Taarifa kumuhusu VITA RASHID KAWAWA

Mkurabitambo

JF-Expert Member
Feb 3, 2010
230
57
Juzi wakati wa kuchangia hoja ya bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13,Vita Kawawa alisimama na kujaribu kueleza kuhusu deni la taifa.Kiukweli ninachoweza sema alijitahidi kutuhadaa watanzania kwa mahesabu yake yasiyo na tija.
Vita alisikika akisema kila mtanzania anadaiwa tSH 440000 Ambayo ukiigawa kwa idadi ya siku na kwa riba ya mkopo inaonyesha kila mTanzania anahitajika kulipa shilling 17 kila siku kulipia deni la Taifa.

Turudi katika hoja ya mch Msigwa mbuge wa Iringa,yeye alisema kwamba kulingana na takwimu zilizopo asilimia 50 ya watanzania ni watoto,na wengine 25-30 ni wazee,hivyo kuifanya Tanzania kuwa na wazalishaji wachache zaidi ya walaji.

Hoja yangu ni juu ya Vita Kawawa kudai eti deni hili linabebeka, atuambie linabebekaje? chukulia mfano wa Mtanzania wa kawaida mwenye familia ya watoto watano, na ndugu wamtegemeao 3 hivyo kufanya ratio kati ya mzalishaji na walaji kuwa 1:8.Hivyo deni la watu nane linahudumiwa na mtu mmoja.

Tunaposema deni la taifa limepanda bwana Vita ujue kwamba tunaolihudumia linatuumiza,usijifananishe eti Tanzania na Japan wapi na wapi bwana..Tunatarajia wawakilishi wetu Bungeni mtumie ubongo kufikiri na sio masaburi

TAIFA LINAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA NA UDHAIFU WENU VIONGOZI NA USHABIKI WAO WA KISIASA
 
Mimi nina mtoto wangu ana mwaka mmoja na miezi 8 tayari anadaiwa hata kabla hajajitambua masikini my country deni kubwa afu umasikini wa tatu kutoka mwisho duniani
 
mtoto wangu wa mwisho ana miezi mitano, hata nusu mwaka hajafika, lakini tayari anadaiwa...deni walilokopa viongozi waliopita liliiishia kwenye mifuko ya wadhalimu, wakajenga majumba na mahotel, sasa sisi tunawalipia...watoto wao wanafaidi jacho letu.....
 
Napita tu. Hawa ndo watoto wa vigogo kama akina le mutus ambao huwa hawafikiri beyond their nose!!! Le mutus alitoa mpya facebook kwa kumkandia Mh. Mnyika kwa kutumia neno udhaifu. Yale mawe aliyoporomoshewa kule FB hatasahau, kila rafiki yake amempa ukweli!!!!!!
 
Jamani vita anategemea kevu,pale bungeni na uwakilishi wa wananchi.ACHA atumie Masaburi.
 
Hawa watoto wa viongozi tuliokuwa tunawaheshimu sana kwa utendaji wao, wamekuwa kama magubegube vile, siasa za uongo, siasa za maji taka, wamekuwa DHAIFU sana, Sijui wamepatwa na pepo gani
 
Kwa mawazo yangu kukopa si hoja kila mtu hukopa lakini mbona Magamba hawatuambii tunakopa kufanyia nini wakati ujenzi wa barabara mashule, Vyuo dawa hospitali etc bado shida???
 
Mie napita tu jamani. Kumbe Vitta Kawaw bado ni mbunge? ndo mara ya kwanza nini kuongea bungeni toka aingie bungeni baada ya kumwangusha mzee Pius Mbawala.

  • :smow:


  • :mad:
 
Juzi wakati wa kuchangia hoja
ya bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13,Vita Kawawa alisimama na
kujaribu kueleza kuhusu deni la taifa.Kiukweli ninachoweza sema
alijitahidi kutuhadaa watanzania kwa mahesabu yake yasiyo na tija.
Vita alisikika akisema kila mtanzania anadaiwa tSH 440000 Ambayo
ukiigawa kwa idadi ya siku na kwa riba ya mkopo inaonyesha kila
mTanzania anahitajika kulipa shilling 17 kila siku kulipia deni la
Taifa.

Turudi katika hoja ya mch Msigwa mbuge wa Iringa,yeye
alisema kwamba kulingana na takwimu zilizopo asilimia 50 ya watanzania
ni watoto,na wengine 25-30 ni wazee,hivyo kuifanya Tanzania kuwa na
wazalishaji wachache zaidi ya walaji.

Hoja yangu ni juu ya Vita Kawawa kudai eti deni hili
linabebeka, atuambie linabebekaje? chukulia mfano wa Mtanzania wa
kawaida mwenye familia ya watoto watano, na ndugu wamtegemeao 3 hivyo
kufanya ratio kati ya mzalishaji na walaji kuwa 1:8.Hivyo deni la watu
nane linahudumiwa na mtu mmoja.

Tunaposema deni la taifa limepanda bwana Vita ujue kwamba
tunaolihudumia linatuumiza,usijifananishe eti Tanzania na Japan wapi na
wapi bwana..Tunatarajia wawakilishi wetu Bungeni mtumie ubongo kufikiri
na sio masaburi

TAIFA LINAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA NA UDHAIFU WENU
VIONGOZI NA USHABIKI WAO WA KISIASA

vita kawawa na ngeleja wanawahadaa watz juu ya deni la taifa.
 
Huyu anayesema kuwa deni linabebeka anapaswa kupimwa, deni linazidi budget ya serikali ya mwaka kwa trilioni tano yaani deni ni trilion 20 wakati budget ni trilion 15 hafu aseme linabebeka? Hii nchi bwana!!!!!
 
hao magamba si huwa wanaongea bila data surely hata mimi hicho kitu kiliniudhi sana kuchukulia hilo suala kishemeji wakati ni mzigo mkubwa sana
 
Hawa wanasiasa ni wanafiki na wazandiki walitakiwa watuambie hizo trilioni 22 zimetumikaje badala yake wanaleta siasa kwenye suala nyeti kama hili eti deni linabebeka.
 
Back
Top Bottom