Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unataka achimbe mitaro na kuweka mabomba mapya. Kazi yake ni kushinikiza serikali na anafanya hivyo, wacha uchawi.Hoja yako nzuri ila wapo watu wanakusifia kwa kukutia ujinga. ukweli ni kwamba tatizo la maji nisugu na limatukela wengi fanya kazi shungulikia maji, pia huja fanya chochote kuhusu ajira. timiza ahadi wananchi tunataka kuona utekelezaji wa AMUA sio watusi kwa kikwete.
Wenzio wa Bonyokwa hawataki hata kukuona. Kiswigo humu kalalamika mpaka kakaukiwa na sauti. Mbunge wewe siyo msikivu.
Napokea kwa unyenyekevu pongezi zilizotolewa na wachangiaji mbalimbali hapa JF lakini izingatiwe kuwa michango yangu bungeni ni matokeo ya heshima mliyonipa ya kuwawakilisha. Aidha yapo maoni machache ambayo yametoa tafsiri tenge kuhusu kazi ya mbunge na wengine mmetaka nieleze nimefanya kazi gani za maendeleo jimboni Ubungo.
Tarehe kama ya leo 21 Agosti 2005 nilianza mchakato wa kuwa kugombea ubunge nikiwa kwenye chakula na watoto yatima, tarehe kama hiyo mwaka 2010 nilianza kampeni za uchaguzi mitaani Ubungo, tarehe hii hii kwa mwaka huu wa 2012 naomba niitumie kutoa taarifa fupi ya utekelezaji kwa masuala ya maendeleo katika mwaka wa fedha 2011/2012 uliomalizika tarehe 30 Juni 2012; http://mnyika.blogspot.com/2012/08/taarifa-fupi-kuhusu-kazi-za-maendeleo.html kuhusu elimu, ajira, miundombinu, maji, usalama, uwajibikaji, ardhi na afya; taarifa ya kina ya utekelezaji nitaitoa nitakapotimiza miaka miwili ya utendaji.
Hivyo, ufanisi wa ubunge wangu upimwe kwa kuzingatia msimamo huu kuhusu kazi nne za mbunge katika kuwezesha maendeleo: http://mnyika.blogspot.com/2010/03/natangaza-rasmi-dhamira-ya-kugombea.html ambao niliwaeleza wananchi wakati wa uchaguzi hivyo nilichaguliwa ikifahamika wazi kuwa huo ndio wajibu ambao nitautekeleza katika kipindi cha miaka mitano.
Bado naendelea kuamini kwamba jimbo la Ubungo na taifa kwa ujumla tutapiga hatua ya haraka zaidi ya maendeleo kupitia mabadiliko katika mifumo yetu ya mgawanyo wa rasilimali na usimamizi wa matumizi ya fedha za umma na pia kwa kuweka mazingira bora ya kisera, kisheria na kiutendaji wa sekta binafsi.Tuliyoyafanya mpaka sasa ni sehemu tu katika mahitaji makubwa ya maendeleo kutokana na pengo la miaka 50 ukilinganisha na fursa ambazo taifa letu linazo; hata hivyo naamini miaka mitatu iliyobaki itafanya miaka mitano ya kuisimamia Serikali iliyopo madarakani hivi sasa pamoja na udhaifu wote uliokuwepo kuleta tofauti katika maendeleo majimboni.
Ni katika muktadha huo wakati mwingine tunazimika kuwakilisha na kuwasilisha matakwa ya wananchi namna hii: http://www.youtube.com/watch?v=ES4OMOD_xME tukiamini kwamba watawala wenye dhamana kwa sasa ya kukusanya kodi watasikiliza na kuzingatia vipaumbele vya maendeleo vya wananchi.Aidha, baada ya kazi mkutano wa nane wa bunge naomba kutumia fursa mjadala utakaofuatia taarifa hii kupata maoni yenu kuhusu masuala ninayopaswa kuyapa kipaumbele katika kuwawakilisha na kuwatumikia jimboni katika kipindi cha mwezi Septemba mpaka Oktoba 2012 kabla ya kuanza kwa mkutano wa tisa wa bunge na pia kuhusu maandalizi ya mwaka 2013.
Kero nyingi zinazoendelea kuwepo kwa sasa ni neema iliyojificha (blessing in disguise) ili tuendelee kuunganisha nguvu ya umma kuendeleza wimbi la mabadiliko. Narudia tena kuwakumbusha kuwa nguvu ile ile tuliyoitumia kwenye kutafuta kura na kulinda kura ndio naiomba toka kwenu katika hatua hii ya kufanya kazi za kuwezesha maendeleo kwa kutimiza wajibu kila mmoja wetu kwa nafasi yake, kuisimamia serikali na kuunganisha rasilimali za wadau wengine; Maslahi ya Umma Kwanza.
kila ninapokusikia bungeni, naamini kwamba Tanzania siyo kama inavyoonekana, kuna "vichwa" sema nafasi ya kutosha haijapatikana. Tuombe mungu moto mliouanzisha, utufikishe tunakotamani!
Mimi binafsi nakuombea makubwa zaidi ya Ubunge, ikiwezekana Uwaziri Mkuu, na hata "URAIS" maana bado 'unadai'
natamani ungekuwa mbunge wangu.
Mi ni Mwananchi wa Monduli
kila ninapokusikia bungeni, naamini kwamba Tanzania siyo kama inavyoonekana, kuna "vichwa" sema nafasi ya kutosha haijapatikana. Tuombe mungu moto mliouanzisha, utufikishe tunakotamani!
Mimi binafsi nakuombea makubwa zaidi ya Ubunge, ikiwezekana Uwaziri Mkuu, na hata "URAIS" maana bado 'unadai'
natamani ungekuwa mbunge wangu.
Mi ni Mwananchi wa Monduli
Mnyika yale yote ulioahidi hujatekeleza hata moja, ila kwa kupiga domo bungeni hilo umefanikiwa, nia yetu ya wakazi wa ubungo ni kutekeleza uliyotuahidi vinginevyo 2015 ukae mguu sawa ukalime.
Big up JJ.
Mungu aendelee kukupa afya na nguvu ya kuwapigania wananchi
Hoja yako nzuri ila wapo watu wanakusifia kwa kukutia ujinga. ukweli ni kwamba tatizo la maji nisugu na limatukela wengi fanya kazi shungulikia maji, pia huja fanya chochote kuhusu ajira. timiza ahadi wananchi tunataka kuona utekelezaji wa AMUA sio watusi kwa kikwete.
Narudia tena kuwakumbusha kuwa nguvu ile ile tuliyoitumia kwenye kutafuta kura na kulinda kura ndio naiomba toka kwenu katika hatua hii ya kufanya kazi za kuwezesha maendeleo kwa kutimiza wajibu kila mmoja wetu kwa nafasi yake, kuisimamia serikali na kuunganisha rasilimali za wadau wengine; Maslahi ya Umma Kwanza.