T.B Joshua na Askofu Gwajima!

T.B Joshua na Askofu Gwajima!

Mwamakula

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2010
Posts
1,890
Reaction score
384
(1) T.B Joshua alitabiri kuwa Lowasa atashinda kwa Kishindo Urai 2015.

(2) CCM wakasema Lowasa amefuata Uchawi Nigeria.

(3) Wakati wa Kura za Maoni CCM wakakata Jina la Lowasa ili kufifisha Ndoto ya Urais.

(4) Askof Gwajima akajitokeza na Kumshawishi LOWASA ahamie UKAWA.

(5) Rais Johnathan Kutoka Nigeria akaja kushuhudia uchaguzi Tanzania.

(6) Rais Johnathan ni muumini wa T.B Joshua na wote wanatoka Nigeria ambako Bokoharam wamaezindua kiwanda cha Silaha.

(7) Baada ya matokeo ya Uchaguzi UKAWA wametoa vielelezo kuwa Tume ya Uchaguzi imeiba kura na kumpa Mangufuli huku rais Johnathan anashuhudia.

(8) CCM wanao amini kuwa Lowasa alifuata Ucahwi kwa T.B wanageuka na kumwita T.B kuja Tz.

(9)T.B anaingia Tanzania huku akiwa peku peku uwanja wa Ndege na kuanza kumshawishi Lowasa na Ukawa kuwa ana ujumbe wa amani

Maswali yangu ni haya yafuatayo:

(1) Kati ya Askofu Gwajima na T.B nani mpatanishi wa Kweli.

(2) Kama T.B ana amini katika upatanishi ni kwa kwa nini hakuanza kukutana na Askof Gwajima ambaye ni kiongozi wa dini na mtu wa Karibu na Lowasa ili ajue mambo ya kiroho lakini anasema yote hayo Mungu anajua.

(3) T.B Jushua ana sululisha mgogoro huo akiwa anawashirikishirikisha viongozi gani wa Kiroho hapa nchini?

(4) T.B ameja kama kiongozi wa Kiroho ama kiongozi wa Nigeria?

(5) T.B ni mgeni wa nani?? Hapa nchini nani alifanya mipango ya ujio wa T.B?

(6) Paspo haki hapana amani , sasa ni kwa vipi anaweza kutafuta amani kwa kuficha kujua haki ilivyopotea?

Nawaomba viongozi wa kiroho katika Tz kudumu kuomba ili kujua Nabii wa uongo ili Taifa zima lisije likaingia katika kuabudu Mizimu hasa ukizingatia kuwa leo hii kule Marekani wanasherekea sikuuu ya mizimu [Anaglia gzt la TzDaima]
 
mmezidi bwana TB ,TB mwacheni mtumishi wa Mungu afanye kazi yake aliyotumwa na Mungu kwa ajili ya nchi yetu, akimaliza ataondoka.
na hakuna aliyesikia unabii wake kuusu uraisi wa Tanzania.
hayo ni yenu na yamekwisha pita na tuna mshukuru Mungu tuna Raisi mpya,kilichobaki ni kujenge nchi yetu.
 
Kushindwa na kutangwazwa mshindi ni vitu viwili tofaoti
 
Uko wapi ushahidi kuwa TB Joshua alitabiri ushindi wa Lowassa?
Hizo ni propaganda tu.
 
Nilishawauliza mna video clip ya utabiri wa Lowassa? Msitulishe maneno na propaganda zilizoganda
 
mmezidi bwana TB ,TB mwacheni mtumishi wa Mungu afanye kazi yake aliyotumwa na Mungu kwa ajili ya nchi yetu, akimaliza ataondoka.
na hakuna aliyesikia unabii wake kuusu uraisi wa Tanzania.
hayo ni yenu na yamekwisha pita na tuna
mshukuru Mungu tuna Raisi mpya,kilichobaki ni kujenge nchi yetu.[/QUOTE

Kwanini kashindwa kuhubiri Amani huko kwao Nigeria kila siku wanauwana? Au ana uchungu zaidi kwa nchi zingine kuliko nchi yake??!!!
 
TB joshua ni tapeli tu kama matapeli wengine sugu.Tofauti yake yeye anatumia jina la dini. Hebu rudini katika maandiko angalieni Biblia inasema nini kuhusu wanaojiita manabii siku za mwisho huku wakikataa kuishi kama Yesu alivyoaagiza. "Uza vyote wagawie maskini kisha unifuate". hapo manabii wengi hutoka nduki na visingizio kibao.
 
Kama EL anasema kweli kuwa alipata kura 62% na nec ikabadilisha matokeo basi huo ni wazi kuwa ni ushindi wa kishindo. Cha msingi ni pande tuhumu na tuhumiwa kuja na kutuwekea mambo sawa na tukaelewa ili kuondoa hayo maneno ya mtaani!
 
Gwajima ni mshenga anayepaswa kupatanisha Lowassa na Dr Slaa na wala si Dr Magufuli
 
Mleta mada acha porojo zisizo na tija kwa sasa. Fanya kazi.
 
Utangulizi wako una dondoo 9 nyingi ni za kutungwa aidha na wewe mwenyewe au na watu uliowasikiliza na kuwaamini. Ya ukweli katika dondoo zako 9 ni kuanzia namba 3 mpaka 6 tu, yaani dondoo 4 tu. Haya ya kusema mara anapatanisha au kaleta ujumbe au alitabiri au kuna vielelezo yote ni uzushi. Uwe makini.

(1) T.B Joshua alitabiri kuwa Lowasa atashinda kwa Kishindo Urai 2015.

(2) CCM wakasema Lowasa amefuata Uchawi Nigeria.

(3) Wakati wa Kura za Maoni CCM wakakata Jina la Lowasa ili kufifisha Ndoto ya Urais.

(4) Askof Gwajima akajitokeza na Kumshawishi LOWASA ahamie UKAWA.

(5) Rais Johnathan Kutoka Nigeria akaja kushuhudia uchaguzi Tanzania.

(6) Rais Johnathan ni muumini wa T.B Joshua na wote wanatoka Nigeria ambako Bokoharam wamaezindua kiwanda cha Silaha.

(7) Baada ya matokeo ya Uchaguzi UKAWA wametoa vielelezo kuwa Tume ya Uchaguzi imeiba kura na kumpa Mangufuli huku rais Johnathan anashuhudia.

(8) CCM wanao amini kuwa Lowasa alifuata Ucahwi kwa T.B wanageuka na kumwita T.B kuja Tz.

(9)T.B anaingia Tanzania huku akiwa peku peku uwanja wa Ndege na kuanza kumshawishi Lowasa na Ukawa kuwa ana ujumbe wa amani

Maswali yangu ni haya yafuatayo:

(1) Kati ya Askofu Gwajima na T.B nani mpatanishi wa Kweli.

(2) Kama T.B ana amini katika upatanishi ni kwa kwa nini hakuanza kukutana na Askof Gwajima ambaye ni kiongozi wa dini na mtu wa Karibu na Lowasa ili ajue mambo ya kiroho lakini anasema yote hayo Mungu anajua.

(3) T.B Jushua ana sululisha mgogoro huo akiwa anawashirikishirikisha viongozi gani wa Kiroho hapa nchini?

(4) T.B ameja kama kiongozi wa Kiroho ama kiongozi wa Nigeria?

(5) T.B ni mgeni wa nani?? Hapa nchini nani alifanya mipango ya ujio wa T.B?

(6) Paspo haki hapana amani , sasa ni kwa vipi anaweza kutafuta amani kwa kuficha kujua haki ilivyopotea?

Nawaomba viongozi wa kiroho katika Tz kudumu kuomba ili kujua Nabii wa uongo ili Taifa zima lisije likaingia katika kuabudu Mizimu hasa ukizingatia kuwa leo hii kule Marekani wanasherekea sikuuu ya mizimu [Anaglia gzt la TzDaima]
 
TB joshua ni tapeli tu kama matapeli wengine sugu.Tofauti yake yeye anatumia jina la dini. Hebu rudini katika maandiko angalieni Biblia inasema nini kuhusu wanaojiita manabii siku za mwisho huku wakikataa kuishi kama Yesu alivyoaagiza. "Uza vyote wagawie maskini kisha unifuate". hapo manabii wengi hutoka nduki na visingizio kibao.

Yesu hakumaanisha physical assets, alikuwa anamaanisha uache Yale yote matamu unayoyapenda kisha umfuate. Matamu ni Kama uzinzi, ulevi, anasa, na dhambi nyingine tuzitendazo.
 
TB joshua ni tapeli tu kama matapeli wengine sugu.Tofauti yake yeye anatumia jina la dini. Hebu rudini katika maandiko angalieni Biblia inasema nini kuhusu wanaojiita manabii siku za mwisho huku wakikataa kuishi kama Yesu alivyoaagiza. "Uza vyote wagawie maskini kisha unifuate". hapo manabii wengi hutoka nduki na visingizio kibao.
Chunga sana ulimi wako ndugu yangu. Haya ni maisha, huwezi jua kesho. Unaweza kuja kuumwa vibaya, huyo huyo unaemwita tapeli ndo akaja kukuponya. Hujui lolote kuhusu TB joshua, hivyo ni bora unyamaze.
 
Uko wapi ushahidi kuwa TB Joshua alitabiri ushindi wa Lowassa?
Hizo ni propaganda tu.

Watu wanapokaa na kutunga mambo ya uongo uongo namna hii ndiyo chanzo cha nchi yetu kuendelea kuzidi kuwa masikini. Maana huu muda ungetumika kufanya mambo ya msingi kabisa tungekuwa mbali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom