Taarifa kwa umma kuhusu bei za mafuta aina ya petroli hapa nchini kuanziatarehe 10 n

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatangaza bei elekezi na bei kikomo za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 10 Novemba 2010. Pamoja na kutambua bei elekezi na bei kikomo za bidhaa mbali mbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia yafuatayo.

(a) Bei za aina zote tatu za mafuta, za jumla na reja reja hapa nchini zimepanda kidogo ikilinganishwa na toleo lililopita Ia tarehe 27 Oktoba 2010. Katika toleo hill bei za rejareja za mafuta zimepanda kama ifuatavyo: Petroli 2.49%, Dizeli (5000 ppm) 1.01%, Dizeli (500 ppm) 1.11% na Mafuta ya taa 1.89%. Mabadiliko haya ya bei za mafuta hapa nchini yametokana na kupanda kwa bei katika soko la dunia, bei zingepanda zaidi isingekuwa ni kwa sababu ya kupanda kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na dola ya Marekani, (sarafu ambayo huturnika katika manunuzi ya bidhaa za mafuta kwenye soko Ia dunia). Bei za jumla kulinganisha matoleo haya mawili zimepanda kama ifuatavyo: Petroli 2.59%, Dizeli (5000ppm) I .05%, Dizeli (500 ppm) 1.15% na Mafuta ya Taa 2.00%.

(b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei ya bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei elekezi za bidhaa za mafuta ikiwa ni pamoja na bei kikomo. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya naamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

(d) Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei
hizo ziko chini ya bei kikomo (price cap). Bei kikorno ni asilimia 7.5 ya bei elekezi kama ilivyokokotolewa na lomula iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapwa kwenye Gazeti Ia Serikali No. 5 la tarehe 9 Januari 2009.

(e) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ill kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.

(f) Vituo vyote vinavyouza dizeli yenye ubora tofauti (500 ppm na 5000 ppm), vinatakiwa kuonyesha kwenye
pampu za visima husika aina ya mafuta yanayouzwa. Kuuza dizeli tofauti na ile iliyoonyeshwa kwenye pampu ni kosa na itachukuliwa kama ni uchakachuaji wa mafuta ambapo adhabu kali itatolewa kwa mu husika.

(g) Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafiita endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

from: Bei mpya ya mafuta ya petroli Tanzania toka EWURA -
 
Hiyo ndo kasi zaidi, kuongoza kumewashinda washikaji sijui wanadhani indicators zipi zaidi ya hizi zioneshe kushindwa kuongoza nchi!- Kilavo na makame ndio mliotutangazia kuwa wataongoza taifa? This is a sad situation.:doh:
 
Back
Top Bottom