Taarifa kwa Umma kuhusu kujipiga risasi kwa mtu mmoja

cheusimangala_

Senior Member
Dec 1, 2018
114
174
Ndugu Wanahabari, Tarehe 18.08.2019 muda wa saa 05:00hrs alfajiri katika Nyumba ya Shirika La Nyumba la Taifa iliyopo Plot namba 3 na 4, eneo la Soko Kuu la Arusha, Kata ya Kati katika Halmashauri ya Jiji la Arusha Faisal S/O Salimu Ibrahim (19), Mhindi, Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Arusha Meru alijiua kwa kujipiga risasi moja kichwani katika paji la uso katika chumba chake kwa kutumia bunduki aina ya Rifle Winchester inayomilikiwa na Baba yake aitwaye Salim S/O Ibrahim (56yrs) wanaoshi pamoja katika nyumba hiyo.

Chanzo cha tukio hili ni msongo wa mawazo uliotokana na matumizi ya madawa ya kulevya. Aidha mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi wa Daktari.

Natoa wito kwa Makampuni,Taasisi na Watu binafsi wanaomiliki silaha, kutumia silaha hizo kwa umakini mkubwa na pia kuzitunza sehemu sahihi ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea endapo zitachukuliwa au kuibiwa na kutumika vibaya. Tutawafutia umiliki wale wote watakao zitumia silaha hizo kinyume na utaratibu uliowekwa na ambao watabainika kushindwa kuzitunza.

IMETOLEWA NA: ACP – JONATHAN SHANA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
 
Ogopa sana kitu kinaitwa msongo wamawazo ni hatari! Kama haujajiua utagongwa namagari
 
Wahindi Wana watu wanaotwa Koba, kazi yake mara nyingi ni kumaliza kadhia kwenye familia mfano: mzee anayeumwa Sana na amekuwa anatumia fedha za familia, Mtoto wa kihindi aliyezaa na mswahili na familia haitaki mchanganyo, n.k Koba huitwa kumaliza.

Hii story niadithiwa Lindi na Mzee mmoja hivi. Je Kuna mtu aliwahi kuisikia? Je tukio Kama hili laweza kuwa Ni kazi ya Koba?
 
Ni mara chache sana silaha inatumika for self defence

Bora kuachana nazo
 
Ndugu Wanahabari, Tarehe 18.08.2019 muda wa saa 05:00hrs alfajiri katika Nyumba ya Shirika La Nyumba la Taifa iliyopo Plot namba 3 na 4, eneo la Soko Kuu la Arusha, Kata ya Kati katika Halmashauri ya Jiji la Arusha Faisal S/O Salimu Ibrahim (19), Mhindi, Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Arusha Meru alijiua kwa kujipiga risasi moja kichwani katika paji la uso katika chumba chake kwa kutumia bunduki aina ya Rifle Winchester inayomilikiwa na Baba yake aitwaye Salim S/O Ibrahim (56yrs) wanaoshi pamoja katika nyumba hiyo.

Chanzo cha tukio hili ni msongo wa mawazo uliotokana na matumizi ya madawa ya kulevya. Aidha mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi wa Daktari.

Natoa wito kwa Makampuni,Taasisi na Watu binafsi wanaomiliki silaha, kutumia silaha hizo kwa umakini mkubwa na pia kuzitunza sehemu sahihi ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea endapo zitachukuliwa au kuibiwa na kutumika vibaya. Tutawafutia umiliki wale wote watakao zitumia silaha hizo kinyume na utaratibu uliowekwa na ambao watabainika kushindwa kuzitunza.

IMETOLEWA NA: ACP – JONATHAN SHANA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
Siyo wasiojulikana kweli. Tumsubiri kigogo2014 atatupatia taarifa kamili
 
Cheusi Mangala, wewe sio wa kutuletea taarifa rojorojo kama hizi. Wewe tunakujua kama HACKER mbobezi. Naona baada BCM kukiri kuwa ni sauti yake, umeamua kupotea.
 
Wahindi Wana watu wanaotwa Koba, kazi yake mara nyingi ni kumaliza kadhia kwenye familia mfano: mzee anayeumwa Sana na amekuwa anatumia fedha za familia, Mtoto wa kihindi aliyezaa na mswahili na familia haitaki mchanganyo, n.k Koba huitwa kumaliza.

Hii story niadithiwa Lindi na Mzee mmoja hivi. Je Kuna mtu aliwahi kuisikia? Je tukio Kama hili laweza kuwa Ni kazi ya Koba?
Hii hoja sio ya kupuuza.
Kujipiga risasi kwenye paji la uso kwa kutumia Winchester rifle sio kitu rahisi.
 
Huyu sio cheusimangala_ ninayemjua mimi, huyu ni cheupe mangala, hii habari ni ndogo sana kwako, ni sawa na kubeba majani ya ng'ombe watatu kwa kutumia scania semi trail, ni matumizi mabaya ya hela
 
Back
Top Bottom