Syria inafuatia baada ya Libya

Syria inafuatia baada ya Libya

Waarabu ivi wamelogwa au? Wana macho hawaoni wana masikio hawasikii wana akili hawafikili! Wana laana labda
 
Graphic video

 
Last edited by a moderator:
Waziri mkuu wa Syria, amejitenga na utawala wa Assad na kukimbilia Jordan usiku wa kuamkia Jumatatu. Msemaji wa waziri huyo amekanusha taarifa ya televisheni ya taifa ya Syria kwamba waziri mkuu alifukuzwa kazi.
Mohammed al-Otri, ambaye ni msemaji wa waziri mkuu wa Syria Riad Hijab, alilisoma tamko la waziri huyo katika kituo cha televisheni cha al-Jazeera. "Ninatangaza kujitenga na utawala huu unaofanya mauaji na ugaidi na nimeamua kujiunga na wapinzani," alisema Hijab na kuongezea kwamba Assad anafanya mauaji ya halaiki dhidi ya raia wa taifa lake. Msemaji wa waziri huyo alieleza kwamba mpango wa Hijab kuikimbia serikali ya Assad ulipangwa kwa miezi kadhaa na hatimaye ulifanikiwa leo usiku ambapo Hijab pamoja na mawaziri wengine wawili na maafisa watatu wa jeshi walivuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Jordan.
Huko Hijab aliungana na familia yake na inasemekana kwamba yuko katika mazingira salama. Hijab alikuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa madhehebu ya Sunni katika utawala wa Assad ambao kwa sehemu kubwa unajumuisha waumini wa Kialawi. Kiongozi huyo, mwenye umri wa miaka 46, aliteuliwa kuwa waziri mkuu Juni 6 mwaka huu. Kabla ya hapo alikuwa waziri wa kilimo.
 
Hizi nchi za kiislamu huwa sizielewi kabisa. Sijui hizi tawala zinataka au hazitaki nini? Damu ya Hariri haitokaa imwache Assad asilani na kwa hakika ndiyo inayomwita. Ninaweza kuona kitanzi shingoni mwa Assad; rest in hell na uwasubiri Ahmedinejad na Khamenei kwani soon watakuwa wageni wa Lucifer pia.
 
Back
Top Bottom