Taarifa: Aina mpya ya utapeli mjini

64-bit

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
298
147
Nadhani hata humu ni mahala sahihi pakutolea taarifa hii:

Kumekuwa na wimbi la utapeli unaofanyika na watu wanaojipambanua kuwa wanahusika na kampuni ya usambazaji wa mayai ya kisasa, watu hawa huwaambia wateja watume fedha nusu kwa kiasi cha idadi ya tray za mayai wanazotaka then nusu iliyobaki watawalipa watakapofikisha mzigo sehemu husika hivyo mtu akituma hiyo fedha basi imekuwa ameshatapeliwa.

Namba anayotumia kufanya utapeli ni 0786869108 mtu huyu anasema yupo Kisiju na Mbeya.

Hivyo vyombo husika tunaomba mshughulikie suala hili kikamilifu.
 
Nadhani mtu wa kushughulikia hapa sio huyo tapeli ila aliye tapeliwa ndio anapaswa kukamatwa na kushitakiwa kwa ujinga na uzembe wa hali ya juu ambao unasababisha watu kuona kutapelu ni fursa ya kiuchumi. Huwezi mtumia pesa mtu usiyemjua halafu uonekane bado una akili timamu ebo!!!
 
Niungane nawe, unatapeliwaje kijingajinga, mtu mzima unatumaje hela ya mayai wakati ukitembea mjini station za wauza mayai wa jumla kibao, labda kama yeye alikuwa na nia ya kutapeli akatapeliwa.

Maana kafanya mawasiliano na walio Kisiju na walio Mbeya.

Everyday is Saturday... :cool:
 
Tatizo letu tunatumia akili nyingi katika uwongo, uwizi, umbeya, unafiki, ulozi na siyo katika maendeleo, dunia imekuwa ni kama kijiji watu tunafanya biashara na watu kutoka mataifa mbalimbali bila ya kujuana tena biashara ya pesa ndefu kwa mitandano tu. Tatizo hamjui tatizo la kutokuwa muaminifu. Waswahili wanasema za mwizi ni 40.
 
Kuna aina nyingi za utapeli .
1.kuna wale matapeli ambao wanawatapeli wauzaji wa simu kwenye mitandao yaani anaorder simu nyingi na unamletea alipo mfano mkutano Ubungo stendi,au Temeke Sudani au Stendi ya Mbezi mwisho ukishapokea mzigo anajifanya anakupa pesa kwa njia ya NBC bank kisha unapokea meseji kutoka NBC kuwa umepokea pesa ya malipo kutoka kwa labda Juma lakini ukweli hiyo huwa siyo mseji ya pesa huwa ni meseji tu ya kawaida mkiachana na wewe ukitaka kutoa pesa ndipo inagundua kuwa umepigwa,
2.Upigwaji mwingine ni wa kutapeliwa Magari huko mtandao wa kupatana hivyo kama unataka kununua gari kupitia Mtandao hakikisha wakati wa malipo unakwenda kupewa akaunti ya benki ndani ya ofisi za Yard usikubali kulipa juu kwa juu maana wengi wanaoweka matangazo huko Mtandaoni ni Matapeli tu kwa ushauri wa kina nenda kachague gari kwenye yard bila kumpa taarifa yoyote yule na hakikisha unaingia ndani ya ofisi za Yard naunamlipa muhusika kulingana na akaunti aliyekupa au cash,Pia jitahidi kusoma matangazo yote yaliyobandikwa hapo yard .
3.Utapeli wa fashion za kimasai
4.Utapeli wa Mecury
5.Utapeli kwa njia ya Mtandao huu inawahusu hasa mawakala na wale wenye pesa nyingi mitandaoni
6............
 
Nadhani hata humu ni mahala sahihi pakutolea taarifa hii:

Kumekua na wimbi la utapeli unaofanyika na watu wanaojipambanua kua wanahusika na kampuni ya usambazaji wa mayai ya kisasa, watu hawa uwaambia wateja watume fedha nusu kwa kiasi cha idadi ya tray za mayai wanazotaka then nusu iliyobaki watawalipa watakapo fikisha mzigo sehemu husika hivyo mtu akituma hiyo fedha basi imekua ameshatapeliwa.

Namba anayotumia kufanya utapeli ni 0786869108 mtu huyu anasema yupo kisiju na mbeya.

Hivyo vyombo husika tunaomba mshuulikie swala hili kikamilifu
Kwann usimwambie pesa ipo lete mzigo ukifika unachukua pesa yote
 
Mbeya kote huko, miezi miwili iliyopita dada mmoja kafanyiwa hivyo hapa hapa Daslam, uzuri anayefanya huo utapeli anamfahamu na anadai watu wengi wamekwisha tapeliwa akiwadanganya anasupply mayai ya kisasa.

Dada baada ya kuona mizinguo na pesa ashatoa akapeleka shitaka polisi. Polisi ikaamuliwa arudishe pesa ya watu, kapiga danadana kurudisha pesa mwisho wa siku ikabidi waangalie kitu chake chenye thamani ya pesa aliyotoa dada kwa huyo mdanganyifu. Kikaamuliwa kiwanja chenye thamani ya Tsh.3,000,000.
Hata huyo anayejipambanua yupo Mbeya yawezekana 100% yupo Daslam.
 
Nadhani hata humu ni mahala sahihi pakutolea taarifa hii:

Kumekua na wimbi la utapeli unaofanyika na watu wanaojipambanua kua wanahusika na kampuni ya usambazaji wa mayai ya kisasa, watu hawa uwaambia wateja watume fedha nusu kwa kiasi cha idadi ya tray za mayai wanazotaka then nusu iliyobaki watawalipa watakapo fikisha mzigo sehemu husika hivyo mtu akituma hiyo fedha basi imekua ameshatapeliwa.

Namba anayotumia kufanya utapeli ni 0786869108 mtu huyu anasema yupo kisiju na mbeya.

Hivyo vyombo husika tunaomba mshuulikie swala hili kikamilifu

Sasa huu ndio utapeli MPYA? Utatumaje fedha kwa mtu usiyemjua? Alete mzigo ndio umpe cash yake au mwambie kama ana mwakilishi sehemu ulipo ampe huyo mwakilishi wake mayai kisha akiyaleta ndio apewe pesa,ukiona anasema hana wakal/mwakilishi basi huyo ni tapeli.....wafanyabiashara wa ukweli huwa na wawakilishi mikoa yote.
 
Jana Kuna jamaa kanipigia kwa namba ya tigo.
Alafu anasema anafanya kazi HALOTEL.
akaniambia Kuna hela imetumwa kimakosa kwenye laini yako .nikamuuliza sh ngapi akajibu laki 2 na elfu 45.
Nikakwambia Mimi hyo hela sijakuona mwambie huyo aliyetuma atume Tena.
Akakata simu.

Kuna mwingine wa tigo pesa.anajifanya Ni mfanyakazi wa tigo.
Akajifanya kunifundisha jinsi ya kuuza vifurushi vya tigo.
Mimi namsikiliza tu.
Mara bonyeza moja,Mara bonyeza mbili.n.k
Mwisho ananiuliza hyo meseji ya mwisho imeandikwaje
NIKAKWAMBIA IMEANDIKWA SINA SALIO LA KUTOSHA
AKANITUKANA kwanini nakaa na laini isiyokuwa na hela.

Back
Top Bottom