Taarifa kwa mkuu jeshi la polisi IGP na RPC Dodoma

Nyanje

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
1,860
Reaction score
2,386
Kamanda IGP kwa unyenyekevu naomba kutoa taarifa hii kwako kama raia mwema kwamba kuna askari tena ni kiongozi kalidhalilisha jeshi mchana kweupe. Sisi kama raia wema tulitoa taarifa ya wizi kituo cha polisi Mpwapwa kwani huyo mtuhumiwa ni mwizi mzoefu na ni mfanyakazi wa shirika la umeme.

Hapa tunamuona akifanya wizi kutumia gari la shirika, wiki mbili zilizopita tulimuona akiiba tairi mpya zaidi ya 20 na mapipa ya rami baada ya kumpa taarifa kaimu OCD alifika hapa Mtera na kufanikwa kukamata mali hizo nyumbani kwa mtuhumiwa japo muhusika alikuwa safarini walikamatwa vijakazi wake(kinyozi) na mke wake baadaye wakamwachia mwanamke.

Kilichotushanga huyo mtuhumiwa karudi hapa Mtera siku ya Jumatatu na kutangaza live kwamba kamlegeza tayari kaimu OCD na mpaka kiasi alichompa na kwamba hawezi kufika mahakamani.

Mpaka sasa yupo mbaya zaidi anawakashifu polisi wadogo wa kituo cha hapa Mtera kwakweli tumesikitishwa sana na tukio hili kesi kapewa kinyozi wake na ndiye aliyefikishwa mahakamani.

Sisi kama raia wema tunaomba ufanywe uchunguzi upya na tuko tayari kutoa ushirikiano.
 
Ahsante sana raia mwema.

Samahani kwa sasa tuko bize kuwashughulikia Ukawa na CDM. Tukimalizana nao tutakuja kukisikiliza kilio chenu wananchi.

Ahsante kwa utii wako wa sheria bila shuruti.

Ulinzi shirikishi, polisi jamii.
 
si vema kuharibu mada mkuu tutumie majukwaa haya kujenga sorry lakini.
 
Sawa kiongozi, ila hofu yangu hawa uliowaandikia sijui kama wanasoma humu. Na pia huenda wakapuuza.

Ndio jeshi letu hili.
 
Naona rangi ya kudhulumiana, pia naona rangi ya wivu ndani ya huu uzi.
 
Rushwa kubwa kwa viongozo ndani ya Jeshi la polisi sio kosa kwani wengi wao wamewahi au bado wanashiriki.
Umewahi kuhoji utajiri mkubwa walio nao baadhi ya viongozi ndani ya majeshi ikiwemo polisi wameupata wapi ilhali mishahara yao inajulikana.Mbona sheria ziko wazi lakini hazifuatwi?
Ukitaka uone polisi anafukuzwa jaribu kuangalia ana cheo gani?Ukiona cheo chake ni chini ya nyota moja basi ujue huyo atafukuzwa hata kwa kupoteza mia tano ya mtuhumiwa aliyoikabidhi kaunta. Mia tano haiwezi kuwa na mgao kwa Wakubwa wake hivyo hawezi kupata mtetezi.Hapo utaona vyombo vya habari vikiitwa na kupewa taarifa ya kufukuzwa kwa askari kwa kudhalilisha polisi.

Kwa kifupi jeshi la polisi ni kati ya taasisi zinazojitahidi kuchuja kahawa kwenye kikombe cha chai na kumeza majani ya mchaichai yakiwa mazima mazima.

Udhaifu mkubwa unatokana na ukweli kuwa viongozi wa serikali wako bize kutoa maagizo ya kuwashughulikia wapinzani wao wa kisiasa na vyama vya siasa vya upinzani tu.Na kiongozi safi wa dola ni yule anayeonekana kugandamiza demokrasia.

Yapo mengi sana yanayofanyika ya askari wa dogo kukamata wahalifu wa kubwa lakini maocd ,wakuu wa upelelezi na marpc wanamegewa migao minono ili wato maagizo ya kufuta kesi hizo zenye maslahi yatokanayo na rushwa.

Tegeta ESCROL iko kila Idara kwa namna yake.
CCM na serikali yake ndiye mama wa rushwa zote kubwa nchini.
 
Hapa JF siyo polisi,isitoshe Polisi si rahisi kushughulikia ripoti ya kwenye mitandao labda iwe inahusu Chadema au Ukawa ndiyo wanaweza kuishughulikia vinginevyo umeula wa chuya maana Polisi hawezi kumkamata Askari na Askari hawezi kumkamata Polisi.
 
kamanda IGP kwa unyenyekevu naomba kutoa taarifa hii kwako kama raia mwema kwamba kuna askari tena ni kiongozi kalidhalilisha jeshi mchana kweupe sisi kama raia wema tulitoa taarifa ya wizi kituo cha polisi mpwapwa kwani huyo mtuhumiwa ni mwizi mzoefu na ni mfanyakazi wa shirika la umeme hapa tunamuona akifanya wizi kutumia gari la shirika wiki mbili zilizopita tulimuona akiiba tairi mpya zaidi ya 20 na mapipa ya rami baada ya kumpa taarifa kaimu OCD alifika hapa mtera na kufanikwa kukama mali hizo nyumbani kwa mtuhumiwa japo muhusika alikuwa safarini walikamatwa vijakazi wake(kinyozi) na mke wake baadaye wakamwachia mwanamke kilichotushanga huyo mtuhumiwa karudi hapa mtera siku ya j3 na kutangaza live kwamba kamlegeza tayari kaimu OCD na mpaka kiasi alichompa na kwamba hawezi kufika mahakamani mpaka sasa yupo mbaya zaidi anawakashifu polisi wadogo wa kituo cha hapa mtera kwakweli tumesikitishwa sana na tukio hili kesi kapewa kinyozi wake na ndiye aliyefikishwa mahakaman sisi kama raia wema tunaomba ufanywe uchunguzi upya na tuko tayari kutoa ushirikiano.

Mkuu sasa hivi kila mmoja anakula kwa urefu Wa kamba yake! Kama Wewe kamba yako ni fupi wacha ufe njaa! Kama ungekuwa na uchungu ungekubali tuchezewe hivyo na hawa majizi ya escrow?
 
Naona rangi ya kudhulumiana, pia naona rangi ya wivu ndani ya huu uzi.
Kwanini umekimbilia kuattack personality na sio facts zilizotolewa? Hata kama kuna wivu kwa mfano, je hizo facts ni useless? Una taarifa kiasi gani mpaka kuconclude ni wivu?
 
kamanda IGP kwa unyenyekevu naomba kutoa taarifa hii kwako kama raia mwema kwamba kuna askari tena ni kiongozi kalidhalilisha jeshi mchana kweupe sisi kama raia wema tulitoa taarifa ya wizi kituo cha polisi mpwapwa kwani huyo mtuhumiwa ni mwizi mzoefu na ni mfanyakazi wa shirika la umeme hapa tunamuona akifanya wizi kutumia gari la shirika wiki mbili zilizopita tulimuona akiiba tairi mpya zaidi ya 20 na mapipa ya rami baada ya kumpa taarifa kaimu OCD alifika hapa mtera na kufanikwa kukama mali hizo nyumbani kwa mtuhumiwa japo muhusika alikuwa safarini walikamatwa vijakazi wake(kinyozi) na mke wake baadaye wakamwachia mwanamke kilichotushanga huyo mtuhumiwa karudi hapa mtera siku ya j3 na kutangaza live kwamba kamlegeza tayari kaimu OCD na mpaka kiasi alichompa na kwamba hawezi kufika mahakamani mpaka sasa yupo mbaya zaidi anawakashifu polisi wadogo wa kituo cha hapa mtera kwakweli tumesikitishwa sana na tukio hili kesi kapewa kinyozi wake na ndiye aliyefikishwa mahakaman sisi kama raia wema tunaomba ufanywe uchunguzi upya na tuko tayari kutoa ushirikiano.

Hivi wewe nchi hii gerez na mahakama yapo kwa vibaka na maskini lakini kwa watu wa kati na kwenda juu vitu hivyo haviwahusu.Angalia hata picha hii,aliyeibiwa na msimamizi wa Serikali yetu tukufu,na pia walioapa kwa katiba hii anakweda mahakamani kuomba Bunge lizuiwe kujadili mambo ya Tegeta ESCROW.Maana yake nini? Ikulu na viongozi wote wa juu wanahusika na wizi huo.Mbunge Kafulila hana polisi wala Usalama wa Taifa anajua mambo haya,mkuu wa nchi,Waziri mkuu na mawaziri vyombo vyote mnavyo hamjafanya lolote.Mbwembwe zote za Uwanja wa Uhuru ni MAVI MATUPU.Kuanzia leo sitoi mchango wa maabara na wala sichangii mwenge.
 
Kwanini umekimbilia kuattack personality na sio facts zilizotolewa? Hata kama kuna wivu kwa mfano, je hizo facts ni useless? Una taarifa kiasi gani mpaka kuconclude ni wivu?

Mkuu nafurahi sana watu wa aina yako haya majukwaa yakitumika hv heshima itakuwepo wajua muda mwingi watu wametanguliza siasa mbele badala ya kuangalia mambo ya msingi nilichomaanisha mimi ni kwamba kama maswala haya yataachwa kwenye jeshi la polisi itakuwa ni tabia kwani watu wataona tukitoa taarifa polisi tunakuwa tumewapa dili baadhi ya viongozi kwahiyo bora kuchukua hatua mkononi na zaidi mimi naamini si polisi wote wanafanya haya mambo kwani kuna askari tunaona wakifanya kazi zao vema tu mpaka mtu anastaafu anaendelea kuheshimiwa na jamii wapo na tunawajua.
 
Wakuu mimi nadhani mleta uzi ameandika hilo, najua wengine wanaweza kulidaka na kuwa deal kwao wakimhoji ocd kisha mhusika na kuvuta hela nao pia. Yale yale ya kasusura. But all in all ni vema kumsaidia mleta uzi maana ni kweli hata kama wamezulumiana, lakini taarifa hizo ni nyeti na muhimu kufanyia kazi.
Rushwa kubwa kwa viongozo ndani ya Jeshi la polisi sio kosa kwani wengi wao wamewahi au bado wanashiriki.
Umewahi kuhoji utajiri mkubwa walio nao baadhi ya viongozi ndani ya majeshi ikiwemo polisi wameupata wapi ilhali mishahara yao inajulikana.Mbona sheria ziko wazi lakini hazifuatwi?
Ukitaka uone polisi anafukuzwa jaribu kuangalia ana cheo gani?Ukiona cheo chake ni chini ya nyota moja basi ujue huyo atafukuzwa hata kwa kupoteza mia tano ya mtuhumiwa aliyoikabidhi kaunta. Mia tano haiwezi kuwa na mgao kwa Wakubwa wake hivyo hawezi kupata mtetezi.Hapo utaona vyombo vya habari vikiitwa na kupewa taarifa ya kufukuzwa kwa askari kwa kudhalilisha polisi.

Kwa kifupi jeshi la polisi ni kati ya taasisi zinazojitahidi kuchuja kahawa kwenye kikombe cha chai na kumeza majani ya mchaichai yakiwa mazima mazima.

Udhaifu mkubwa unatokana na ukweli kuwa viongozi wa serikali wako bize kutoa maagizo ya kuwashughulikia wapinzani wao wa kisiasa na vyama vya siasa vya upinzani tu.Na kiongozi safi wa dola ni yule anayeonekana kugandamiza demokrasia.

Yapo mengi sana yanayofanyika ya askari wa dogo kukamata wahalifu wa kubwa lakini maocd ,wakuu wa upelelezi na marpc wanamegewa migao minono ili wato maagizo ya kufuta kesi hizo zenye maslahi yatokanayo na rushwa.

Tegeta ESCROL iko kila Idara kwa namna yake.
CCM na serikali yake ndiye mama wa rushwa zote kubwa nchini.
 
ushiboy kwahiyo hawa escrow kuna wivu name kudhulimiana?
vivian do you really know wapi wizi wa escrow ulipoa anzia?
So, unataka kuniaminisha kwamba wizi wa matairi 20 na wizi wa kulifisi Taifa unafanana?
 
Last edited by a moderator:
Naona rangi ya kudhulumiana, pia naona rangi ya wivu ndani ya huu uzi.

Ni vema kusoma kwa makini kilichoandikwa kuliko kukimbilia kucoment uchulo wako watu sielewewi hivyo vichwa vyenu vina kazi ya kutunza kamasi tu.
 
Sawa kiongozi, ila hofu yangu hawa uliowaandikia sijui kama wanasoma humu. Na pia huenda wakapuuza.

Ndio jeshi letu hili.

Kama umeweza kusoma wewe kwanini ashindwe waziri wa mambo ya ndani ya nchi,IGP,kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma si itakuwa maajabu na zaidi katiba ya nchi ina ibara inayosema katika kutoa taarifa hakuna mipaka.
 
vivian do you really know wapi wizi wa escrow ulipoa anzia?
So, unataka kuniaminisha kwamba wizi wa matairi 20 na wizi wa kulifisi Taifa unafanana?

wizi ni wizi.
 
Last edited by a moderator:
Ahsante sana raia mwema.

Samahani kwa sasa tuko bize kuwashughulikia Ukawa na CDM. Tukimalizana nao tutakuja kukisikiliza kilio chenu wananchi.

Ahsante kwa utii wako wa sheria bila shuruti.

Ulinzi shirikishi, polisi jamii.

Halafu amesahau waziri wao aliwahi kusema mishahara ya polisi ni midogo sana hivyo wanastahili kupewa rushwa.
 
Kwanini umekimbilia kuattack personality na sio facts zilizotolewa? Hata kama kuna wivu kwa mfano, je hizo facts ni useless? Una taarifa kiasi gani mpaka kuconclude ni wivu?

Mkuu, it's not personal attack.
Huo ni mtazamo tu, as you know here we dire talk openly.
ukiangalia zaidi ya mletauzi alichoandika lazima upate kujiuliza maswali kadhaa
1. Kwanini tukio la wizi wa matairi 20 aripoti kwa mkuu wa jeshi?
2. Kwanini aonyeshe kuumizwa na kitendo cha kukamatwa kijana anaeamini kwamba hausiki?
3. Kwani hakuna matukio mengine makubwa ya wizi zaidi ya hayo matairi 20?
Kwakifupi maswali ni mengi kuliko majibu
 
Well, ungeweka sababu hizi katika post yako ya mwanzo hakafu ndo ukahatimisha kuwa unadhani ni wivu, pengine nisingeshangaa. Hata hivyo, sababu kama kuumizwa na kukamatwa kwa kijana asiyehusika nadhani ni sahihi kabisa (kama kweli kijana hahusiki). Sio jambo jema kupaza sauti ukiona mtu asiye na hatia anaonewa? Tunasikia sauti za watu wengi kuhusiana na wanyonge kubambikiziwa kesi polisi, je sio sahihi kupinga ufedhuli huu?
 
Back
Top Bottom