Synovate: Vinara tisa urais 2015

Synovate: Vinara tisa urais 2015

...kila ninapopata bahati ya kuisoma taarifa ya utafiti uliofanywa Synovate,huo napata tabu sana kuutofautisha utafiti wao na utabiri wa marehem Shekhi Yahaya...
 
Utafiti huu hauna togauti na U tabiri wa Shekhe Yahaya, hivyo kwa yule mwenye akiri ataupuuza ila kwa yule mshabiki ataendelea kuushabikia. Haijawahi kutokea kuwa na utafiti hambao hauna Sample au dodoso hivyo ni saw tu na ule aliokuwa anaufanya Shekhe Yahaya maana ulikua ni wamaoni yake binafsi.
 
Mkuu Regan Morgans, kama haya ni matokeo ya utafiti, sasa hii ya wewe kuuliza kama jee ni kweli, unamaana unamashaka na utafiti huu wa Synovate?.

Kwa kusaidia tuu, sio tuu ni kweli kabisa kuwa EL anaanza kukubalika zaidi, bali baadhi ya Watanzania wanaanza kuukubali ukweli kuwa EL ni jembe la ukweli!.

Haya maroroso tunayoyashuhudia katika kuporomoka kwa elimu yetu ni baadhi tuu ya matokeo ya serikali dhaifu ya JK kuitelekeza mipango ya EL na shule za kata ili kumkomoa, sasa imejikuta yenyewe ndio inakomoleka na kufikia 2015, EL atakuwa juu kabisa on top of the charts ili kufungua tuu njia na kunyoosha mapito ya "the chosen one!".

" Jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!".

Yeye ndie ule mwamba wa Kaskazini unaozungumziwa kwenye maandiko mbalimbali kuwa
"Wewe ni mwamba, juu ya mwamba huu, nitalijenga taifa langu!".

Pasco.
Pasco Lowasa hawezi kuwa na majibu ya matatizo ya tanzania ya sasa labda asiwe mwanaCCM! Mgombea yoyote wa CCM hafai kuongoza hili taifa kuanzia 2015! Synovate huwa inatumiwa kisiasa, na wanaendelea na kazi yao ya kutumika! Wameshindwa kumuondoa Dr. Slaa kwenye mioyo ya watanzania sasa wanatumia tafiti mufilisi kuwaaminisha watanzania kuwa eti sasa Dr. Slaa hakubaliki!
 
Last edited by a moderator:
Sasa wanataka watuaminishe nini sisi wananchi juu ya uo utafiti wao
 
Je Mzee wa Gombe ana asilimia ngapi? Kama mmemtupa nje, tegemeeni lazima litakuja kuyakanusha matokeo ya utafiti wenu. Maana jamaa linajiona eti kama watu wanaliona Obama flani vile!
 
Mwamba wa kaskazini akaombe useneta wa kakazini,sisi tuna taka kiongozi bora,mwamba kwa watanzania.
 
Mhhh... malengo ya tafiti za synovate si zinafahamika... Ni lini walifanya tafiti zinazo endana na uhalisia???
 
Ivi awa synovate hawana kazi ya kufanya? Tafiti hazina hata mantiki,na sijui wanatumwaga na nani?
 
utafiti unaonyesha kuwa Lowassa anazid kukubalika kadri ya siku zinavyozd kwenda. JE HII NI KWELI?
2013 hii,na kadiri tunavyokaribia 2015 watakuja na mfululizo wao wa tafiti unaoonyesha EL anazidi kukubalika kadiri 2015 inavyokaribia,mjini mipango bwana.
 
mimi nadhani haya ni maoni binafsi ya mhariri hayana chembe ya ukweli
 
Hii synovate kwa serkali makini ilipaswa kufungiwa na si kufungia gazeti makini kama Mwanahalisi.
 
Ongera Dr. endelea kukaza buti.

Mbona inaonekana umaarufu wa Dr. Slaa umeporomoka kutoka 42% hadi 17%? Hii inaashiria nini? Watu wamemchoka au wameichoka CHADEMA? Umaarufu wa CHADEMA nao umeshuka! Inaonekana kama kuna negative correlation kati ya M4C na umaarufu wa CHADEMA.

Mkuu Ritz umeamka?
 
Last edited by a moderator:
CCM yatamba
Katika utafiti huo,
CCM kimeonyesha kuwa ni chama ambacho asilimia 52 ya wananchi wangependa kujiunga nacho, kikiwa kimepanda chati kwa asilimia moja kutoka asilimia 51 mwaka jana.

Kwa upande wa
Chadema, wananchi ambao wanapenda kujiunga nacho imeshuka kutoka asilimia 35 mwaka 2011 hadi 31 mwaka jana.



kwa maana hiyo ccm itaendelea kupanda huku chadema ikizidi kuporomoka???????????????????? maana nyingine ni kwamba chadema itakuwa na mgombea mzuri lakini chama dhaifu.
 
Kwangu mimi naamini rushwa ndo tatizo kubwa na hayo matatizo mengine yanatokana na tatizo rushwa
 
Mbona inaonekana umaarufu wa Dr. Slaa umeporomoka kutoka 42% hadi 17%? Hii inaashiria nini? Watu wamemchoka au wameichoka CHADEMA? Umaarufu wa CHADEMA nao umeshuka! Inaonekana kama kuna negative correlation kati ya M4C na umaarufu wa CHADEMA.

Mkuu Ritz umeamka?


Na hapo utafiti umefanyika kabla ya kufukuzwa kwa madiwani wawili wa musoma, makam mwenyekiti wa bavicha pamoja na wenzake akina mwampamba na wale waliojitoa akina kisandu na eddo makata
 
Pasco Lowasa hawezi kuwa na majibu ya matatizo ya tanzania ya sasa labda asiwe mwanaCCM! Mgombea yoyote wa CCM hafai kuongoza hili taifa kuanzia 2015! Synovate huwa inatumiwa kisiasa, na wanaendelea na kazi yao ya kutumika! Wameshindwa kumuondoa Dr. Slaa kwenye mioyo ya watanzania sasa wanatumia tafiti mufilisi kuwaaminisha watanzania kuwa eti sasa Dr. Slaa hakubaliki!

PUNGUZA MAHABA YASIYO NA MAANA DOGO, ulitaka apewe asilimia mia wakati hakubaliki???? tumia kichwa kwa recomended use usibadili matumizi
 
Shirika la utafiti la Synovate, limetoa matokeo ya utafiti uliofanyika mwezi December mwaka jana ambayo yanonyesha ya kuwa endapo uchaguzi ungefanyika saa,katibu mkuu wa CHADEMA, Dr Willbrod.Slaa, angeibuka mshindi kwani anaongoza katika orodha ya wanaotajwa kugombea uraisi.

Katika matokeo hayo Dr.Slaa amepata ailimia 17 akifuatiwa na waziri mkuu Mizengo Pinda aliepata ailimia 9 huku akifungana na naibu katibu mkuu wa CHADEMA mh. Zitto kabwe ambae nae amepata asilimia 9.

Wengine ni waziri wa ujenzi Dr.Magufuli aliepata asilimia 8 akifuatiwa na mh. Lowassa aliepata ailimia 7 huku mwenyekiti wa taifa wa CUF mh. Lipumba akipata ailimia 5.

Hata hivyo, kura za Dr.Saa zimeshuka kwa asilimia 25 kutoka asilimia 42 alizopata mwaka 2011 na hata mh.Pinda nae kura zake zimeshuka kwa asilimia 3 kutoka asilimia 12 alizopata mwaka 2011, wakati mh. Zitto kabwe asilimia zake zimebaki kama zilivyokuwa mwaka 2011 kwa kupata kiwango hicho hicho cha asilimia 9.

Pia,wamo waziri wa mambo ya nje,mh.Membe,ambae amepata ailimia 4 akifungana na mwenyekiti wa CHADEMA,mh.Mbowe ambae nae amepata asilimia 4 na waziri wa ushirikiana wa Afrika Mashariki,mh.Samuel Sitta aliepata asilimia 2.

Source:Mwananchi online la trh 26/02/2013.
 
Tukikaribia uchaguzi hawa hawa watasema Slaa ni wa pili kisa mlungula wa chama Tawala
 
Back
Top Bottom