dropingcoco
Senior Member
- Jun 21, 2008
- 124
- 11
juzi nimepanda bus tajwa hapo juu, kwa kweli abiria tuliteseka sana, lilikuwa linaendeshwa na dereva anaitwa Salakana,huyu bwana alikuwa anakimbia sana na mbaya zaidi huku anaongea na simu kila wakati, watu tulihama makampuni mengine tukiamini wapo makini,lakini sasa wanapoelekea watapoteza wateja, ukizingatia na magari yao siku hizi yameanza kuwa mabovu....tunawashauri wajirekebishe

JUZI NDIO SIKU GANI?
Mlikuwa mkitoka wapi kwenda wapi?
Ukitaka mambo haya yafanyiwe kazi weka uthibitisho wa taarifa zako!...Mimi nipo hatua 30 toka ofisini kwao, naweza fanya lolote nikipata usahihi wa taarifa hizi!

Vinginevyo KILIMANJARO ni kampuni ya usafirishaji yenye heshima sana kwa route za Dar-Arusha!
juzi maana yake nini?ukienda oficn utajua route,dereva na kondakta wa hilo bus.hii kadhia hutokea sana halafu ukiwapeleka polisi wanahonga,dawa yao ni kuwaanika namna hii ili wajirekebishe!
Wanasoma Jamiiforum?
hata kama hawasomi taarifa watazipata tu!jf kiboko we subiri watakurupuka huko waliko kujibu tuhuma.
Kama vipi ni kuwatosa tu wapate heshima bahati nzuri route ya Dar-Arusha ina magari mengi tu ya maana. Karibu Dar express!!
Kama vipi ni kuwatosa tu wapate heshima bahati nzuri route ya Dar-Arusha ina magari mengi tu ya maana. Karibu Dar express!!
Pole best!a a....inawezekana tulipanda bus moja nn,mm nilipanda jmosi kutoka Ars-Dar, huyohuyo dereva alikuwa anaendesha na alikuwa anaongea na simu kila wakati, na tulipofika sijui panaitwa kisangara gari liliharibika,tulikaa almost lisaa lizima,kutoka hapo mwendo ulikuwa mdundo, kwa kweli nilikuwa siwezi kusafiri na kampuni nyingine kwa route hiyo lakini itabidi nihame, kwa anayemfahamu mmiliki wa hayo mabus na namba yake ya simu atupatie ili aweze kusababishwa kuwafundisha madereva wake kuwa na adabu na roho za watu
Pole best!
Ningejua ile tiketi ni ya basi hilo ningeifanya nap-kin dakika ileile!
Itabdi sasa urudi na Ngorika ile ya mchina!