Taarifa kutoka mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya

Jemmie

JF-Expert Member
Mar 6, 2018
216
285
1132875
 
Waache kujitetea wakati watu wanasema yaliyo ya kweli. Hakuna cha kukusanya maoni wala nini, tunajua ndio tayari mliishapitisha hayo mabadiliko maana tukiwa kama wananchi tumeyashuhudia baada ya kwenda kutibiwa tukiwa na kadi zetu.
Kuna baadhi ya huduma mnadai mfuko unachangia 75% na mgonjwa anachangia 25% haya mambo hatukuyazoea.
Kuna baadhi ya dawa ukiandikiwa, zikijazwa kwenye mfumo inaonesha hazijasajiliwa wakati mwanzo zilikiwepo.
Kuna baadhi ya dawa mnadai mpaka akaandike specialist huku wanajua kabisa wako wachache, na hata ukimpata ni mpaka awe katika kituo cha hadhi yake, vinginevyo hatambuliki kama ni physician. Yaani kero kero tu ilimradi watu tukose huduma.
 
Mambo yameharibika.
Magofool hawatakii mema watanzania.
Praise team nimewakaribisha mwenyeewe!!!
 
Naona wameshindwa kukanusha kuwa si habari za kweli ila wamesema sii habari rasmi hivyo zinaweza zikawa za uongo ama za kweli
 
duh kweli kuongoza nchi sio kama kuongoza wizara, jamaa amefeli mno.
 
Kuna baadhi ya huduma mnadai mfuko unachangia 75% na mgonjwa anachangia 25% haya mambo hatukuyazoea.
Kuna baadhi ya dawa ukiandikiwa, zikijazwa kwenye mfumo inaonesha hazijasajiliwa wakati mwanzo zilikiwepo.

Matumizi yao makubwa ya fedha inayotokana na michango ya wanachama yapo kwenye management badala ya huduma kwa wanachama wanyonge
 
Matumizi yao makubwa ya fedha inayotokana na michango ya wanachama yapo kwenye management badala ya huduma kwa wanachama wanyonge
Na ndio hapo wanapofeli.

Hospitali zenyewe zinalalamika kuwa zinaweza kutuma madai ya 100mil, mwisho wa siku wakalipwa 50mil, okey hata kama wamegundua shida iko kwa hospitali husika, hizo pesa huwa wanapeleka wapi badala ya kuboreshea huduma.
Hii NHIF shida tupu.
 
Nimepoteza kadi nataka niipate chap chap je makao makuu ni wapi ili niende muda huu.
Nipo Dar es Salaam
 
Lisemwalo lipo, kama halipo lipo njiani linakuja! Kwani uhuni wa NHIF unaanza leo!
Na limeshafika! Juzi nimekwenda hospitali nikaambiwa hiyo namba yako haipo. Nilibaki nashangaa. Kwa vile ilikuwa Jumamosi niligugumia na maradhi yangu hadi Jumatatu nilipopeleka taarifa. Niliumia sana.
 
Na ndio hapo wanapofeli.

Hospitali zenyewe zinalalamika kuwa zinaweza kutuma madai ya 100mil, mwisho wa siku wakalipwa 50mil, okey hata kama wamegundua shida iko kwa hospitali husika, hizo pesa huwa wanapeleka wapi badala ya kuboreshea huduma.
Hii NHIF shida tupu.
NHIF ni moja ya unyonyaji kwa watumishi. Kiwango cha 5% kinachokatwa ni kikubwa. Usemalo ni kweli, kituo kinaweza kudai 20m kikaishia kulipwa 12m. Na huwa hawatoi taarifa kunapokuwa na mabadiliko aidha ya bei za dawa au vipimo.

Matokeo yake kituo kinapodai kinakatwa kwa maelezo kwamba bei zilizoandikwa sio sahihi.

Waendelee kuwakomesha watumishi wakati wao wakijilipa posho kibao.
 
Back
Top Bottom