Symbion Power acquires DOWANS Power plant

Chairman wa hii kampuni ni Amb Wilson kama mna mkumbuka aligombana na serikali ya Bush kuhusu Iraq baada ya mke wake kutajwa jina waziwazi kwamba anafanya kazi USA. Inawezekana wamepewa pesa za misaada ya USA kwa kusaidia nchi masikini na wameona badala ya kutoa pesa kwa Tanzania ni bora watoe kwa kampuni ambazo zinasaidia Tanzania. Mimi nahisi pesa ya hii mitambo imetoka kwenye fund ya kusaidia Investment za Africa. Obama ameamua kutumia mbinu tofauti badala ya kutoa pesa.

Symbion Power
 
Ni lini wataiwasha na je bei ya umeme watayowauzia TANESKO itakuwa sawa na ya Dowans wenyewe? Akaambiwa kwamba mkataba wao Symbion ni siri na muuzaji hivyo bei waliyonunulia hawawezi kuitaja. Kuhusu bei ya umeme itayouziwa TANESKO wamesema itakuwa poa na kwamba wataitangaza Jumatatu wanapotarajiwa kuwa na mkutano wa pamoja na kampuni hiyo. Kwa sasa wamesema wako tayari kuwasha umeme ila wanangoja treni la gesi la Songosongo lililoharibika lianze kazi na wao hawana noma wala nini na mambo ya siasa kwao hayana nafasi bali ni kazi tu na blah blah pembeni.

Baada ya taarifa kwenye vyombo vya habari kuhusu ununuzi wa mitambo ya Dowans. Kampuni ya kimarekani ya Symbion Power yenye makao yake makuu Washington DC, leo imethibitisha kwamba imekwisha weka sahihi mkataba wa ununuzi wa mitambo hiyo iliyopo Ubungo Dar es Salaam.

Paul Hinks, Meneja Mtendaji wa Symbion amewaambia wanahabari sasa hivi katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski kuwa, "mazungumzo na Dowans yalikuwa ni magumu hasa ukizingatia historia ya mradi wenyewe. Kwa hiyo ilibidi kufanya uchunguzi wa kina kujiridhisha na kila kipengele cha makubaliano na pia ubora wa mitambo na tumejiridhisha kuwa mitambo hii iko katika hali nzuri ya matunzo".

Hinks aliendelea kusema "nafarijika kusema kwamba sasa tumemaliza na kukamilisha mkataba wetu na Dowans na tupo tayari kuzalisha umeme hapa nchini. 120MW inaweza kusaidia kupunguza matatizo ya umeme hasa ukizingatia kuwa nchi inakabiliwa na tatizo kubwa la mgao wa umeme. Lakini, laiti kama TANESCO haitaafiki, tuna miradi mingi duniani ambayo inahitaji mitambo hii.

Mwasisi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power LLC, Paul Hinks, akiongea na wanahabari sasa hivi hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Symbion Power Africa, Balozi mstaafu Joseph Wilson
"Pamoja na ukweli kwamba tunauwezo wa kuitumia mitambo hii pengine duniani, Symbion inakusudia kupendekeza kwa TANESCO waridhie mitambo hii itumike hapa nchini. Mitambo hii imefanyiwa majaribio hivi karibuni na wataalamu wa kimataifa na imedhibitika kuwa iko katika hali nzuri sana na inaweza kuanza kutumika ndani ya muda mfupi sana kwa mategemeo ya kiwango cha hali ya juu", alisema.



Hinks pia kafafanua kwamba Symbion itashirikiana na kampuni ya Kimataifa ya kimarekani ya ProEnergy Services (PES) ambayo inauwezo na uzoefu mkubwa katika sekta ya umeme yenye makao yake makuu Missouri, Marekani. PES ambayo inajishughulisha na uzalishaji wa umeme sehemu mbalimbali duniani itakuwa ni mbia wa kutoa huduma ya uhandisi na uendeshaji wa mitambo.

Amesema Symbion Power tayari inauzoefu mkubwa katika miradi ya umeme ambayo inafadhiliwa na Serekali ya Marekani kama vile yale yaliyo chini ya Millenium Challenge Corporation. Symbion pia inashughulika na usambazaji wa umeme vijijini Tanzania inayojumuisha takriban kilometa 3,000 ya miundombinu ya kusambaza umeme.

Wakati huo huo, mwenyekiti wa Symbion Africa, Balozi mstaafu wa marekani katika nchi mbalimbali, Joe Wilson, alisema mitambo tuliyoinunua iliyoko Ubungo, imekaa bila kutumika takriban miaka mitatu sasa, wakati nchi imekuwa ikipata matatizo makubwa ya mgao wa umeme inayoleta changamoto katika uchumi wa nchi. Kwa niaba ya bodi ya wakurugenzi ya Symbion, nasema tutafarijika ikiwa TANESCO itahitaji huduma kutoka kwetu".

Symbion ni kampuni ya Kimarekani yenye makao yake makuu Washinton DC Marekani. - www.symbion-power.com

 
kila rais na dili zake.

inavyoonekana katika miaka yake 10 ya uongozi, kikwete amejikita zaidi katika dili za umeme, mgawo, madini, dowans, richmond you name it.
 
Je kama hawa Symbion wamenunua hiyo Dowans, Je lile faini lililotakiwa tuwalipe Dowans litakuwa limefutika au bado liko palepale? RA bado anacheza karata zake hata mkimfukuza chamani kwenu!! Wadanganyika kumbukeni RA ndio mwenye power of attorney ya Dowans kwahiyo hawa symbion walikuwa wanafanya biashara na RA; imekula kwetu hiyo!!
 
Unajua sisi watanzania ni watu wa kuhurumiwa, hii mitambo badala ya kuinunua wenyewe, tumeingiza siasa badala ya kufanya mazingira kuichukuwa na kuwa mali ya serikali sasa tunaiacha iuzwe kwa mzungu ili atuuzie huku akiweka bei anayotaka. Sisi siasa zinakotupeleka siko nawaambia kila kukicha tunafanya makosa yaleyale!!! sio watu wa mipango, sio watu wakufikiri yajayo, hatutaki kujifunza kutokana na yaliyotupata nafikiri tunamatatizo makubwa ya kiakili, kifikra na ujanja wa kufanikiwa umetupitia kushoto sana!!!!!!:A S angry:
 
Inaelekea Symbion Power ina uzoefu mkubwa katika kujenga miundo mbinu ya kusambaza umeme lakini hawana uzoefu wowote katika uzalishaji. Kununua DOWANS na sehemu tu ya matumizi ya faida wanaoipata kwenye miradi ya MCC waliyonayo hapa Tanzania.
 
Haya sasa sijui vita yetu ya ufisadi itasaidiwa na nani kama usa nao wameingia kununua mitambo yenye harufu ya ufisadi!
Napata hisia kuwa rushwa hizi kubwa zinafadhiriwa na mataifa haya makubwa! Juzi hela za rada wanatupangia kwa kupeleka,leo tena hivyo ahaaa!
 
Inaonekana sekta ya kuzalisha umeme Tanzania inapendwa na makampuni yanayoongozwa na waliopitia ktk masuala ya ulinzi na usalama. Dowans Ali Hadaiwi alikuwa brigedia wa jeshi la Omani akishikilia masuala ya ulinzi wa Sultani wa Omani.

Hawa Symbion Power viongozi wake wa juu mmoja ana nishani ya kutukuka kwa ujasiri wake wa kutumikia vikosi maalumu vya Uingereza na mwingine alikuwa mshauri wa masuala ya usalama ktk baraza la ulinzi huko USA.

Overview

Progress through partnership.

Symbion Power was built on a foundation of partnership and cooperation. Even our name – a derivative of the word Symbiosis – reflects the cooperative relationship we maintain with key suppliers, local partners and subcontractors.
Balancing Progress and Security.

With considerable experience working in the dangerous environments of Iraq and Afghanistan, Symbion brings a unique methodology to every project. Our experienced security teams and our engineers work hand-in-hand with our clients to make careful judgments that facilitate both progress and safety.
We draw extensively on the experience of our partner Hart Security Limited.
Nothing is more important than the health, welfare, and safety of our staff, our partners, our subcontractors, and the people that make our work possible.
Always Ready to Adapt.

At Symbion, we understand that circumstances on the ground can change quickly. That's why we've built a dynamic organization that is always ready to adapt.
In the United States, Europe the Middle East, Africa and Asia we've built lasting relationships. We've partnered with manufacturers for equipment-specific training through Symbion Power Centers, our own training schools, in northern Iraq and Kabul, Afghanistan. A training school will be established in Tanzania in 2011. We understand that our success and our progress are inextricably linked, and we take great pride in our work.
A U.S. Company with a World of Experience.

The Symbion management team has extensive experience in the design, engineering and the procurement and construction of complex international electricity projects. Their combined experience covers work in the United States, Africa, the Middle East, Europe and Asia and Australia.
Symbion has partnering agreements with major manufacturing and contracting companies, including one of the world's leading equipment suppliers, Alstom Grid, for substation, power, transmission and distribution projects. In Tanzania Symbion is partnered with leading US transmission and distribution contractor Pike Electric Inc.
Symbion is a U.S. company with offices and subsidiaries in Washington, D.C.; Delaware, USA; Limassol, Cyprus; Cape Town, South Africa; Dubai, U.A.E.; Baghdad, Iraq; Erbil, Kurdistan; Port-au-Prince, Haiti; Dar es Salaam and Morogoro, Tanzania.

Leadership:

Chairman Symbion Power Holdings

richard-westbury.jpg

Lord Richard Westbury MBE
Lord Westbury had a distinguished military career as an Officer in the Scotts Guards and for the British Special Air Services (SAS). A pioneer of the security industry, Lord Westbury was formerly the Deputy Chief Executive of The Leadership Trust and the Chief Executive Officer of Defense Systems Limited (DSL), one of the earliest and most successful international security companies headquartered in London. He is the founder and chairman of Hart Security.

Chairman, Symbion Power Africa

joseph-wilson.jpg

Ambassador (ret.) Joseph Wilson
Ambassador (ret.) Joseph Wilson serves as the Chairman of Symbion Power, Africa. Ambassador Wilson has extensive experience in Africa, the Middle East, and Europe. As an American diplomat, he served as Ambassador to Gabon and Sao Tome and Principe in the administrations of Presidents George H.W. Bush and Bill Clinton. He also served as Special Assistant to President Clinton in charge of African Affairs at the national Security Council. In addition to Gabon and Sao Tome and Principe, Ambassador Wilson also served in Niger, Togo, South Africa, Burundi, and Congo (Brazzaville).

Source: Symbion Power
 
M k w e r e anajaribu kila mbinu kuhakikisha Kampuni yake ya Dowans wanalipwa. Hivi pale walipoweka mitambo yao wanalipia? Je kama dowans imekufa inakuwaje tena mitambo ile ile ilipiwe tena na wale wale waliokataa mwanzo?

M k w e r e hana nia ya dhati kukabili head on tatizo la umeme kwa sababu ni mfaidikaji.
 
naomba mungu lisije likawa tego jingine hilo, maana nikisikia tanesko,dowans,richmond nachan'ganyikiwa!!!!
 
Hawa wakubwa hawachoki na huu uchuuzi? kila kukicha wameuza kampuni kwa huyu, mara yule. Sasa wameamua kuwauzia wanajeshi!!!
 
Naona na kazi za ukorokoroni tutapatiwa huko Iraq na Afghanistan ili wastaafu wa kutoka majeshi yetu TZ wajiongezee pensheni.

''We've partnered with manufacturers for equipment-specific training through Symbion Power Centers, our own training schools, in northern Iraq and Kabul, Afghanistan. A training school will be established in Tanzania in 2011. We understand that our success and our progress are inextricably linked, and we take great pride in our work'' - www.symbion-power.com.
 
Kampuni ya symbioni power imenunua mitambo ya dowans. Wana mpango wa kuingia mkataba na Tanesco ibaki nchini. Wanadai wamefanya uchunguzi wa kutosha na kuona mitambo inatunzwa vizuri. Wamepitia pia mchakato wa namna mitambo ilivyo ingizwa na hawahusiki na historia ya nyuma ya mitambo hiyo. Nahisi wataendelea kunukia kidowans dowaans. Habari cten
 
Back
Top Bottom