagombea wetu kwa amani ili tuwape Watanzania fursa ya kuchagua kwa amani ili taifa liendelee kuwa la amani, umoja, utulivu na mshikamano mara baada ya uchaguzi.

Imetolewa na:

January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
29.09.2015

Makamba kabla hujalileta kwetu ungewapelekea viongozi wa matusi na kugawa watanzania kama Nape Makongoro Msukuma Lusinde na Bulembo ili walisome kwanza.
 
Kamweleze baba yako

Hivi we January unafikiri sisi hatujui nyie ccm mnayowafanyia ukawa?naona umekosa cha kuongea unataka kazi kick
 
Duuh comment yangu ya kwanza na ya pili ishanyofolewa.... Haya bana maboss hakuna shida.... Only 24 dayz remain
 
Hivi ccm wanadhubutu kutoa kauli km hii wakati jaji lubuva ametoka kuwaonya waache matusi majukwaani?nani anaongea lugha za kudhalulisha na matusi km sio viongozi wa ccm? Nape jana katukana sana, msukuma wote tulimsikia, Lusunde, pia Mwigulu wao kazi yao maalumu ni matusi. Sasa huyu analeta unafiki gani? Labda kashtushwa na mafuriko ya jana Tanga!
 
Back
Top Bottom