Suala la kufuta majina
yote na kuanza usaili upya sio tatizo ila kumbuka serikali huwa inaenda
kwa utaratibu..mfano mchakato mzima wa usaili ulikuwa umeshatengewa
fungu kwa ajili ya zoez zima.ukumbi wa kule baraza la maaskofu ulikuwa
unalipiwa kwa siku plus watu wote wa kamati walikuwa wakilipwa posho kwa
uendeshaji wa mchakato..sasa ukisema tufute ina mana tuanze upya tena
watu wafanye usaili upya,twende posta tukachukue barua kwa magar na
uchambuz mpya(use of money resource).then tu shortlist na kuanza usaili
upya hapo unazungumzia january sasa..then kumbuka kati ya watu 200 sio
wote walipendelewa wapo waliokuwa na sifa zote na walifaulu usaili kwa
haki ila wapo wachache ambao ndio washukiwa.je hatima ya wale ambao
hawausiki na mfano ingekuwa ni wewe ndo ulipita kwa haki ungependa jina
lako likatwe sababu ya wengine..ndio mana katibu ametoa taarifa kuwa
amesitisha na sio kufuta ili kupisha uchunguzi wa hizo tuhuma zilizofika
mezani kwake..kwaiyo sio rahis kusema zifutwe bila ushahid wowote
angefanya hivyo angekuwa yupo kinyume na taratibu za kazi.
safi sana mahasimu ya dr.chami yasikusumbue timiza wajibu.