Jiwe la Ukara
Member
- Jul 15, 2011
- 44
- 31
TAARIFA KWA UMMA
TAHADHARI YA UWEPO WA DAWA BANDIA KWENYE SOKO
1. Utangulizi
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Na.1 ya mwaka 2003. Mamlaka ina jukumu la kudhibiti ubora, ufanisi na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii.
Kuanzia tarehe 21 Agosti 2011 hadi tarehe 8 Septemba 2011, TFDA ilifanya ukaguzi katika maeneo 390 ya kuuzia dawa na kutolea huduma za afya yaliyopo katika mikoa 13 hapa nchini ili kubaini ubora na usalama wa dawa zilizopo katika soko na kuchukua hatua stahiki. Mikoa hiyo ni Ruvuma, Dodoma, Mwanza, Mtwara, Lindi, Morogoro, Mbeya, Kagera, Manyara, Pwani, Tanga, Kigoma na Dar Es Salaam.
2. Matokeo ya ukaguzi
Kufuatia ukaguzi uliofanyika, TFDA imefanikiwa kukamata aina tano (5) za dawa bandia na pia dawa moja (1) ambayo imesambazwa kwa kiasi kikubwa bila kuwa imesajiliwa na TFDA kama Sheria Na.1, 2003, inavyoelekeza. Dawa bandia zilizokamatwa ni kama ifuatavyo:-
a. Artemether + Lumefantrine (ALu) yenye jina la biashara "Coartem" ambayo ni mojawapo ya Dawa Mseto ya kutibu ugonjwa wa Malaria.
b. Dawa ya kutuliza maumivu ya Ibuprofen ambayo inauzwa kama Erythromycin Stearate BP 250mg.
c. Pheoymethylpenicillin (vidonge) yenye jina la biashara Penizin - V d. Elphedrin na Elphedren zote za vidonge.
e. Laifin (Sulphamethoxazole + Pyrimethamine) vidonge. Dawa ambayo haijasajiliwa ni Orodar (Sulfadoxine + Pyrimethamine) vidonge. Maelezo ya kina yanayotofautisha dawa halisi zilizosajiliwa na dawa bandia ni kama ilivyoanishwa katika jedwali hapa chini:
Na. | Dawa halisi iliyosajiliwa | Maelezo ya dawa bandia |
1. | · Jina la dawa: Artemether + Lumefantrine (ALu) (Coartem) tablets · Mtengenezaji: Norvatis Pharmaceuticals Corporation, Suffern, New York, USA · Mwaka wa kutengenezwa:2007 · Mwaka wa kumaliza matumizi:2009 · Sehemu zinapopaswa kupatikana:Vituo vya afya Serikali | · Jina la dawa: Artemether + Lumefantrine (ALu) (Coartem) tablets · Mtengenezaji: Norvatis Pharmaceuticals Corporation, Suffern, New York, USA · Mwaka wa kutengenezwa: umebadilishwa kuwa 2009 · Mwaka wa kumaliza matumizi: umebadilishwa kuwa 2012 · Sehemu zinapopatikana kwa sasa: Maduka ya Dawa (Famasi na Maduka ya Dawa Muhimu) na Vituo vya Afya vya watu Binafsi |
Ufafanuzi: a) Dawa hizi ziliisha muda wake wa matumizi. Hivyo mwaka wa kutengenezwa umefutwa kutoka mwaka 2007 na kuwa mwaka 2009. Aidha, mwaka wa kumaliza matumizi umefutwa kutoka mwaka 2009 na kuwa mwaka 2012 b) Dawa hizi zimepatikana katika wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro |