Synod 2009 na mtizamo wake dhidi ya Afrika

Mitaa michafu ya umasikini haiwezi kuzaa watakatifu...

Kuna ombwe kubwa sana kati ya walionacho na wasionacho ambalo linaendelea kukua kila kukicha,siyo Tanzania tu bali Afrika nzima,wachache waliopata nafasi za uongozi wanazitumia kujinufaisha kwa njia za kifisadi hasa kutoka vyama tawala ambavyo viongozi wake wamejisahau na kuona wanahati miliki ya kutawala mataifa yao,wengi wanatake advantage ya ignorance ya watu wa vijijini ambao kwao vyama vilivyoleta uhuru ndio source ya amani na utulivu,..kwa hivyo kila uchaguzi unapofika hurudisha serikali hizo tawala madarakani,kwao umeme,barabara za lami is not any issue at all.

Nimefurahi baba Askofu Mtega amekumbuka wajibu wao kama viongozi wa dini ,amekiri kwamba hawakufanya kazi yao sawasawa ya kuwahubiri na kuwahudumia kiroho viongozi wa serikali za kiafrika,kitu ambacho ametaka kifanyike mara moja..

Required: Deeper evangelisation, advocacy and prophetic voice to our governments.

Jambo hili ni zuri kwa sababu ninaamini ufisadi hauwezi kuondolewa kwa viongozi wa dini kulalamika ama ndani au nje ya nchi.Kwangu mimi tunapowashutumu mafisadi ni vema pia tukaangalia wajibu wa viongozi wa dini katika kuwaandaa viongozi wetu kiroho maana kama wakiandaliwa vizuri watakuwa waadilifu...

I wish i could have an access to His Holness Mtega and ask him to comeback home for evangelism as he suggested.
 
Hawa wakatoliki ndiyo huwa ni mwanzo wa vurugu duniani nuksi kwelikweli..unajua hao maaskofu kwakuwa hawana "watoto na wanawake" wakishaharibu wanaenda vatican kujificha....wapuuzi wakubwa ni kuwaogopa kama ukoma...we have good examples Rwanda ni wao wame promote tribal war..halafu wakaenda vatican kichaka cha maovu" wajinga tu hao...soon they will be exposed and they will fail.
 
..nadhani mleta hoja amefanya kazi kubwa...lakini ieleweke hadhira aliyokuwa akiongea nayo BABA askofu ni kikao cha maaskofu[kikao cha ndani]...it was not a public adress...

..kama tutaanza kufuatiliana na kuchukua mazungumo ya ndani ya viongozi wa dini au siasa na kuyaleta hapa basi muda si mrefu tutaaribu amani hivihivi...

....chukulia mfano umepata fursa kushiriki kikao cha ndani....na ukachukua mameno yaliyokuwa yanaendelea kwenye mjadala kabla ya maafikiano na kuyaleta nje ..ni lazima yatasababisha usumbufu kwa jamii...
 
Mkuu FM,

Hapana, hii ni African Synod na baada ya kufanyika habari huwa tayari kwenye "public domain" hadi katika intenet.

Kwahio sidhani kama itakuwa ni siri sana.

Ukisoma katika link ifuatayo utapata ni ni kimezungumzwa leo nna maaskofu hawa kutoka Afrika.

http://www.indcatholicnews.com/news.php?viewStory=14995
 
wameficha tangu zamani uchafu wao..lakini sasa wameanza kuonyesha chuki zao kwa jamii ya kiislam waziwazi...after all maaskofu amani hawajali ikiharibika kwasababu hawana familia na wanamakazi yao vatican..there very irresponsible human being....damn
 
Hawa wakatoliki ndiyo huwa ni mwanzo wa vurugu duniani nuksi kwelikweli..unajua hao maaskofu kwakuwa hawana "watoto na wanawake" wakishaharibu wanaenda vatican kujificha....wapuuzi wakubwa ni kuwaogopa kama ukoma...we have good examples Rwanda ni wao wame promote tribal war..halafu wakaenda vatican kichaka cha maovu" wajinga tu hao...soon they will be exposed and they will fail.

>you cant be serious.....tukianza kuchambua nani anastahili matusi yako...tutakesha hapa na wala tusifikie muafaka....

hizu dini tumeletewa na wazungu na waarabu...lakini asili na dini yetu waafrika ni moja ..dini ya mizimu!!!...sioni kwa nini tutoane ngeu au kutukanana....
 
..nadhani mleta hoja amefanya kazi kubwa...lakini ieleweke hadhira aliyokuwa akiongea nayo BABA askofu ni kikao cha maaskofu[kikao cha ndani]...it was not a public adress...

..kama tutaanza kufuatiliana na kuchukua mazungumo ya ndani ya viongozi wa dini au siasa na kuyaleta hapa basi muda si mrefu tutaaribu amani hivihivi...

....chukulia mfano umepata fursa kushiriki kikao cha ndani....na ukachukua mameno yaliyokuwa yanaendelea kwenye mjadala kabla ya maafikiano na kuyaleta nje ..ni lazima yatasababisha usumbufu kwa jamii...

Mkuu Philemon,
Mimi ndiye mleta hoja. Nimeileta baada ya kusoma taarifa mbalimbali za kila kinachoendelea tangu Synod ya waafrika hiyo ianze.

Inabidi nitofautiane na hoja yako kwamba kikao hiki ni taarifa za ndani. Kwa mtizamo wako ni kwamba ni kama vile habari ime-leak.

Hapa si hivyo. Synod hii inaendeshwa kwa uwazi na kila siku taarifa za presenters zinatolewa kwenye website zinazofuatilia masuala ya kanisa katoliki. Ukinisoma vizuri kuna mahala nimesema wanahabari wa hapa nchini hawachangamkii Synod hii wakati wenzao duniani wanagombana kupata kila kinachotamkwa mule.

Hivyo forum mbalimbali zimejadili Synod hii hata kabla haijanza. Kuna wengi walifikia hata Kutania kuwa waafrika hawahitaji Synod wanahitaji shibe. Ni utani lakini inaonyesha inavyojadiliwa. Na imejadiliwa hivyohivyo hadi leo na hadi itakapoisha Octoba 25.

NImeleta hoja hii kwa kuona iweje Ulaya, America, Asia wajadili Synod mitandaoni na sisi tumekaa tu.

Mijadala inafanyika dunia nzima kwa sababu Synod inaendeshwa kwa uwazi kama vile unavyowashuhudia kina Zitto Kabwe bungeni.

Sikupenda kauli ya Kingunge bungeni lakini kwa mawazo yako ina maana hata yeye ilbidi tusubiri bunge limalize kikao ndiyo tuanze kujibu hoja zake. Hapana. Kingunge alijibiwa kuanzia keso yake hadi bunge lilipoisha na hadi alipoita tena kikao kingine pale nyumbani kwake.

Hivyo dunia nzima itaendelea kujadili kila anayetoa mada mle ndani ya Synod. Tuwashukuru Vatican kutoa wazi kila linalojadiliwa kwenye synod kama ambavyo imekuwa kawaida.

Kumbuka Synod wanakribishwa hata wasio wakatoliki na wanashiriki hivyo hakuna chochote cha siri au kusubiri itakapoisha.

Kikubwa ni kwamba tutamsikia Papa akifunga Syno hii na vile vile Papa huchukua muda hata wa iaka kuyatafakari yalyoongelewa kwenye Synod kama hizi iwe ya Waafrika kama hii, ya wamarekani ya Ulaya nk.
 
>you cant be serious.....tukianza kuchambua nani anastahili matusi yako...tutakesha hapa na wala tusifikie muafaka....

hizu dini tumeletewa na wazungu na waarabu...lakini asili na dini yetu waafrika ni moja ..dini ya mizimu!!!...sioni kwa nini tutoane ngeu au kutukanana....
Sijaona sehemu nimetukana kwenye thread yangu...labda unionyesha...nimesema "Maaskofu ni wachochezi siku zote na mifano ipo na sababu kubwa ni kwamba hawana familia.(wake na watoto) so wakiharibu wanakwneda kwenye heaven yao huko vatican....that is facts ..kama unataka tukupe na zingine tutakupa..kwa ufupi jamaa ni waharibifu...wameshindwa kutangaza dini kwa amani wanaanza kutafuta namna ya kugawa jamii kwa minajili ya kidini..shame on the them.
 
Mkuu FM,

Hapana, hii ni African Synod na baada ya kufanyika habari huwa tayari kwenye "public domain" hadi katika intenet.

Kwahio sidhani kama itakuwa ni siri sana.

Ukisoma katika link ifuatayo utapata ni ni kimezungumzwa leo nna maaskofu hawa kutoka Afrika.

http://www.indcatholicnews.com/news.php?viewStory=14995

..ni vema mtu anapoamua kuchukua hoja iliyowasilishwa mkutanoni anaileta hapa ..tungepa rasimu ya yale YALIYOKUBALIWA kwenye mkutano..maana uzefu wangu wa mikutano ni kuwa kila mjumbe anakuja na makali yake....na maoni mengine huwa msimamo mkali ,wa kati au wa kadiri...

sasa sijui mnategemea maaskofu wakikutana wanaongea nini zaidi ya namna ya kuimarisha zaidi dini yao...kama vile masheikh nao wakikutana wanavyojadili namna ya kuimarisha dini zao...
 
Baba Askofu ana maana gani katika maneno hayo ambayo nimehighlight kwa kijani?
Is he saying Islam is a threat in Tanzania? I would like him to substantiate this claim as it might sow seeds (or fertilize them) of mistrusts between Muslims and Christians in Tanzania.

Nimeogopa kidogo kutokana na hiyo kauli maana inasema mengi sana..............................!

hayo ni madai mazito sana kutolewa na kiongozi wa dini. Lakini ni madai mazito kwa sababu yamejumuisha Uislamu na kuchafua amani. Ningependa ayatolee utetezi au ayafute kwani msingi wake ni ujinga. Huwezi kujumuisha Uislamu au makundi ya Waislamu wote na kuwakweka katika kundi moja la kutishia amani na kutaka kufuta Ukristu.
 
Mkuu FM,

Nimekuelewa kabisa "in principal" kwamba hii habari haikupaswa kuwa nje ya RC community na kusambaa kwa wider audience JF ikiwemo.

Lakini siku zote watu ambao ni kioo cha jamii yoyote ile ni lazima kwa namna kubwa tu wawe responsible kwa matamshi wanayotamka na kuwa tayari kwa any consequences.

Pia watoa mada wenzangu nafikiri hii mada hapa si mahala pake.
 
hayo ni madai mazito sana kutolewa na kiongozi wa dini. Lakini ni madai mazito kwa sababu yamejumuisha Uislamu na kuchafua amani. Ningependa ayatolee utetezi au ayafute kwani msingi wake ni ujinga. Huwezi kujumuisha Uislamu au makundi ya Waislamu wote na kuwakweka katika kundi moja la kutishia amani na kutaka kufuta Ukristu.

Maadam hakuna mwana-Synod aliyekana kauli yake basi kauli ile inakuwa ni ya Synod nzima. Aliyeitisha Synod ni Papa Benedict XVI na ndiye atakayehitimisha. Hivyo ni bora kama kuna ambaye hakuelewa basi habari na mjdala huu uwafikie Vatican wajue kuwa kuna nchi moja inaotwa Tanzania imebuka na swali la namna hii. Maana ni Tanzania tu ndiyo ninaona inahoji zaidi wakati Synod ni ya Africa na nchi zote zinaangalia na hilo alilotamka Mtega si issue inayowaumiza kichwa.
 
Mkuu FM,

Nimekuelewa kabisa "in principal" kwamba hii habari haikupaswa kuwa nje ya RC community na kusambaa kwa wider odience JF ikiwemo.

Ingekuwa hivyo isingewekwa kwenye internet kila mwanadunia akaisoma.
Hebu tujiulize. Tunadhani kwamba wanaptamka kauli kama hizi hawajui kwamba zitajadiliwa kama tunavyojadili.

In particular Mtega ambaye ni askofu toka Tanzania ambaye juzi tu ameona jinsi tulivyojadili waraka unaoendelea kujadiliwa hadi sasa.

Mimi naamini kwama wamejiamini vya kutosha na kama ni majibu naamini wanayo. Vinginevyo wangefanya siri na msingejua hata chembe. Si mnaelewa Kanisa Katoliki walivyo maprofesa wa siri kwa jambo wasilotaka mjue!
 
Mkuu Philemon,
Mimi ndiye mleta hoja. Nimeileta baada ya kusoma taarifa mbalimbali za kila kinachoendelea tangu Synod ya waafrika hiyo ianze.

Inabidi nitofautiane na hoja yako kwamba kikao hiki ni taarifa za ndani. Kwa mtizamo wako ni kwamba ni kama vile habari ime-leak.

.

Heshima mbele!!

mkuu waandishi wetu wengi wao wanapenda vya kutafunwa ...vya kunyonga hawaviwezi..nakubaliana na wewe hoja hii inahitaji mijadala..ya kisomi...siunajuwa ni mada ya kisomi...bora wewe umesoma kuliko wanaoanza kupinga au kuunga mkono bila kuisoma..

SYNOD ya afrika ni kikao muhimu ..lakini kwa niwajuavyo maaskofu ...vikao vyote vya kufikia maamuzi yanayoweka mustakabali wa kanisa duniani kote ...huwa off the camera....na hakuna leakage...hadi uamuzi ufikiwe...na hata ukifikiwa ..hufikishwa kwa public muda na wakati waliochagua....ukiona mjadala umefika hadi forum ...basi ujuwe ni mjadala wa kawaida....uamuzi hufikiwa kati ya kikao cha papa na makardinali ......kwa tanzania anayehudhuria ni cardinal pengo...uamuzi unaofikiwa huitwa MTAGASO...na hadi sasa kuna mitagaso mitatu tu[I,II,III]

moja ya maamuzi yaliyosaidia kuimarisha ni mtagaso wa II ambao ni miaka ya 60..ulikubali dini katoliki kufundishwa kwa kutumia local languages[au international languages]...kabla walatoliki wote duniani waliendesha dini KILATINI...kama waislamu wanavyoendesha dini kiarabu...au waisrail ..ki ebrew...

Mtagaso wa iii...ulifanywa miaka ya kati ya utawala wa yohane paul ii.moja ya maamuzi maarufu yaliyofikiwa ni UTAMADUNISHO...yaani kuzidi kuboresha dini ..na mawasiliano..kwa ku localise litrujia ya kanisa..mfano ni kuwa ukienda china wakatoliki wanaendesha ibada kwa lugha yao ....na kuimba na kucheza kwa staili zao,kukaa kwa tamaduni zao[makanisani tunakaa kwenye viti lakini ukienda baadhi ya maeneo wanakaa chini ...kwa kuwa ndio utamaduni wa eneo husika].....lengo ni kuleta dini kwa watu na waimiliki....wataalamu wanasema kuwa kama utaratibu huu wa utamaduni na lugha ungekuwapo wakati wamisionari wa mwanzo wanapeleka dini bara asia...basi kanisa katoliki lingekuwa na waumini wengi asia kuliko kote duniani...kwani ugumu waliopata wamisionari huko china ilikuwa kuwabadili kama mnavyojuwa watu wa asia wanavyoamini tamaduni zao....ilikuwa ngumu kuanza kwanza kuwahubiria,kuwabatiza ,kuwafundisha kilatini...na tamaduni za kanisa za kimagharibi.....hii ilisababisha wamisionari wengi walioenda uchina na maeneo kama hayo kuishia kuchinjwa....laiti wangeiingia kwa namna..inayotumika leo basi....ingekuwa tofauti..

sisi waafrika ndio pekee tumekubali kupokea dini za kigeni tena kwa lugha za kigeni bila resistance ya maana...na hata leo ..bado tuendelee kuamini kuwa MUNGU NI MZUNGU!!??? au MUARABU???
 
Baba Askofu ana maana gani katika maneno hayo ambayo nimehighlight kwa kijani?
Is he saying Islam is a threat in Tanzania? I would like him to substantiate this claim as it might sow seeds (or fertilize them) of mistrusts between Muslims and Christians in Tanzania.

Nimeogopa kidogo kutokana na hiyo kauli maana inasema mengi sana..............................!

Mh Zitto,

Nisingedhani hilo la Askofu lingekuwa la ajabu kwa mtu kama wewe to the extent ya kudemand explanation! - Afterall yeye ni askofu wa kikristo, na pia nadhani anaisemea Africa nzima. Naamini kuwa ma Immam wengi tu wanashinda kuusema ukristo actually hata mwongozo wa waislam unaongea sana kuhusu ubaya wa ukistro! Why make a big fuss about the presentation ya Askofu. Let serious politicians do clean politics! Hivi leo na kesho akiibuka Kakobe, Gamanya, Sheikh Ponda na wenzao na statements kama hizi tutademand explanation toka kwao!
 
HATA WAISLAMU WANAWEZA KUPEWA KITI AU NA HATA UNO...tatizo kubwa ninaloliona kati yao nji UMOJA .....mfano kwa kuwa mecca ipo saudi arabia ....nashangaa kwa nini waislamu wanachelewa kuifanya saudi arabia iwe makao makuu ya uislamu....na wakaunda nchi wakaiita MECCA ...iwe ndani ya saudi kama VATICAN ilivyo ndani ya ITALIA.

WAKIFANIKIWA KUKASIMU UONGOZI WAO kwa kuwa na kiongozi wao mkuu kidunia ...itakuwa rais kujenga umoja wa dini dunia nzima...na sauti yao itasikika zaidi..

suala la mataifa ya kiislamu kukosa umoja ...linamsumbua sana hata ghadafi ..yeye huwaita cowards....[wamarekani wamekalia hadi saudi arabia yenye mecca]......na ndio kisa cha ghadafi kujiegemeza sana upande wa AU......ni baada ya juhudi zake za kutaka umoja miongoni mwa mataifa ya kiarabu ...kukutana na masikio yasiyosikia..

MOD mada za SYNOD tunaomba ziunganishwe...
 
Wakaeneze ukatoliki africa siyo? hakuna la maana wanataka ku-christinize africa...through startegic influence/
wanasaidia nini common man in the street wale waleeeeeeeeee

Kueneza ukatoliki ? Hapana nadhani ukatoliki hauhitaji kuenezwa maana umesha jieneza na kwa namna ama nyingie hata wewe unasaidia kuuneza .Kama unabisha kazi kwako .
 
Wakaeneze ukatoliki africa siyo? hakuna la maana wanataka ku-christinize africa...through startegic influence/
wanasaidia nini common man in the street wale waleeeeeeeeee

Naona mjadala umeshika kasi na watu tayari they are approaching to land to the moon .Watu wameacha hoja za msingi sasa wameanza yao .Lakini ni sawa maan ni uhurun wa mawazo .
Tumaini usiogope sana kwamba Ukatoliki utaenezwa mbona una enea tu na wewe unasaidia kuuneza ? Ukatoliki upo na watu hawaupiganii hapana . Naomba kuuliza ama nataka uangalie mwenyewe .Tukivuka mwaka vyema popote utakapo kuwa utashuhudia makelele kial kona ya Dunia juu ya Feb 14 eti siku ya wapendanao . Basi hata waislam utakuta tumo kusherehekea kwa bidii . Ile si siku ya wapendanao ni siku ya Wakatoliki . Waroho wa pesa wamewazuga kwaba ni Valentine Day lakini who was Valintine ?

He was a roman Catholic Priest aliye wekwa gerezani kwa kuwafungisha watu ndoa huku mtawala wa kirumi akiwataka vijana kuingia jeshini ili akapigane kuitwaa Ulaya .Fr. Valentine was against the idea na akawa anawataka watu waishi maisha yao kama wanavyo amua . Kwa kifupi ukatoliki upo na kwenda kuanzia AU . Tungojee tuone siku St. Valentine nenda kanisani siku hiyo utasikia anatajwa na ibada itakuwepo .

Nimetoa mfano kwa ufupi ili ujue kwamba mengi hufanywa lakini ni mila za wakatoliki na hata waislam wanafuata . Ukibisha nitaleta ushahidi uone ninacho kisema.

Turudie hoja .
 
mimi binafsi naogopa sana TZ tunapoelekea kuhusu udini..cha muhim tusiingizwe kwenye siasa za western countries na udini..leo mmarekani anampinga afghanstan na talleban ambae anamuita terrorist lakini ndo huyo alimuezesha kinguvu za kijeshi wakati wa kuibomoa soviet union....
iran na USA hawapatani lakini iran huyohuyo anafanya biashara na Russia...
USA ame force nchi za Africa kuingiza terrorst Legislation katika nchi zao, ambazo kweli zinalinda maslahi yao
hebu niambieni maana ya Terrorist ni ipi?
je terrorist ni yule ambae ni anti USA?
 
Back
Top Bottom