calmdowndear
JF-Expert Member
- Jul 12, 2011
- 605
- 273
So amechukua cheo Cha Judith Mutawali
Uteuzi huu unaenda sambamba na saga za EAC na uozo uliobainika kwa wahamiaji haramu hususan Banyarwanda, TISS hapa wamewajibika vema kutazama the root cause ya hii kitu.
mtuwekee cv yake.asije akawa anatoka mlima mulenge
ndio huyo huyo mkuu alikuwa mtu wa mission town haina mfanoMkuu, huyu Chemundugwao si alikuwa anashinda kutwa pale posta mpya na kanisa la St Albans au YMCA?
Nafikiri hizi zote zilikuwa ni kona zake za kukutana na wateja wa passport maana zilikuwa ni karibu na Mambo ya Ndani na tokea Uhamiaji ipelekwe Kurasini biashara si itakuwa ngumu kidogo kwenye usafiri?
10. Toa nafasi –Wape nafasi wasomi waonyeshe ujuzi wao, wape nafasi wakomavu waonyesha uwezo wao, wape nafasi waadilifu wadhibiti mianya ya rushwa,wizi na ubadhirifu wa mali ya umma.
Mwisho uiombe Serikali ikupatie fungu la kutosha kwa ajili ya kupanga safu yako (timu ya ushindi) ili kupata "Big result now" ikibidi "review organization chart" kwani taasisi nyingi za umma muundo wake wa kiutawala ni mbovu hivyo inapelekea utendaji na utekelezaji wa majukumu kuwa mgumu, nakutakia kila heri katika kutumikia majukumu yako mapya ya kazi.
Ninamfahamu kidogo huyu Ambokile.....Na hapa ndo panaponipa wasiwasi. Ni kweli huyu bwana anaijua Uhamiaji? Ni kwamba Ambokile inaaminika tangu aingie Uhamiaji hajawahi fanya kazi nje ya Dar es salaam......yaani baada ya kutoka Dar ni moja kwa moja London. Anajua kimsingi Idara hii inamatatizo gani kiutendaji mipakani, mawilayani hadi mikoani? Isije kuwa ni tatizo lile lile kama la Ulungi ambaye pia hakuwa na 'experience' yoyote na mikoani.
Hawajawahi kusema Uhamiaji inaongozwa na Cadema? Maana siku hizi kila uchaga unaunganishwa na Chadema hata ukiwa ndani ya CCMMagnus Ulungi alikuwa kama boya pale, ngoja aje huyo pengine ataondoa ule utando a wachaga waliojaa HQ kwa kujifanya wao ndio wamesoma peke yao na kwamba wengine elimu zao wazitumie Tandahimba, Kazulamimba, Nampembe na Chwaka
Poor Ulungi alikuwa amewekwa mfukoni na vilaza Shayo, Mongi Kishe & Co.
Hawajawahi kusema Uhamiaji inaongozwa na Cadema? Maana siku hizi kila uchaga unaunganishwa na Chadema hata ukiwa ndani ya CCM
Mkuu JamboJema,
Kuijua Uhamiaji mpaka ufanye kazi mikoani?
Ambokile amefanya kazi Uhamiaji hapo makao makuu, Airport, TIC na kwa miaka minane sasa kama Mwambata wa Uhamiaji London. Kipindi chake cha kukaa London kimeongozana na kipindi ambacho Uhamiaji imekuwa issue kubwa kwa hizi nchi za West na hivyo kushirikiana kwa karibu sana na nchi zetu katika kupambana na suala la Wahamiaji haramu. Kwahiyo Ambokile amefaidika na mafunzo na uzoefu ambao utamsaidia sana nyumbani kama ataungwa mkono na wenye nchi.
Lakini pia Ambokile amezaliwa na kukulia Kyela ambako ni mpakani na suala la Uhamiaji sio geni kabisa. Ana Elimu yake nzuri tu ya Bachelor ya UDSM miaka ya 80 na baadaye Masters ya UK.
Kikubwa ni mchapa kazi mzuri na pia ni binadamu kwa utu. Binafsi ninaamini kama wenye nchi Watamuunga mkono basi kuna faida kubwa kwa Ambokile kupewa hiyo nafasi maana hajachafuka na madudu ya Uhamiaji kwa miaka kumi iliyopita. Yeye anakuja kama mtu aliyetoka nje ya Uhamiaji. Na hapa duani ukitaka kufanya mabadiliko ya kweli basi lete mtu toka nje ya organisation.
Mafanikio makubwa mkuu Ambokile. Uzuri matatizo yote ya Uhamiaji unayajua vizuri maana tumeyaongelea mara nyingi sana. Sasa ni kujaribu kuweka kwenye vitendo solutions mbalimbali na kuikoa nchi yetu kutokana na majanga mbalimbali ya Wahamiaji haramu na matumizi mabaya ya passports zetu.
Wish you all the best.
Ungekuwa unasimamia hoja bila kusukumwa na ushabiki kama hivi tungekuwa mbali sana ktk kutokomeza udhalimu hapa nchini.asante mh. kwa hili, uhamiaji haramu ni tatizo kubwa san ahapa nchini, tulifanya kama pripirity, fukuza wote tuanze mojs kama vile ndio tanzania imepata uhuru wake
Toa MaDCI JNIA, KIA, HQ, Namanga waliojazana wakigonga mihuri, kazi ambazo wanapaswa kufanya kazi Mawilayani kama MaDIOs na wakihamioshwa bado wanahonga utumishi na kurejea vituo vya awali,
Matokeo yake mawilayani wakuu wa Uhamiaji huko ni maafisa wanaokaimu wenye vyeo vidogo, Ambokile ukifika ofisini omba orodha ya MaDIOs wote na uombe wakwambie waliothibitishwa na wanaokaimu nafasi hizo na ni kwa muda gani wamekaimu, na je nafasi hizo zinapaswa kushikiliwa na maafisa wa kuanzia vyeo gani?
Kiukweli maafisa wanaopaswa kushika nafasi za wilaya wengi wakipangiwa hawaendi wamejazana ktk vituo vyenye neema kama KIA, Namanga, JNIA, Tunduma, Makao Makuu ila mawilayani hawataki kwa sababu huko maporini hakuna maslahi kwao. Ambokile timua vibabu vyote katika vituo hivyo.
Kuwa makini na Maafisa kadhaa ambao huamua nani afanye kazi wapi? Wao huhakikisha watoto, wajukuu, mashemeji na wapambe wao wanaendelea kufanya kazi katika vituo nilivyovitaja na wengine wasiowajua wakibaki maporini na kustaafia huko,
Ambokile fanya kazi bila woga, usiwe na upendeleo safisha Uhamiaji yote
Nawasilisha