Synovate: Vinara tisa urais 2015

Synovate: Vinara tisa urais 2015

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
WAKATI baadhi ya wanasiasa wakiwa wameanza kujiwinda kwa ajili ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Shirika la Utafiti la Synovate limetoa matokeo ya utafiti wake ambao unaonyesha vigogo tisa kuwamo katika mchuano huo.

Utafiti huo umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi baada ya kuongoza orodha hiyo akipata asilimia 17.

Katika matokeo ya utafiti huo uliofanywa Desemba mwaka jana, Dk Slaa anafuatiwa kwa mbali na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amefungana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kila mmoja akipata asilimia tisa.

Hata hivyo, licha ya kuongoza, Dk Slaa ameporomoka kwa asilimia 25 ikilinganishwa na matokeo ya utafiti kama huo uliofanywa na taasisi hiyo mwaka 2011 ambapo alipata asilimia 42.

Kadhalika, umaarufu wa Pinda ambaye anaongoza miongoni mwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeshuka kwa asilimia tatu kutoka 12 za mwaka juzi, wakati Zitto ameendelea na kiwango kilekile cha asilimia tisa alizopata katika utafiti uliotangulia.

Wengine wanaofuata na asilimia walizopata kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (8), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (7) na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (5).

Pia wamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (4) ambaye amefungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (4) na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2).

Ikilinganishwa na utafiti wa 2011, Lipumba ameporomoka kwa asilimia tisa.
Lowassa amepanda kwa asilimia sita, Dk Magufuli asilimia nne, Mbowe na Membe wamepanda kwa asilimia mbili kila mmoja, wakati Sitta amebaki katika kiwango kilekile cha asilimia mbili.

Hata hivyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wananchi ambao hawana uamuzi wa kuchagua mtu yeyote kati ya hao kwa sasa ni asilimia 18, likiwa ni ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na utafiti uliotangulia.

CCM yatamba
Katika utafiti huo, CCM kimeonyesha kuwa ni chama ambacho asilimia 52 ya wananchi wangependa kujiunga nacho, kikiwa kimepanda chati kwa asilimia moja kutoka asilimia 51 mwaka jana.

Kwa upande wa Chadema, wananchi ambao wanapenda kujiunga nacho imeshuka kutoka asilimia 35 mwaka 2011 hadi 31 mwaka jana.

Uwezekano mkubwa wa CCM kupanda chati ni kutokana na ukweli kuwa mwaka jana kilikuwa na uchaguzi ulioanzia ngazi ya mashina hadi taifa na kuibua vuguvugu kubwa masikioni mwa wananchi.

Chadema hakikuwa na harakati kubwa za kisiasa ukiacha kampeni ya Movement For Change (M4C), ambayo kwa kiasi haikuwa na pilika kama uchaguzi wa CCM.
Chama kingine ni CUF ambacho kimeporomoka kwa kupata asilimia 10 mwaka 2011 hadi nne mwaka 2012.

Hata hivyo, asilimia ya wananchi kutokutaka kujihusisha na chama chochote imepanda kutoka asilimia mbili mwaka 2011 hadi 12 mwaka 2012.

Rushwa
Katika suala la rushwa nchini, utafiti huo umeonyesha kuwa kati ya watu 10 waliohojiwa, wanne walikuwa na maoni kuwa rushwa imeongezeka kufikia asilimia 41, asilimia 30 walisema iko palepale, asilimia 23 walisema imepungua na asilimia tano hawajui.

Utafiti huo unaonyesha kuwa mapambano dhidi ya rushwa hayajabadilika tangu 2011katika taasisi za Serikali ukisema haionekani kama kuna utashi wa kisiasa kupambana na tatizo hilo katika taasisi hizo kama Jeshi la Polisi na Mahakama ambazo zimeonekana kuwa nyuma katika mapambano hayo.

Katika utafiti huo, polisi ndiyo inayoongoza kwa rushwa baada ya asilimia 33 ya watu waliohojiwa kulitaja jeshi hilo, ikifuatiwa na Mahakama asilimia 16 na sekta ya afya ikiwa na asilimia 16.

Utafiti huo umeonyesha matatizo makubwa yanayoikabili nchi kwa sasa ni njaa, gharama za maisha, umaskini, migogoro ya kidini na ukosefu wa ajira.

"Asilimia 50 wametoa maoni kuwa njaa ni tatizo kubwa ikifuatiwa na gharama za maisha asilimia 44, migogoro ya ya kidini asilimia 43 na ukosefu wa ajira asilimia 34."

"Inamaanisha kuwa rushwa na mfumuko wa bei havichukuliwi kama ni tatizo kwa Watanzania wengi kama ilivyojionyesha mwaka 2011," inaeleza taarifa ya utafiti huo.

Wananchi wameeleza kuwa mambo muhimu ambayo yanatakiwa kupewa kipaumbele ni pamoja na sekta ya afya kwa asilimia 24, elimu asilimia 21, ajira asilimia 18, chakula asilimia 17 na miundombinu asilimia 16.

Source: Mwananchi
 
utafiti unaonyesha kuwa Lowassa anazid kukubalika kadri ya siku zinavyozd kwenda. JE HII NI KWELI?
 
huu utafiti mimi wala siuamini yaani mizengo Pinda ashike nafasi ya pili? kwa Lipi alilofanya haswa hili la kulia bungeni au kusema Liwalo na Liwe na maswahibu ya Dr. Ulimboka??
 
Hivi mtu unawezaje kuandika habari yooooote hii, na kuweka asilimia zooote hizo, bila kutoa sample space ilikuwa vipi (watu wangapi, kutoka wapi etc) na methodology iliyotumika ( wamepewa questionnaires, wamepigiwa simu etc).

Gazeti lina mhariri hili?

Tutajuaje kama sample space si madarasa mawili ya shule moja ya sekondari yanayojumuisha wanafunzi waliojichokea na kujaza questionnaires randomly kama sehemu ya adhabu ya utovu wa nidhamu?

NB: The original post has been updated with more details since this post demanded a better explanation.
 
Hivi mtu unawezaje kuandika habari yooooote hii, na kuweka asilimia zooote hizo, bila kutoa sample space ilikuwa vipi (watu wangapi, kutoka wapi etc) na methodology iliyotumika ( wamepewa questionnaires, wamepigiwa simu etc).

Gazeti lina mhariri hili?

Tutajuaje kama sample space si madarasa mawili ya shule moja ya sekondari yanayojumuisha wanafunzi waliojichokea na kujaza questionnaires randomly kama sehemu ya adhabu ya utovu wa nidhamu?

vipi na wewe ni mgombea?
 
Spinning kama hizi zitauzwa sana ikizingatiwa wanunuzi ni wengi nchini.

Hii kwa lugha za mitaani unaweza kuita kata funua (chop and change) ili kumtoa nyoka pangoni na kusikia kelele zake.

Siasa ni mchezo mchafu (political marketing planning process)
 
mwanangu mi unanikwaza sana unapotoa data ambazo huna hukakika nazo wenye kuwachagua hao wote ni wananchi sasa je unazijua roho za wananchi tanzania yote watanzania wamecoka na maisha bhana wataweza kuchagua hata jiwe ili mradi tu hao janmmaa wakose huo ulaji wao
 
utafiti unaonyesha kuwa Lowassa anazid kukubalika kadri ya siku zinavyozd kwenda. JE HII NI KWELI?
Mkuu Regan Morgans, kama haya ni matokeo ya utafiti, sasa hii ya wewe kuuliza kama jee ni kweli, unamaana unamashaka na utafiti huu wa Synovate?.

Kwa kusaidia tuu, sio tuu ni kweli kabisa kuwa EL anaanza kukubalika zaidi, bali baadhi ya Watanzania wanaanza kuukubali ukweli kuwa EL ni jembe la ukweli!.

Haya maroroso tunayoyashuhudia katika kuporomoka kwa elimu yetu ni baadhi tuu ya matokeo ya serikali dhaifu ya JK kuitelekeza mipango ya EL na shule za kata ili kumkomoa, sasa imejikuta yenyewe ndio inakomoleka na kufikia 2015, EL atakuwa juu kabisa on top of the charts ili kufungua tuu njia na kunyoosha mapito ya "the chosen one!".

" Jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!".

Yeye ndie ule mwamba wa Kaskazini unaozungumziwa kwenye maandiko mbalimbali kuwa
"Wewe ni mwamba, juu ya mwamba huu, nitalijenga taifa langu!".

Pasco.
 
Hivi mtu unawezaje kuandika habari yooooote hii, na kuweka asilimia zooote hizo, bila kutoa sample space ilikuwa vipi (watu wangapi, kutoka wapi etc) na methodology iliyotumika ( wamepewa questionnaires, wamepigiwa simu etc).

Gazeti lina mhariri hili?

Tutajuaje kama sample space si madarasa mawili ya shule moja ya sekondari yanayojumuisha wanafunzi waliojichokea na kujaza questionnaires randomly kama sehemu ya adhabu ya utovu wa nidhamu?

i like your argument.
 
unwarrated analysis, this time wameinvolve wanasiasa kumi tano DR SLAA amepata asilimia 17% mwaka jana alipopata asilimia 42% walihusisha watu wangapi? kwa mwanahesabu yeyeote kusema percentage za dr slaa zimeshuka kwa 25% ni lazima na mwaka jana awe amehusisha watu 15 ama sivyo rates za mwaka jana na mwaka huu ni uncomparable.
 
Wamejitahidi kuchakachua asilimia za Dr. Slaa wakabakiwa na 17%! Yaani alipopambana na reigning president alikuwa juu, leo hii ashuke! Synovate acheni kutumiwa bana semeni ukweli halisi maana mmejua tofauti na kuonyesha Dr anaongoza wananchi wangewadharau maana huo ndio ukweli ambao hata kipofu anauona.
 
Mods naomba mrekebishe hiyo headline ya threa kwani hailezi chochote. Pendekezo: "Utafiti wa Synovate: Dr Slaa aongoza mbio za urais,
 
Mkuu Regan Morgans, kama haya ni matokeo ya utafiti, sasa hii ya wewe kuuliza kama jee ni kweli, unamaana unamashaka na utafiti huu wa Synovate?.

Kwa kusaidia tuu, sio tuu ni kweli kabisa kuwa EL anaanza kukubalika zaidi, bali baadhi ya Watanzania wanaanza kuukubali ukweli kuwa EL ni jembe la ukweli!.

Haya maroroso tunayoyashuhudia katika kuporomoka kwa elimu yetu ni baadhi tuu ya matokeo ya serikali dhaifu ya JK kuitelekeza mipango ya EL na shule za kata ili kumkomoa, sasa imejikuta yenyewe ndio inakomoleka na kufikia 2015, EL atakuwa juu kabisa on top of the charts ili kufungua tuu njia na kunyoosha mapito ya "the chosen one!".

" Jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!".

Yeye ndie ule mwamba wa Kaskazini unaozungumziwa kwenye maandiko mbalimbali kuwa
"Wewe ni mwamba, juu ya mwamba huu, nitalijenga taifa langu!".

Pasco.

Pasco, unamaanisha Lowasa ni "Yesu"?
 
Mbona mimi sijawekwa wajameni, mbona nakubalika sana jamani... Hahahahaaa

My take: Sijawahi kuwa na imani na hii taasis ya synovate maana ilitumiwa kisiasa 2010!
 
Hivi jamaa ana PHD ya somo gani? Kuna kichaa aliwahi kuandika kuwa Phd hiyo haitambuliki na Tume na haina tofauti na Phd aliyonayo shehe Ponda. Ya kweli haya.

Acha kuongelea ujinga , reply thread hapo juu mkuu, hilo swali watu washalijibu sana au wewe hiyo siyo account yako. post 1400, lakini unaandika utumbo , hiyo kitu waache waulize wageni siyo wewe mkuu.
 
Back
Top Bottom