Taarifa kwa umma

Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,552
2,360
Katika kuendeleza utamaduni wetu wa uvumilivu wa kisiasa na kuheshimu mawazo tofauti, kulinda haki ya kutoa maoni na kusimamia misingi ya kupingana bila kupigana. Chama chetu kinasikitishwa mno na tabia iliyojitokeza ya baadhi ya watu, taasis za umma au binafsi, makampuni, mashirika, asasi za kiraia au serikali kuwa tabia ya kupinga au kuwa na maoni tofauti na chama chetu. Kwa maoni yetu sisi tunasimamia maslahi ya umma, na kwenye kila mauaji yanayojitokeza hatuna la kuwajibika wala hatustahili chembe ya lawama ila ni lazima kila mtu awe upande wetu kutupongeza na kuilaumu serikali. Tungependa wanachama, mashabiki na wapenzi wetu waendelee kutuunga mkono kwenye msimamo wetu huu wa utume. Pamoja na orodha ndefu ya watu, taasis, na mashirika tuliyoyasusia tunapenda kuongeza vitu vifuatavyo pia kuwa tumesusia kwani navyo vinarudisha nyuma juhudi zetu kuikomboa Tanzania kwa mtazamo wetu. Vitu hivyo ni :-
1) Jua 2)Mvua 3) Amani 4) Maendeleo
Tunawaomba muendelee kutupa ushirikiano bila kufikiria.
Imetolewa na Idara ya Ukosoaji.
 
Yani watumishi wa mafisadi hauwakosi katika maneno yao! Pole sana!

Kawaambie raia wako macho zaidi ya watarajiavyo!

ccm ni nuksi full!
 
Yani watumishi wa mafisadi hauwakosi katika maneno yao! Pole sana!

Kawaambie raia wako macho zaidi ya watarajiavyo!

ccm ni nuksi full!

Sikubaliani na wewe ila sintokutukana, kukebehi wala siwezi kuisusia JF. Tanzania bila kususa inawezekana nimekwisha chukua hatua.
 
Back
Top Bottom