karibukwetusingida
JF-Expert Member
- Mar 10, 2014
- 290
- 138
Baadhi ya vyombo vya habari leotarehe 29 julai, 2014 vimeandikakwa makosa kuwa ajira za uhamiajizilizositishwa jana zinahusiana na70 zilizopatikana baada ya usailiuliofanyika katika uwanja wa taifa.
Ukweli ni kuwa usaili wa nafasi ya mkaguzi msaidizi wa uhamiaji ambao awali ulianzia uwanja wa taifa ulienda vizuri hadi wakapatikana wasailiwa wa kujaza nafasi 70 za mkaguzi msaidizi wa uhamiaji.
Zoezi hilo halikuwa na matatizo yoyote, na waliochaguliwa walitakiwa kuripoti kazini tarehe 29 julai lakini kwa sababu ya sikukuu sasa wataripoti baada ya sikukuu.
Hivyo tunapenda kufafanua kuwa wasailiwa waliochaguliwa kujaz anafasi 70 za mkaguzi msaidizi wa uhamiaji hawahusiki na usitishwaji uliotangazwa jana na wanatakiwa kuendelea na mipango ya kuripoti kazini kama ilivyotangazwa hapo awali.
Wasailiwa wanaohusika nakusitishwa kwa ajira zao ni wale waliokuwa wameshiriki katika zoezi la kuajiri konstebo na koplo wa uhamiaji ambao idadi yao ni 200,ambao walitakiwa kuripoti tarehe 06 agosti, 2014 lakini kwa sasa hawa ndio wanaelekezwa wasubiri hadi hapo watakapopewa maelekezo mengine.
Sgnisaac J. Nantanga
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi, 29 Julai, 2014