Taarifa kwa Umma - CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa kwa Umma - CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ochu, May 5, 2010.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2010
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  [​IMG] TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAAMUZI YA
  CHA KAMATI KUU.

  Taarifa inatolewa kwa umma kupitia kwa vyombo vya habari kwamba Kamati Kuu ya CHADEMA ilifanya kikao chake cha kawaida jumapili tarehe 25 mpaka tarehe 26 2010 jijini Dar es salaam katika Hoteli ya Markham kikiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe.

  Kikao hicho kilikuwa na ajenda zifuatazo:

  Kufungua kikao; Kuthibitisha Ajenda; Kuthibitisha muktasari wa kikao cha Kamati kuu cha tarehe 02/12/2009; Yatokanayo na Kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 02/12/2009; Taarifa ya Hali ya Siasa na Utendaji katika kipindi cha Disemba 2009 mpaka Machi 2010; Taarifa ya Kamati ya Wabunge; Uchaguzi wa BAVICHA ngazi ya taifa; Taarifa ya Halmashauri; Ratiba na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010; Taarifa ya Fedha Disemba 2009 mpaka Machi 2010 na Makadirio ya Bajeti ya Uchaguzi Mkuu 2010; Mengineyo na Kufunga Kikao.

  Yafuatayo ni maamuzi ya kikao hicho ambayo chama kinapenda kuwataarifu wanaCHADEMA na watanzania kwa ujumla katika ajenda mbalimbali:

  1.0 Kuthibitisha Ajenda na muktasari wa kikao cha Kamati kuu cha tarehe 02/12/2009 na kupitia yatokanayo na kikao kilichopita:
  Kamati Kuu ilithibitisha ajenda za kikao husika na muktasari wa kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 02/12/2009. Kamati Kuu imepitisha muundo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya chama. Kamati kuu ilijadili na kupitisha maamuzi mbalimbali kuhusu rufaa 13 zilizowasilishwa na wanachama mbalimbali kuhusu uchaguzi wa chama katika baadhi ya nafasi katika maeneo kadhaa nchini. Taarifa za maamuzi zitatolewa kwa warufani kwa kuzingatia katiba, kanuni na itifaki ya chama.


  Kamati kuu ilipokea taarifa na kuthibitisha Makatibu wa Wilaya/Majimbo/Mikoa katika maeneo ambayo vigezo vya kikatiba, kikanuni na kiutendaji vimetimizwa. Aidha kamati kuu imekasimu mamlaka kwa sekretariati ya Kamati Kuu taifa kuthibitisha makatibu katika maeneo yaliyowazi ama yatayokuwa wazi katika kipindi cha uchaguzi mkuu. Taarifa kwa mikoa/wilaya ambazo makatibu na sekretariati zao zimethibitishwa na ambazo hazijathibitishwa zitatumwa kwa mujibu wa itifaki kupitia mawasiliano ya kichama.

  2.0 Taarifa ya Hali ya Siasa na Utendaji katika kipindi cha Disemba 2009 mpaka Machi 2010

  Taarifa ya kina ya hali ya siasa Tanzania iliwasilishwa kwa kamati kuu ikiwa na sehemu kuu mbili; taarifa ya hali ya siasa kwa ujumla na taarifa ya utendaji ya chama. Taarifa hiyo itasambazwa ngazi mbalimbali za chama kwa kuzingatia itifaki na mawasiliano ya ndani ya chama.

  Kamati kuu iliipokea, kuitafakari, kuijadili na kufikia maamuzi yafuatayo ambayo CHADEMA ingependa wanachama na umma wayafahamu:


  Kamati Kuu ya chama imefadhaishwa na namna serikali inayoongozwa na CCM inavyoshindwa kuchukua maamuzi sahihi na kamili kuhusu masuala mbalimbali yanayoligusa taifa mathalani utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu Richmond; Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira; Unyama dhidi ya Wananchi Ngorongoro;


  Uchafuzi wa Maji ya Mto Tigiti wilayani Tarime; kushindwa kushughulikiwa hatua kamili kwa watuhumiwa wakuu wa ufisadi katika kashfa ya EPA, Tangold, Deep Green, Meremeta; Madai ya Muda mrefu ya Wafanyakazi Nchini nk. Kamati Kuu inaiona hali hii inayoendelea kama ishara ya udhaifu wa kiungozi ndani ya serikali na kufilisika kifalsafa na kimaadili ndani ya chama tawala na madhahara kuwa na hodhi (monopoly) ya chama kimoja katika vyombo vya maamuzi. Hivyo, Kamati Kuu inatoa mwito kwa watanzania kuendelea kuunganisha nguvu ya umma katika kutaka mabadiliko ya kweli katika taifa badala ya kupumbazwa mafanikio kiini macho yanaoenezwa kwa kutumia vibaya fedha za walipa kodi katika ziara za viongozi wa serikali zinazofanyika kwa wingi zaidi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.


  Kwa upande mwingine Kamati Kuu imepokea taarifa za utendaji wa chama katika kipindi cha Disemba 2009 mpaka Aprili 2010 na kupongeza mafanikio yaliyopatikana hususani kupitia Operesheni Sangara na hivyo kuazimia kwamba ziara za kichama ziendelee katika mikoa mingine nchini. Kamati Kuu imepitisha muundo wa chama na utambulisho wa wanachama wa CHADEMA Nje ya nchi; aidha kamati kuu ilipitisha viwango vya kiingilio kwa wanachama wa nje wa CHADEMA wanaoishi nje ya nchi.


  Kamati Kuu iliamua kuwa wakati ambapo marekebisho kwenye taratibu za Baraza la Wazee yanasubiri mchakato husika kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama; Sekretariati ya chama iidhinishe sekretariati ya Wazee iweze kufanya kazi kwa kuwahusisha viongozi wa wazee wa mikoa ya kichama ya Kanda Maalumu ya Dar es salaam.


  Kamati Kuu ilipokea mapendekezo ya awali toka kwa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) kuhusu taratibu za kuwapata wabunge na madiwani wa viti maalumu na kuekeleza marekebisho yafanyike na kuwasilishwa katika kikao kijacho.


  Pia, BAWACHA ishauri namna ya kushughulikia kikwazo cha kisheria ambacho kinalazimisha vyama kuwasilisha majina kabla ya uchaguzi mkuu kukamilika na hivyo kukosekana fursa ya kuteua wagombea kwa kuzingatia ufanisi katika matokeo ya uchaguzi.  Kamati kuu imepokea taarifa ya vitisho na hujuma zinazofanywa (na vyombo vya dola kwa shinikizo la CCM na serikali inayoongozwa na chama hicho) kwa viongozi wa chama na wawakilishi wa wananchi kupitia CHADEMA katika maeneo mbalimbali ya nchi.


  Kamati Kuu inalaani vitendo hivyo na kutoa mwito kwa wanachama na wananchi wapenda demokrasia na maendeleo kutoa taarifa ya vitendo vya namna hiyo vya kihalifu na uvunjaji wa haki za msingi za kikatiba vinavyofanywa.


  Kamati Kuu inatoa mwito kwa taasisi za kutetea haki za binadamu na washirika wa kimaendeleo kufuatilia kwa karibu hali ya kisiasa ya Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu yakiwemo maneno na vitendo vya viongozi wa vyombo vya dola na serikali kwa ujumla ili kuhakikisha mazingira ya uchaguzi yanakuwa huru na haki. Aidha Kamati Kuu inaelekeza sekretariati kuendelea kufuatilia kwa karibu hali hiyo na kuchukua hatua zinazostahili zikiwemo za kisheria ili kukabiliana na hali hiyo.


  3.0 Taarifa ya Kamati ya Wabunge na Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA
  Kamati Kuu ilitaarifiwa kuhusu kazi mbalimbali ambazo zimefanywa na wabunge wa CHADEMA kama sehemu ya kutekeleza majukumu kwa wananchi, chama na taifa kwa ujumla. Aidha kamati kuu imeelezwa taarifa ya kazi zinazofanywa na Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA za Karatu na Tarime.


  Kamati kuu imeazimia kuwapongeza wabunge wa CHADEMA kwa kazi nzuri wanayoifanya pamoja na uchache wao ambayo imeleta tija kwa taifa ikiwemo mathalani katika siku za karibuni kuishinikiza serikali ya CCM kuvunja mkataba na Kampuni ya RITES kwenye shirika la Reli nchini (TRL) na kupitishwa kwa Sheria mpya ya Madini.


  Aidha Kamati Kuu inazipongeza pia Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA pamoja na madiwani wake kwa kazi wanazofanya za kuutumikia umma kwa uadilifu na kutoa uongozi mbadala.  Hata hivyo, bado serikali ya CCM haijaweza kuwachukulia hatua waliohusika na kuingia mikataba mibovu na haijaweza kufanya mabadiliko kamili ya kisheria na kiuongozi yenye kuleta tija kamili kwa watanzania.


  Hivyo, Kamati Kuu imetoa mwito kwa watanzania kufanya mabadiliko ya mfumo wa utawala ili kuwa na uongozi na sera mbadala zitakazowezesha watanzania kunafaika kikamilifu na rasilimali za nchi yetu.


  4.0 Uchaguzi wa BAVICHA ngazi ya taifa:
  Kamati Kuu ilipokea taarifa kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Ngazi ya Taifa ambapo fomu za wagombea zilitolewa na kupokelewa kuanzia tarehe 7 Februari mpaka 2 mwezi Machi 2010. Kamati kuu ilipokea fomu za wagombea waliorudisha fomu katika kipindi husika.


  Kamati Kuu iliazimia kwamba tarehe ya uchaguzi wa Baraza la Vijana Ngazi ya Taifa isogweze mbele hadi tarehe itakayotangazwa na Kamati Kuu. Aidha maeneo ambayo BAVICHA ilishafanya uchaguzi katika ngazi za Mkoa, Wilaya, Majimbo na kata, ngazi husika zinatambuliwa rasmi na ziendelee kufanya kazi kama kawaida.


  Kamati Kuu ya chama inachukua jukumu la kuthibitisha makatibu wa BAVICHA katika ngazi husika na inakasimu mamlaka kwa sekretariati kutekeleza wajibu huo.


  Kamati Kuu imeunda Kamati Maalumu kuongoza shughuli za BAVICHA ngazi ya taifa katika kipindi cha kuanzia sasa mpaka baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.


  Kamati hiyo inaundwa na wafuatao:

  John Mnyika, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje (Mwenyekiti wa Kamati), Ali Chitanda, Afisa Vijana (Katibu wa Kamati), Regia Mtema, Afisa Mafunzo na Mjumbe wa Kamati Kuu ( Mjumbe), na Seleman Maabad Mohamed, Afisa Vijana Zanzibar (Mjumbe). Kamati Kuu iliazimia kuwa katika kufanya kazi za vijana sekretariati ya chama iunde sekretariati ya vijana ya muda kwa kuhusisha viongozi wa vijana wa mikoa ya Dar es salaam.

  5.0 Ratiba na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010
  · Kamati kuu ilithibitisha (kwa mamlaka iliyokasimiwa na Baraza Kuu) ratiba ya uchaguzi mkuu na ya vikao vya chama kuelekea uchaguzi mkuu 2010.


  Tarehe za kuchukua na kurudisha fomu kwa upande wa Udiwani, Ubunge na Uwakilishi ni kuanzia tarehe 3 Mei mpaka tarehe 9 mwezi Agosti 2010.


  Majimbo yamepewa fursa ya kupanga ratiba za maeneo husika kwa idhini ya sekretariati ya Kamati Kuu ndani ya mipaka ya tarehe iliyotolewa. Tarehe za uchukuaji fomu kwa nafasi ya Urais zitatangazwa katika hatua ya baadaye.


  · Kwa mujibu wa azimio la Mkutanao Mkuu wa chma 2005,Kamati Kuu ilipitisha mfumo wa kura za maoni (primaries) kabla ya vikao vya uteuzi wa awali na kuthibitisha uteuzi kufanyika kwa mujibu wa katiba. Kura za maoni za udiwani zitafanyika kwenye ngazi ya Tawi, za Ubunge kwenye eneo la Tarafa na za Urais kwenye ngazi ya Majimbo (Kanda).


  Maelekezo kuhusu namna kura husika zitakavyofanyika pamoja na wajumbe wataoshiriki yatatolewa kwa ngazi husika za chama.


  · Kura za maoni kwa wagombea nafasi za Udiwani, Uwakilishi, Ubunge na Urais zitafanyika katika kipindi cha kati ya Juni Mosi na Agosti Mosi. Majimbo yamepewa fursa ya kuandaa ratiba za maeneo husika kwa idhini ya sekretariati kwa kuzingatia mipaka iliyotolewa.


  · Uteuzi wa awali wa wagombea udiwani utafanywa na Kamati Tendaji za Kata kati ya Julai Mosi na Agosti Mosi; wakati uteuzi wa awali kwa upande wa Ubunge na Uwakilishi utafanywa na Kamati Tendaji za Majimbo kati ya tarehe 2 Agosti na 9 Agosti, 2010 kutegemea na ratiba zitazopangwa na ngazi husika kwa idhini ya sekretariati ya kamati kuu ya chama.


  · Mkutano wa Uteuzi wa Awali wa wagombea Ubunge wa Viti Maalum utafanywa na Halmashauri Kuu ya Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) tarehe 8 mwezi Agosti mwaka 2010. Kamati Kuu inatarajiwa kuthibitisha uteuzi wa wagombea Ubunge na Uwakilishi tarehe 10 Agosti 2010.


  ·Baraza Kuu la chama litapendekeza wagombea Urais na Makamu wa Rais wa Muungano na Rais wa Zanzibar na ilani ya chama tarehe 11 Agosti 2010 na Mkutano Mkuu utatea mgombea Urais na kuthibitisha ilani ya chama tarehe 12 Agosti 2010.Ratiba ya kuchukua fomu na kurejesha itatolewa na Kamati Kuu ijayo.


  · Kamati kuu ilipokea taarifa za maandalizi ya kisera/ilani, kioganizesheni, kimkakati, kisheria na kirasilimali kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kupitisha maazimio mbalimbali.


  ·Kamati Kuu imeridhia ushirikiano wa kimkakati na vyama vingine vya upinzani na kuruhusu ushirikiano wa ngazi ya chini kama utakavyoainishwa na vikao vya juu vya chama. Pale ambapo pataonekana panafaa.

  6.0 Taarifa ya Fedha Disemba 2009 mpaka Machi 2010 na Makadirio ya Bajeti ya Uchaguzi Mkuu 2010:


  Kamati kuu ilipokea taarifa ya fedha katika kipindi cha kuanzia mwezi Disemba 2009 mpaka Machi 2010.


  Kamati Kuu imepokea makadirio ya bajeti ya chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kuielekeza sekretariati kuendelea kuipitia kwa kuzingatia vipaumbele vya kimkakati pamoja na kuendelea kufuatilia vyanzo vya mapato. Kamati Kuu inakadiria kwamba kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 CHADEMA itatumia kiasi kisichozidi bilioni tano; kiwango ambacho kitahusisha kampeni zote za chama kwa ujumla wake kuanzia kwenye udiwani, ubunge na urais kwa matumizi yote ya uteuzi ndani ya chama pamoja na kampeni zenyewe. Chama hakina kiasi hicho cha fedha na mikakati inaendelea kuandaliwa na kutekelezwa kwa ajili ya kukusanya fedha kwa wanachama na wapenzi.

  7.0 Mengineyo
  Kamati Kuu ilipokea kama sehemu ya ufunguzi wa kikao taarifa ya Tanzia ya Marehemu Balozi (Mstaafu) Christopher Ngaiza na kikao kilisimama kwa dakika moja ya ukimya kwa heshima yake kutokana na mchango wake katika chama.


  Kamati Kuu ilipokea na kuidhinisha taarifa ya Mwenyekiti kumteua Wakili Edson Mbogoro toka Ruvuma kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.


  Taarifa imetolewa tarehe 2 Mei 2010 na:

  ………………
  Katibu Mkuu,
  Dr Wilbroad Slaa(Mb)
   
 2. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2010
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Chadema haina jipya katika siasa za Tanzania,wakae na ukilimajaro/Umoshi wao!
   
 3. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Rutunga M, sioni huo ukilimanjaro/umoshi katika miniti hizi! Mwaka huu mtazuga kikwelikweli! Hebu fikiria kama vyama vyote vingekuwa vinatoa taarifa kwa uma kwa namna hii ya Chadema! Dr Slaa asante kwa kutupa taarifa, kazeni mwendo.
   
 4. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Chadema alutacontinua, hakuna kurudi nyuma, jaribuni kuwa makini nia watu kama akina Rutunga M. Kama Rutunga haumo siukae kimyaaa.
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  umefilisika kichwani
   
 6. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2010
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160  Kuwa kwenye nini

  chadema imejaa ukabila huo ndiyo ukweli,
  Tazama viti maalum ,uongozi nk

  Ni chama chenye malengo safi lakini hilo kwao/kwenu ni DOA
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nahisi wewe ni miongoni mwa wazee wa dar es salaam waliokuwa wanampigia makofi na kumshangilia Kiwete.
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli nilichosoma nikilinganisha na yale tunayosoma kwenye chama cha kijani.... naona ni sawa tu na mvinyo kwenye chupa tofauti... hakuna la zaidi wandugu... ila vyema tuishi kwa matumaini:)
   
 9. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Mnyika kapewa Uenyekiti wa vijana kinyemela, aibu kweli kweli CHADEMA. Mnashindwa hata kuendesha uchaguzi wa vijana?

  Hata tangazo lenu limekaa utafikiri limetolewa na CCM.

  Hongera Dr. Slaa na Zitto, nyie ndio wapinzani wa kweli, sio kama huyo mwenyekiti wenu.
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kazi nzuri Dr. Slaa Mungu Akubariki sana Amen
   
 11. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Bravo CHADEMA Tunawapat, aluta continua, mkoloni na afungashe, nusu karne ya mtosha teh teh...
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  muheza hao unaowapa hongera ni wana sisi m?
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Unawasifu wachezaji unamdharau kocha anayepanga formation ya 4-4-2 kazi kweli kweli
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Labda ni chuki dhidi ya wachagga,kuna watu wako radhi tubaki masikini milele kuliko viongozi wa makabila flani flani kutawala nchi,ni tatizo ambalo mwalimu hakulitatua kabla hajafa,ni ukabila "Uliobarikiwa" na "Kuhalalishwa"
   
 15. B

  Bull JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha mbumbumbu: M/kiti Mbowe Kafeli masomo O-Level

  Katibu: Mchungaji Slaa, kapata cheti kwa kusoma kitabu cha Nabii Paul, Mazumbukuku wanashabikia mpaka Minute za vikao, Chadema nikichekeshooooo !!!
   
 16. m

  magee Senior Member

  #16
  May 6, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wewe na CCM damdam.
  ................na ccm tuisemeje??ccm na mafisadi wao ama ccm na uislamu wao ama ccm na wizi wao????
   
 17. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Bull.

  Acc. to Thesaurus dictionary,

  1. An offensive term for talk or writting dismissed as foolish or in accurate.
  2. Male of cattle. An uncastrated adult male of any breed of domestic cattle or other bovine animal.
   
 18. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha !!! Je ni kipi chenye jipya?? Mbona kile cha kwenu Chama Cha Majambazi hamtoi taarifa kwa umma na kila kitu ni closed mpaka tufukue huko? Hongereni Chadema kwa kuongelea mambo muhimu ya mustakabali wa nchi yetu!!!! It is the oooonly political party which dares talking openly!!!! Vingine vinasubiri Chadema iibue mambo halafu ndipo navyo vinaangalia upepo na kuanza kubeza!!!!! Yaani mamluki ni hatari sana!!!
   
 19. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Dr Wilbrod Slaa,
  Wewe umetumwa????????????????

  Ni kweli umetumwa na nina amini kuwa umetumwa......kutokana na matendo yako..........
  na aliyekutuma nimeshamfahamu...
  sio mwingine ila MWENYENZI MUNGU Kuwa mtetezi wa wanyonge mbayuwayu wa Tanzania.
  :angry:
   
 20. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #20
  May 6, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Wewe ndio unaleta Uchaga hapa, wengine tunaongelea utendaji wa viongozi, wewe unaleta mambo ya Uchaga.

  Huyo Mwenyekiti wenu, angelikuwa kocha angeshafukuzwa siku nyingi.

  Tatizo lenu mnafikiri JF ndio inawakilisha Watanzania, ikija mwezi wa kumi kipigo, na mnaanza kulialia, kumbe tatizo lenu ni kocha mbovu.

  Uongozi gani wa kuahirisha uchaguzi wa vijana na kuweka vibaraka wa Mbowe kwenye madaraka?
   
Loading...