Taarifa fupi kutoka Serikali ya Wanafunzi

Taarifa fupi kutoka Serikali ya Wanafunzi

Kahumbi Lumola

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2012
Posts
359
Reaction score
2,569
Mimi naitwa Lumola Steven Kahumbi ni Waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi DIT, juzi tarehe 14/08/2014 saa 2 usiku, mimi pamoja na Mh. Mwenyekiti halali wa TAHLISO MUSA MDEDE, Rais wa DITSO, Spika wa bunge IFM, Mweka HAZINA WA TAHLISO, Spika wa bunge DITSO pamoja na Waziri wa fedha IFM tulikamatwa na watu waliojitambulisha kuwa wao ni polisi tukiwa tunakula chakula kisha walitufunga pingu wakatupeleka kituo cha polisi Osterbay ambapo walituchukua maelezo mpaka saa 8 asubuhi baada ya maelezo walituweka mahabusu kwa tuhuma ya uchochezi.

Asubuhi walitutawanya katika vituo tofauti tofauti vya polisi na ilipofika mchana waliturudisha osterbay ambapo tuliongea na RPC kinondoni na baadae alikuja afisa kutoka kanda maalumu ya Dar es salaam. mpaka hivi sasa sisi sote tumeachiwa kwa dhamana. Mapema katika wiki zilizopita tulitoa tamko la kuipa serikali kuu siku 7 wawe wametimiza malipo ya fedha kwa ajili ya field ambayo wameyachelewesha kwa wiki 5 lakini siku 7 zilikwisha na serikali haikutimiza agizo letu kwao, tukakutana tena na vyombo vya habari tarehe 13/08/2014 ambapo tulitangaza maandamano nchi nzima kwa ajili ya kuishinikiza serikali kulipa fedha hizo Kwa ufupi hiyo ndio ilikuwa sababu ya sisi kukamatwa.

Katika HIstoria ya nchi yetu tangu tulipozaliwa kama Taifa huru haijawahi kutokea Uzembe na Makusudi kama haya kwa serikali kuchelewesha fedha za field kwa wiki saba. Ni tukio jipya kabisa ambalo kwa kila anayejua umuhimu wa field kwa wasomi lazima ataishangaa serikali yetu kwamba Inafikiria nini. Walituhoji sana kuhusu kibali lakini tulichowajibu, tuliwaambia hayo yanayoitwa maandamano bado hayajafanyika kwahiyo hatuwezi kuhoji juu ya uhalali au uharamu wake.
 
Mbona kuna kanusho kwamba huyo Mdede si Rais wa Tahliso? Ingia hapa. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/707961-tahliso-watoa-tamko-kali-yasema-mdede-anatumika-new-post.html
 
Poleni sana wakuu,mwenyekiti wa bunge la katiba na mbunge wa urambo na aliyekuwa spika wa bunge la JMT na waziri wa africa mashariki bwana samwel john sitta kaidhinisha malipo ya vipaza sauti vya kukodi kwa siku 8.5m kutoka ukumbi wa mikutano wa ACC jijini arusha wakati nyie mna week saba mnahitaji pesa kiasi tu kwa ajiri ya FIELD na matokeo yake mmekamatwa na kuwekwa ndani kwa kudai haki ya kikatiba na kimsingi kabisa?

Nimemtaji bwana samweli kwa sababu na yeye kishawahi kuongoza maandamo ya wanafunzi wa chuo kikuu na badae kuitwa na mwalimu kwenda kusikilizwa na matokeo yake akalabwa bakora za kutosha na mwalimu ila nyie mmelala sero,sasa mkikutana na vyombo vya habari mtatoa tamko gani tena kwa mara nyingine litakalofanya serikali sikivu iwasikilize? Kama la awali limewapeleka sero?
 
Sisi wanafunzi bhana tuna matatizo sn!
Linapokuja suala la shekeli tupo juu na ikitokea serikali kufanya uzembe huwa tunataka nchi nzima wajue, waone, waamini kuwa serikali imetukosea sn!
LAKINI kwenye mambo ya kitaifa na yanayowagusa wananchi, HAYATUHUSU KAMWE!
Mfn. Mbolea, katiba, rasilimali, madini nk.
 
Poleni sana wakuu,mwenyekiti wa bunge la katiba na mbunge wa urambo na aliyekuwa spika wa bunge la JMT na waziri wa africa mashariki bwana samwel john sitta kaidhinisha malipo ya vipaza sauti vya kukodi kwa siku 8.5m kutoka ukumbi wa mikutano wa ACC jijini arusha wakati nyie mna week saba mnahitaji pesa kiasi tu kwa ajiri ya FIELD na matokeo yake mmekamatwa na kuwekwa ndani kwa kudai haki ya kikatiba na kimsingi kabisa?

Nimemtaji bwana samweli kwa sababu na yeye kishawahi kuongoza maandamo ya wanafunzi wa chuo kikuu na badae kuitwa na mwalimu kwenda kusikilizwa na matokeo yake akalabwa bakora za kutosha na mwalimu ila nyie mmelala sero,sasa mkikutana na vyombo vya habari mtatoa tamko gani tena kwa mara nyingine litakalofanya serikali sikivu iwasikilize? Kama la awali limewapeleka sero?

Nmecheka sana mchabgo wako huu!
 
Pole sana mkuu ila kwa kifupi wanavyuo mnatuchanganya,wengi wenu mnaipenda serikali iliyopo madarakani na chama tawala lakini mkitendwa mnakuja kulalama huku,Sasa nyie mkipewa hizo fedha tutapata wapi hela ya mbio za mwenge?mi nadhani mvumilie mwende field kwa kujifunga mkanda naombeni muwe
na uzalendo kama cc wafanyakazi tunavyokatwa kodi kwenye mshahara ambao ukiuliza mchanganuo ukilinganisha na maisha kupanda hupewi majibu ila unatishiwa kufukuzwa kazi.Nawaombeni mjikaze kisabuni hayo ni mazoezi ya kujiandaa kuja uraiani ambako pia hakuna haki.
 
Kama tulivyofanya na Mtatiro miaka Ile kazeni kulala sero au segerea sio issue.mtawini tu.
 
Poleni sana wasomi wetu! Pesa zote zimepelekwa BMK kulipa vipaza sauti na maposho poshooooo!! Umeelewa!
 
Sie kaka zenu tuliandamana kudai demokrasia miaka ya 80's na 90's, naona hawa watoto wanaadamana kudai posho, tumekwisha. Vijana wa siku hizi bure kabisa!
 
Huu ndio upuuzi mwingine, baada ya kuwatia nguvuni watu wanaodai haki ya kwa tuhuma et wanataka kuandamana bila kibali sasa mbona hawakutoa majibu lini hao wanafunzi watapatiwa hela zao??? Je haikuwa haki yao kudai hiyo hela??? Kama kuna tatizo lilitokea majibu yake yako wapi?? Je maandamano siyo haki ya kila mtanzania kikatiba??
Alaaaah huu ndio upuuzi mwingine sasa
 
Amakando ufafanuzi wa kina kuhusu MUSA MDEDE na uenyekiti wa TAHLISO utatolewa siku za usoni.
 
Mimi naitwa Lumola Steven Kahumbi ni Waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi DIT, juzi tarehe 14/08/2014 saa 2 usiku, mimi pamoja na Mh. Mwenyekiti halali wa TAHLISO MUSA MDEDE, Rais wa DITSO, Spika wa bunge IFM, Mweka HAZINA WA TAHLISO, Spika wa bunge DITSO pamoja na Waziri wa fedha IFM tulikamatwa na watu waliojitambulisha kuwa wao ni polisi tukiwa tunakula chakula kisha walitufunga pingu wakatupeleka kituo cha polisi Osterbay ambapo walituchukua maelezo mpaka saa 8 asubuhi baada ya maelezo walituweka mahabusu kwa tuhuma ya uchochezi.

Asubuhi walitutawanya katika vituo tofauti tofauti vya polisi na ilipofika mchana waliturudisha osterbay ambapo tuliongea na RPC kinondoni na baadae alikuja afisa kutoka kanda maalumu ya Dar es salaam. mpaka hivi sasa sisi sote tumeachiwa kwa dhamana. Mapema katika wiki zilizopita tulitoa tamko la kuipa serikali kuu siku 7 wawe wametimiza malipo ya fedha kwa ajili ya field ambayo wameyachelewesha kwa wiki 5 lakini siku 7 zilikwisha na serikali haikutimiza agizo letu kwao, tukakutana tena na vyombo vya habari tarehe 13/08/2014 ambapo tulitangaza maandamano nchi nzima kwa ajili ya kuishinikiza serikali kulipa fedha hizo Kwa ufupi hiyo ndio ilikuwa sababu ya sisi kukamatwa.

Kkatika HIstoria ya nchi yetu tangu tulipozaliwa kama Taifa huru haijawahi kutokea Uzembe na Makusudi kama haya kwa serikali kuchelewesha fedha za field kwa wiki 7. Ni tukio jipya kabisa ambalo kwa kila anayejua umuhimu wa field kwa wasomi lazima ataishangaa serikali yetu kwamba Inafikiria nini. Walituhoji sana kuhusu kibali lakini tulichowajibu, tuliwaambia hayo yanayoitwa maandamano bado hayajafanyika kwahiyo hatuwezi kuhoji juu ya uhalali au uharamu wake.

Ivi mimi najiulizaga hizi pesa (laki tatu kwa kila mjumbe na 8.9 mil za kukodisha maiki kwa siku) za katiba mpya ambayo mpaka sasa haina dalili za kupatikana kwanini wasingepewa hawa wanafunzi? na kwanini kama kweli nchi haina pesa why pesa za bunge la katiba hawacheleweshewi? sio siri hii nchi inatia hasira sana!!
 
Kwa hii ipo hivi je vyuo vikifunguliwa si itakuwa balaa...bila pesa ya kujikimu maisha ni magumu kwa kweli chuo.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu TAHLISO linatoa taarifa ya kukanusha habari zilizo samba kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii juu ya maandamano ya amani ya wanafunzi kesho ijumaa kuelekea ofisi za Wazir Mkuu kushinikiza Serikali kutoa shilingi bilioni 6.6 kwa ajili ya mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

TAHLISO kama shirikisho lina kanusha taarifa hiyo,na kulaani vikali matumizi mabaya ya kutumia jina la shirikisho kwa manufaa binafsi,aidha anaejiita mwenyekiti wa Tahliso katika taarifa hiyo Musa Mdede si MWENYEKITI HALALI kwa sababu vikao halali vya vya shirikisho vilivyofanyika tarehe 03 hadi 04 /05/2014 katika Chuo cha Kodi vilimwondoa madarakani,na kwa mujibu wa katiba ya shirikisho nafasi yake ilikaimiwa na makamu mwenyekiti wa Tahliso,hivo taarifa aliyoitoa sio sahihi ni ya upotoshaji kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania.

Aidha,uongozi wa Tahliso ulipata taarifa za ucheleweshaji wa malipo ya fedha za mafunzo ya vitendo kwa baadhi ya vyuo na kuweza kulifatilia swala hilo ili kuhakikisha fedha hizo zinapatikana kwa wakati,katika majukumu yake uongozi uliwasiliana na Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania - HESLB ili kupata hatima ya malipo kwa vyuo ambavyo havijapata fedha hizo,hususani Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino (saut) Mwanza na Tabora,Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji-Mbeya,Chuo kikuu cha Tumain Makumira-Iringa, Chuo kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stephano Moshi (SMUCCO) na Chuo Kikuu cha Jordan Morogoro.

Hata hivyo Bodi ya Mikopo imeendelea kuchukua hatua za haraka katika kuhakikisha vyuo husika vinapata fedha hizo haraka iwezekanavyo nakuweza kuzitoa kwa wanafunzi ambao wanaendelea na mafunzo yao ya vitendo katika maeneo mbalimbali,na leo hii Chuo kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stephano Moshi (SMUCCO) na Chuo Kikuu cha Jordan Morogoro vitapatiwa fedha zote zinazohitajika,taratibu za kifedha zinaendelea kufanyika ili vyuo vilivyobakia viweze kupata fedha hizo kwa siku ya kesho.

Uongozi wa Tahliso unawaomba wanafunzi wote wav you vikuu ambao hawajapata fedha hizo kuwa watulivu wakati wakisubili kupata fedha zao,na hatua kadha wa kadha zinaendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha wanafunzi wote stahiki wanapatiwa fedha zao kwa wakati.

Imetolewana :
ABDI MAHMOUD ABDI
MAKAMU MWENYEKITI TAHLISO.
14/08/2014

............................
 
sasa mimi ninamuuliza swali huyo Makamu mwenyekiti wa TAHLISO. kwa kuwa kwa mujibu wake anadai kwamba Musa Mdede sio Mwenyekiti halali baada ya kuvuliwa na kikatiba kwa sasa yeye ndio mwenyekiti halali swali upi msimamo wake juu wanafunzi ambao wapo field wiki ya saba na hawajalipwa pesa ya field na mbali na kuwa na msimamo yeye kwa kutambua kuwa ndio mwenyekiti ni lini amefuatilia juu ya suala hilo la wanafunzi kupewa pesa na alipewa majibu gani na ni lini alitoa mrejesho kwa wanafunzi juu ya kazi anazowafanyia kwa ujumla maana taarifa yake inaonyesha yeye ni mwenyekit tangu mwezi wa tano.
 
Back
Top Bottom