Taarifa kwa Umma: Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ashiriki Ibada Takatifu ya Pasaka Dodoma

Kila kitu kina makusudio yake...

VP Mpango ni upande wa pili wa shilingi kwa JPM

Usishangae kwa baadae VP akaogopeka nchini + taasisi + maofisini kuliko mkuu wa nchi.

Huyu Mh ni noma.....nilipoanza kuuona ukorofi wake ni wakati ule akizungumza na mameneja wa TRA mikoa ya nchi nzima kwa lugha ya kijeuri jeuri...akafukuza na watumishi
Tatizo mfumo huu wa uongozi huwa ni wa pure ujamaa na ujamaa si mfumo rafiki kwa wafanyabiashara.
 
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango amehudhuria ibada takatifu ya kuadhimisha sikuluu ya Pasaka Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.

Mheshimiwa Mpango akiwa ibadani hapo alipata fursa ya kuzungumza na Waamini walioshiriki pamoja na Watanzania
Muache hii mambo ya upuuzi!! Akishiriki ibada kuna haja gani tujue? Yeye kuomba Mungu ni ajabu gani? Pumbuavu sana acheni stupid nonsense zenu!!!
 
Wameanza ujinga wao,dadeki, mambo ya kusali au kuswali yanatuhusu nini sisi!

Sasa subiri tuone huo ujinga wao utampelekea wapi unatuletea umagufuli sisi!
 
Kusali, kuswali ni masuala ya kibinafsi sana. Nakerwa na tabia za viongozi kila waendapo kusali au kuswali, kuongozana na makamera na kuutaarifu umma. Hizi tabia alikuwa nazo Rais Daniel Arap Moi ambaye pia alijiita mtukufu.
Nyakati za utawala wake kule nchini Kenya, kila jumapili ilikuwa lazima aende kusali na kwenye taarifa ya habari ya KBC, habari ya kwanza ilimuhusu yeye, amesali wapi.
Ninawashauri viongozi wangu wa awamu ya sita wasiiendekeze tabia hii, haina tija yoyote kwa Watanzania. Watanzania tunataka kutaarifiwa masuala ya maendeleo sio nani kasali/kaswali wapi.
 
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amehudhuria ibada takatifu ya kuadhimisha sikuluu ya Pasaka Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.

Mheshimiwa Mpango akiwa ibadani hapo alipata fursa ya kuzungumza na Waamini walioshiriki pamoja na Watanzania
Mh. Makamo wa Rais Dkt. Mpango nakushauli uachane na tabia ya kutoa matamko ukiwa kwenye Ibada, achana kuongelea mambo ya Kaizari ukiwa Kanisani.

Ukienda Kanisani wewe pata ibada yako and then ondoka zako. Fanya kama walivyokuwa wanafanya akina; Mwl. Nyerere, Mwinyi, Mkapa hata na JK wakati wa awamu ya 4.

Ukinyanyuka kwenye kiti chako uwapo kanisani na kwenda kuongea ukaribishwapo waumini wataondoa attention yoote ya ibada na kuipeleka kwako hivyo kuondoa uwepo wa ibada. Nakushauli tena achana na tabia hizo, na itakujengea heshma kubwa kwenye jamii. Kanisani ni mahali pa kuabudu na kumsikiliza mchungaji, askofu, padri, kwa misikitini sheikh n.k.

Asante!
 
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amehudhuria ibada takatifu ya kuadhimisha sikuluu ya Pasaka Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.

Mheshimiwa Mpango akiwa ibadani hapo alipata fursa ya kuzungumza na Waamini walioshiriki pamoja na Watanzania
Aisee
 
Asijiingize katika utaratibu wa kutoa matamko kanisani kama alivyokuwa Mwendazake.
Anakoelekea huyu ni kulekule, nyumba za ibada zibaki kwa ajili ya ibada.
Viongozi wa siasa mbona wana uwanja mpana sana wa kuzungumza na Taifa siyo lazima kanisani
 
Mmeanza tena na taarifa za ajabu ajabu.

Sasa hii taarifa inamanufaa/mchango gan kwa wananchi?
Aya msisahau kututarifu na rais akienda mskitin kuswali
 
wameanza ujinga wao,dadeki!

mambo ya kusali au kuswali yanatuhusu nini sisi!

sasa subiri twone huo ujinga wao utampelekea wapi!

unatuletea umagufuli sisi!
Unaongea kama nani sasa...

Mwenzio ni VP wa nchi,wewe ni balozi wa majungu.

Kwani hafahamu hilo?
 
Mwacheni mwenda zake akwende na upuuzi wake!! Sisi hatutaki tena mambo ya HOVYO/KISHAMBA Tanzania.
 
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amehudhuria ibada takatifu ya kuadhimisha sikuluu ya Pasaka Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.

Mheshimiwa Mpango akiwa ibadani hapo alipata fursa ya kuzungumza na Waamini walioshiriki pamoja na Watanzania

Kwa kiongozi wa kisiasa sio utaratibu mzuri baada ya misa kuzungumza kanisani, sio mahali pake, hii tabia itamea itakuwa mbaya sana
 
Back
Top Bottom