Taarifa Fupi kuhusu Kazi za Maendeleo Jimboni Ubungo (AMUA)

Wenzio wa Bonyokwa hawataki hata kukuona. Kiswigo humu kalalamika mpaka kakaukiwa na sauti. Mbunge wewe siyo msikivu.
 
Hoja yako nzuri ila wapo watu wanakusifia kwa kukutia ujinga. ukweli ni kwamba tatizo la maji nisugu na limatukela wengi fanya kazi shungulikia maji, pia huja fanya chochote kuhusu ajira. timiza ahadi wananchi tunataka kuona utekelezaji wa AMUA sio watusi kwa kikwete.
 
Daima amekuwa mtu wa maneno mengi na sio vitendo! Azipokee changamoto na kuzifanyia kazi 2015 sio mbali.
 
Unataka achimbe mitaro na kuweka mabomba mapya. Kazi yake ni kushinikiza serikali na anafanya hivyo, wacha uchawi.
 
Wenzio wa Bonyokwa hawataki hata kukuona. Kiswigo humu kalalamika mpaka kakaukiwa na sauti. Mbunge wewe siyo msikivu.

Wewe unajua kazi ya Mbunge? Laumu serekali na Ccm kwa kukaa madarakani miaka 50 hukuwatu wana shea maji na wanyama
 

hongera mkuu kwa juhudi zako kutatua kero jimboni kwako. napenda kukumbusha shida kubwa ya maji inayowakabili wakazi wa mbezi mjimpya, mshikamano na makabe. mheshimiwa hali ni mbaya sana gharama ya maisha iko juu sana sababu ya shida kubwa ya maji. wakazi wa maeneo tajwa hawajui sababu inayosababisha maji yasisambazwe kwa wakazi wa maeneo haya. watu wanaishi kwa maji ya kununua mwaka mzima nayo upatikanaji wake umekuwa wa shida siku hizi hivyo kusababisha bei yake kupanda. kuna mchezo mchafu unafanywa na dawasa wa kufunga bomba kubwa lililopo mbezi mwisho na kulifungua wanapojisikia hivyo kuleta mateso makubwa kwa wakazi wa mbezi. pigania viosk vya maji vilivyopo mbezi mwisho, stop over na kwa yusufu vifungwe na badala yake mabomba yasambazwe kwenda majumbani kwa watu. huu mradi wa uuzaji maji kati ya dawasa na waliomilikishwa mabomba haya ni janga kwa wakazi wa mbezi. fanyia kazi mheshimiwa!
 
kila ninapokusikia bungeni, naamini kwamba Tanzania siyo kama inavyoonekana, kuna "vichwa" sema nafasi ya kutosha haijapatikana. Tuombe mungu moto mliouanzisha, utufikishe tunakotamani!

Mimi binafsi nakuombea makubwa zaidi ya Ubunge, ikiwezekana Uwaziri Mkuu, na hata "URAIS" maana bado 'unadai'

natamani ungekuwa mbunge wangu.

Mi ni Mwananchi wa Monduli
 

Na huku Jang'ombe je, ni vizuri nao wakina Mariam Msabaha na Raya Ibrahim nao wakatupa taarifa zao.

Asha
 

Wabunge wote waungane, moto uliowashwa uendelezwe
 
Mnyika yale yote ulioahidi hujatekeleza hata moja, ila kwa kupiga domo bungeni hilo umefanikiwa, nia yetu ya wakazi wa ubungo ni kutekeleza uliyotuahidi vinginevyo 2015 ukae mguu sawa ukalime.

duh, yani wewe ktk yote hayo umeona kupiga domo bungeni tu? wameshindwa ccm for 51years ataweza mnyika kwa miaka hii miwili? unazikumbuka ahadi za jk 2010? ametimiza kwa asilimia ngapi mpk sasa?
 
Kamanda mnyika safi sana kwa kazi unayofanya,sisi wakazi wa ubungo tupo pamoja na wewe na tunakuamini sana,tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu,wao wana pesa na risasi sisi tunaMUNGU anayetupigania.
 
Mkuu Mnyika,kwanza nakupongeza kwa juhudi zako na endelea hivyo hivyo
Tunashukuru leo upo nasi hapa kwenye forum. Nina ombi kwako mkuu wangu. Kwa niaba ya wapigakura wako wa kimara Matosa (kimara B) kuanzia kanisa la KKT kuelekea kigango cha Matosa hatujawahi kupata maji tangia hii miundo mbinu ya kichina imewekwa lakini wanzetu wengia kuanzia Temboni wanapata maji kwa mgao mara mbili kwa wiki.Tumejaribu kufuatilia hapo Kimara DAWASCO lakini majibu yake ni kuwa tupo kilimani na maji hayawezi kufika huko mpaka wapate kibali kutoka makao makuu ya kutupagia mgao wetu wenyewe lakini tangia tumefuatilia imekuwa subirini mpaka imechosha
hii ni tangia March mpaka leo wanasema tutapangia mgao wetu

Tutashukuru kwa hilo
 
hongera mnyika.. kazi unafanya. wanaokudiss wana chuki binafsi..ni wagen tu kwao vunjo kelele wanapigia ubungo...
 

Hv kazi za mbunge ni kukutafutia ajira?kwanini usimuulize baba rizmoko hilo swali la ajira maana yeye ndiye atakuwa na jibu sahihi sio mbunge wetu bhana.
 


Hongera sana Mbunge wangu na waepukeni wasaliti mapema msikae nao karibu!!
 
Kuna tofauti Kati ya wabunge Kama Mnyika na wabunge Kama Ndesamburo.... Wewe ni Mbunge wa Chadema makao makuu,msemaji wa chama na sio msemaji wa wananchi....
Nakuombea ubadilike Kwa sababu taiga bado linakuhitaji Kwa mchango wako.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…