Taarifa kwa umma kuhusu kesi ya Lipumba na wenzake

Tangazo limekaa kisanii kukwepa mkono wa dola.Maharagande ameogopa kuandika neno Chama cha cuf badala yake katumia neno Taasisi kukwepa kufungwa jela kwa kua hatambuliki na msajili,ameandika kwa kujificha
Inaonekana hata hiyo kesi yao wameshashindwa kabla ya kuanza kwa kukosa pia sifa
Ha ha haaa,wanaogopa vivuli vyao waende tu watapigiwa sauti na ndugu zao
 
Lipumba tumia busara,achana na CUF endelea na mambo mengine.Hichi unachokifanya ni kwa maslahi yako binafsi
 
Huu ni ujinga ambao Mimi binafsi siuafiki. Kukusanyika mahakamani kunasaidia nini?
Chama kinajua Lipumba sio Mwenyekiti na kavamia ofisi kama jambazi huku akipewa support na Msajiri, sasa jambazi unamuachia nyumba akivamia kwako?
Viongozi halali wachukue wanachama wao watiifu waende hapo Buguruni na kumtoa kwa nguvu Lipumba na kama shughuli hiyo itapoteza maisha ya watu basi damu hiyo itakuwa mikononi mwa msajiri na jeshi la Polisi wanao mbeba Lipumba.
Mali zilizopo pale ni juhudi na jasho la wanachama lazima zilindwe.
Amin alipo vamia Kagera kama tungesubiri mpaka tushtaki OAU au UN pengine kesi ya majadiliano ingekuwepo mpaka Leo.
 
CUF inaigiza siasa.
Vyama vya Upinzani Tanzania vimeshindwa kuonyesha kwa vitendo demokrasia vinayoihubiri.
Maalim na Lipumba utadhani ni manabii wa chama, miaka Nenda rudi viongozi ni haohao.
TUNAHITAJI MABADILIKO, TUNATAKA SURA MPYA, MAWAZO MAPYA NA FIKRA MPYA
Sidhani kama CUF wanaigiza siasa. Lipumba aliachia mawazo mapya, lakini CCM wakamrudisha kwa nguvu!
 
Maandamano ya kumusindikiza Lipumba kwenda kuvamia ofisi za CUF yalikuwa maandamano halali,maandamano ya kuwasindikiza viongozi wa CUF mahakamani yataitwa maandamano haramu.
 
Haya mambo ya kukaribisha wapenzi na wanachama Mahakamani kwa wingi maana yake nini na zipi ni faida zake kwa chama husika?
 
Wewe unaigiza nini
unataka kuwaondoa wapambanaji ili mshuke kitahisi.
CUF inaigiza siasa.
Vyama vya Upinzani Tanzania vimeshindwa kuonyesha kwa vitendo demokrasia vinayoihubiri.
Maalim na Lipumba utadhani ni manabii wa chama, miaka Nenda rudi viongozi ni haohao.
TUNAHITAJI MABADILIKO, TUNATAKA SURA MPYA, MAWAZO MAPYA NA FIKRA MPYA
 
Lipumba.png
 
Bila shaka umechoka na chama kilekile kuongoza vilevile,unahitaji na chama kipya kuongoza nchi.
 
Back
Top Bottom